Papa Francisko amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech Petr Fiala
Wakati wa Mkutano wao Alhamisi tarehe 9 Juni 2022 mjini Vatican, wameonesha uhusiano mzuri uliopo kati yao Vatican na Jamhuri ya Czech na juu ya nafasi ya Kanisa katika jamii. Walizungumzia pia juu ya matarajio ya mshikamano na ushirikiano zaidi. Hawakukos kujadili juu ya masuala ya vita nchini Ukraine vinavyoendelea na matokeo yake kwa ngazi ya Kikanda, na Kimataifa kwa namna ya pekee umakini wa hali halisi ya kibinadamu na mapokezi ya wakimbizi. Hata hivyo akiwa na Baba Mtakatifu wamebadilishana kama kawaida ya ziara hizi rasimi zawadi zao.
Kwa upande wa Baba Mtakatifu kwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Czech: Kigae cha shaba kinachoonesha Mtakatifu Martin, ambaye anawalinda maskini akimpatia sehemu ya joho lake. Hati za Kipapa muhimu kama vile :Ujumbe wa Amani wa mwaka huu 2022. Hati juu ya Udugu wa Kibinadamu; Kitabu cha Statio Orbis cha tarehe 27 Machi 2020, kilicho tayarishwa na LEV.
Wakati huo huo zawadi kutoka kwa Waziri Mkuu wa Czech kwa Baba Mtakatifu ni: Biblia yenye nuru; Kitambaa kilichopambwa na wanawake wa Kicheki na Kiukreni; Kitabu cha Kanisa la Cheki kuhusu Mwaka wakfu kwa ajili ya Mtakatifu Ludmila.