Papa Francisko amekutana karibu na watoto 160 wa Treni ya watoto
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wadogo wa toleo la nane la "Treni ya Watoto", tukio lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni ikiwa ni sehemu ya mpango mpana uitwao: "Cortile dei Gentili" yaani Mkutano wa Watu wa Mataifa Jumamosi asubuhi, tarehe 4 Juni 2022 kwenye Uwanja wa Mtakatifu Damasi wa Jumba la Kitume, Vatican. Watoto hao wamesindikizwa na baadhi ya watu wazima na baada ya salamu za Kadinali Gianfranco Ravasi, Mwenyekiti wa Baraza hili, Antonio Organtini, mkurugenzi mkuu wa taasisi ya usaidizi ya Mtakatifu Alessio-Margherita wa Savoia huko Roma inayotembelewa na watoto, na Massimiliano Giansanti, Rais wa Shirika la kilimo la Italia, linalowakilisha na kulinda kampuni zinazohusiana na taasisi na hutoa habari na huduma na ambaye anashirikiana katika tukio hilo, wamekuwa ni watoto waliozungumza na Papa, na kumwuliza maswali waliyo nayo mioyoni mwao kwa uwazi na wakati mwingine, kupendekeza kitu kwake.
Kwa mtoto aliyetaka kujua nchi gani alizotembelea maskini na viongozi wake zimeweza kuboresha hali zao, Papa amejibu kuwa: “Nitakuambia jambo moja: kila nchi ina upekee wake na ninashangaa ni sifa gani tajiri zaidi ya nchi. Na unajua ni sifa gani tajiri zaidi ya nchi? Watu. Siku zote watu ni watu, wanafanana katika hatua fulani, lakini kila mtu ni tofauti, ana mali yake mwenyewe, na kinachonishangaza ni kuona jinsi watu mbalimbali walivyo matajiri na utajiri maalum kwa nchi hiyo. Hapa pia, kati yenu: kila mmoja wenu ana mali yake mwenyewe, utajiri wa nafsi yake, kwa sababu moyo wa kila mmoja wetu, nafsi ya kila mmoja wetu si sawa na mwingine: hapana! Hakuna mioyo sawa, hakuna nafsi sawa: kila mmoja wetu ana mali yake mwenyewe na hii pia inahesabika katika kila nchi. Katika nchi ninayotembelea, daima nimeona utajiri maalum: hii ni njia, na hii ni uzuri wa kazi ya uumbaji. Pia ni lazima tuone hili katika kila mmoja wetu. Ikiwa tunajifunza kuona watu kwa moyo, kuangalia kwa moyo, kujisikia kwa moyo, kufikiri kwa moyo, tutapata mali hii ya kila mtu, ambayo ni tofauti na kila mmoja, daima ni mzuri na tofauti. . Inaeleweka?
Akijibu swali la mwingine kuhusiana na anavyojisikia kuwa Papa, amesema: “Jambo la muhimu, katika taaluma yoyote ambayo maisha yanakuweka, ni kwamba usiache kuwa wewe, na utu [wako] mwenyewe. Ikiwa mtu kuwa mahali pamoja, au ikiwa maisha yamemweka mahali hapo, anabadilisha utu, yeye ni mtu bandia, na hivyo anapotea. Ni lazima kila wakati tuhisi mambo yanapokuja, kwa uhalisia: kamwe, usifiche hisia. Kwa hivyo ninajihisije kama Papa? Kama mtu, kama kila mmoja wenu katika taaluma yake, katika kazi yake. Kwa sababu mimi pia ni mtu kama wewe na ikiwa nina kazi hii lazima nijaribu kuifanya kwa unyenyekevu na zaidi kulingana na utu wangu, bila kujaribu kufanya mambo ambayo ni mageni kwangu. Kwa mfano, nakuuliza: “Unajisikiaje, wewe au ndugu yako pacha, anajisikiaje? "Ninahisi hivi". Hii ni muhimu si kuipoteza. Pia, mtu anapokuwa mkubwa kisha anapewa majumu kama haya, kazi hii na nyingine, usisahau kuwa wewe ni mtu huyo, na usipoteze hisia hiyo.
Papa Francisko aidha ameongeza kusema “Kujibu swali lako: je, ninajisikiaje na kazi hiyo, na huduma hii kama Papa? Ninajaribu kuwa mimi mwenyewe, sio kuchukua nafasi za bandia. Sijui kama hii itakusaidia wewe.
Mtoto mwingine aliuliza:"Je, inachosha kuwa Papa?" Baba Mtakatifu alisema, Mungu anatoa nguvu za kubeba juhudi zake mwenyewe na ni lazima tutekeleze kwa uaminifu, unyofu na kazi. Hata hivyo wakati wa maswali, Baba Mtakatifu alisisitiza jinsi ilivyo muhimu kukumbuka Mungu yuko pamoja nasi, na hisia hiyo ya kulindwa na Bwana, inatusaidia. Jambo baya, alionya, ni wakati hatutaki kuhisi Bwana kuwa karibu na na kuchagua umbali. Siri kubwa ni kuhisi Bwana kuwa karibu. Na hii inasindikiza katika maisha yote."
Mtoto mwingine alimwambia Papa amwombee na Papa akajibu: “Alichosema Ludovica ni kizuri: "Niombee". Ni jambo ambalo tunapaswa kuambiana kwamba waombee kila mmoja wetu. Kwa sababu kuomba kwa ajili ya mmoja wetu ni sawa na kuvuta macho ya Mungu kwetu. Maombi ni kuvutia macho ya Mungu, unapoomba, Mungu anakutazama. Na ulichoomba ni kitu kizuri. Pia unawaombea wengine, unajua? Wewe niombee na mimi nitakuombea, na uhusiano huu wa kuomba maombi ni uhusiano wa udugu, wa urafiki, wa watu wawili au watatu wanaomwomba Mungu awaangalie. Kuomba ni kuvutia macho ya Mungu kwetu, na hii ni nzuri.”