Papa awakumbuka wafiadini 27 wa Hispania waliotangazwa wenyeheri
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amefafanua ushuhuda na kielelezo kilichotolewa na wafiadini 27 wa Shirika la Wadominikani, waliotangazwa kuwa Wenyeheri huko Seville nchini Hispania, ambapo amesema, wanatuonesha njia ya utakatifu. Hawa ni wenyeheri wapya waliotangaza Jumamosi, tarehe 18 Juni 2022. Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana Dominika 19 Juni, Papa Francisko amesema kwamba hata katikati ya ukatili ulioashiria na Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Uhispania, hapakuwa na uhaba wa mifano ya imani dhabiti. Papa alitaja majina ya baadhi ya wanaume na wanawake ambao, alisema, “waliuawa kwa kuchukiwa imani wakati wa mnyanyaso wa kidini yaliyotukia nchini Hispania katika pambano la vita vya wenyewe kwa wenyewe vya karne iliyopita.
Ushuhuda wa kushikamana na Kristo
Papa amesema kwamba "Ushuhuda wao wa kushikamana na Kristo na msamaha kwa wauaji wao unatuonesha njia ya utakatifu na kututia moyo wa kufanya maisha kuwa toleo la upendo kwa Mungu na ndugu na dada zetu.” Watawa hao kutoka katika shirika la Wadominikani aliwakumbuka ni pamoja na “Angelo Marina Alvarez na wenzake kumi na tisa; Giovanni Aguilar Donis na wenzake wanne kutoka Shirika la Wahubiri Ndugu; Isabella Sanchez Romero, mtawa mzee kutoka Shirika la Mtakatifu Dominiki; na Fructuoso Perez Marquez, chuo kikuu cha Kidominikani. Kwa kuhitimisha Papa aliomba kuwapigia makofi wenyeheri wapya.
Kutangazwa kwa wenye hri, Misa iliyoadhimishwa na Kardinali Semeraro
Wakati wa Ibada ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa katika Kanisa Kuu la Seville na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu, alikumbusha na kufafanua juu ya mashahidi hawa kuwa ni “Umati wa watu waliofua mavazi yao katika damu ya Mwanakondoo. Kardinali Semeraro alisema Wenyeheri wetu wapya walikuwa watu tofauti sana katika suala la tabia na historia za kibinafsi. Na “Walikuwa sawa, hata hivyo, karama ya Mtakatifu Dominiki ilikuwa chaguo la kitaaluma ambalo waliliishi kwa uaminifu, uthabiti, ukarimu. Katika Misa ya tarehe 18 Juni 2022 imefikisha pamoja jumla 2,112, ya wafiadini Wakatoliki waliotangazwa kuwa wenye heri au kutangazwa watakatifu katika tukio hilo la Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe vya Uhispania ambavyo vilishuhudia makanisa 2,000 yakiharibiwa na hadi makasisi 8,000 kuuawa, pamoja na makumi ya maelfu ya Wakatoliki walei.
Kardinali akiendelea na mahubiri yake alisema hata katika Injili Takatifu iliyosomwa kwamba “Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, mimi nami niliwatuma hao ulimwenguni”. Injili lazima itangazwe zaidi ya yote kwa njia ya ushuhuda wa udugu na umoja. Katika Wosia wa Evangelii Nuntian wa Mtakatifu Mtakatifu Paulo VI alifafanua vizuri sana kwamba “ Mkristo au kikundi cha Wakristo, ndani ya jumuiya ya wanadamu wanamoishi, wanadhihirisha uwezo wa kuelewa na kukubalika, ushirika wa maisha na hatima na wengine; mshikamano katika juhudi za wote kwa yote yaliyo adhimu na mema”. Kwa maana hiyo hapa pia ni kuangaza, kwa njia rahisi sana na ya hiari, imani katika maadili fulani ambayo ni zaidi ya maadili ya sasa, na matumaini katika kitu kisichoweza kuonekana, na ambacho mtu hawezi kuthubutu kufikiria. Kwa hivyo kwa ushuhuda huu usio na neno, Wakristo hawa wanazua maswali yasiyoweza kukita ndani ya mioyo ya wale wanaowaona wakiishi: kwa nini wako hivi? Kwa nini wanaishi hivi? Nini au nani anawatia moyo? Kwa nini niko kati yetu? Vema, ushuhuda kama huo tayari ni tangazo la kimya kimya lakini lenye nguvu sana na lenye matokeo la Habari Njema» ( Evangelii Nuntian 21).