Papa anatoa wito wa mazungumzo ya maisha na Makanisa ya Kiorthodox ya Mashariki
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Tume mchanganyiko ya Kimataia ya majadiliano ya kitaalimungu kati ya Kanisa Katoliki na Makanisa ya Kiorthodox ya Mashariki, Alhamisi tarehe 23 Juni 2022 jijini Vatican. Papa Francisko akianza hotuba yake ameongozwa na maneno ya kifungu cha Barua ya Mtakatifu Paulo yasemayo: “Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu(1 Cor 1,3-4). Amewashukuru kwa uuwepp wap na kazi yao msingi, na kufurahi kukutana nao baada ya miaka mitatu tangu walipokutana nao katika mkutano wao wa mwisho. Amepongeza hotuba na maneno ya Askofu Kyrillos aliyomwlekea. Baba Mtakatifu amebainisha jinsi ambavyo wako wanakaribia kuhitimisha utafiti muhimu kuhusu Sakramenti, hati ambayo inajionesha kuwa kubwa kwa maana na ambayo kwa msada wa Mungi inaweza kutoa hatua mpya ya mbele kuelekea muungano kamili. Katika muktadha huo, Papa ameongozwa na mambo matatu mafupi ambayo amependa kushirikishana nao.
Ya kwanza Uekuemeni ni msingi wa ubatizo. Ni katika ubatizo ambao unapatikana msingi wa umoja kati ya Wakristo na hamu ya umoja kamili unaoonekana. Shukrani kwa Sakramenti hiyo ambayo tunaweza kuthibitisha na Mtume Paulo kuwa sisi sote tulibatizwa kwa njia ya roho moja na mwili mmoja” (1Kor 12,13). Katika mwili mmoja kuelekea utambuzi wa kweli wa Sakramenti msingi ambayo ni muhimu ili kufikia kukiri pamoja na Mtume Bwana mmoja , imani moja na ubatizo mmoja (Ef, 4,5).
Jambo la pili ni kwamba uekumene daima unatabia ya kichungaji. Kati ya makansia ambayo yanashirikisha mfuasi wa Mtume , kuna maana kubwa inayoonekana ya Tume yao, si juu ya Ubatizo tu lakini hata kuhusu Sakramenti nyingine, ambazo zinapaswa kutia moyo wa tafakari ya kina ya uekumene wa kuchungaji. Katika maana hiyo hata kuwa na muungano kamili, ambapo tayari zimetiwa saini za makubaliano ya kichungaji kwa baadhi ya Makanisa ya Kiorthodox ya Mashariki ambayo yanaruhusu waamini kushiriki katika zana za neema (Unitatis redintegratio, 8). Papa amefikiria kwa namna ya pekee, Waraka wa Pamoja uliotiwa saini mnamo 1984 na Papa Yohane Paulo II na Patriaki Mar Ignatius Zakka I Iwas wa Kanisa la Siro- la Kiorthodox wa Antiokia ambayo kwa hali fulani inawapatia waamini mamlaka ya kupokea sakramenti za Kitubio, Ekaristi na Mpako wa Wagonjwa katika jumuiya moja au nyingine.
Papa pia amekumbuka makubaliano mengine kuhusu ndoa mchanganyiko iliyohitimishwa mnamo 1994 kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiothodox la Siro la Malankar. Hayo yote yamewezekana kwa kutazama hali halisi ya watu na wajumbe wa watu wa Mungu na wema wao , ulio mkuu zaidi ya mawazo na mambo mengine ya kihistoria. Kimsingi hakuna anayeachwa na kukosa nyenzo za neema. Kwa sasa katika muktadha wa maana ya kitalimungu katika Tume yao, isingewezekana kupanua na kuzidisha mikataba hii ya kichungaji, hasa katika mazingira ambayo waamini wetu wanajikuta katika hali ya wachache au ughaibuni? Ni swali Papa amelitoa. Kwa kujibu amesema “ Ni changamoto na swali hili ni changamoto. Roho Mtakatifu atuvuvie njia za kusonga mbele katika njia hii, ambayo inatazamia wema wa watu, wema wa nafsi, wema wa watu wa Mungu, wetu, kila kitu, na si tofauti za kimaadili au kitaalimungu au kiitikadi”. Wema na watu wapo hapo. Yesu Kristo alifanyika mwili, akawa mwanadamu, na hivyo mshiriki wa watu waamini wa Mungu, hakuwa wa wazo, bali akawa mtu. Na lazima siku zote kutafuta mema ya wanadamu na ya watu waamini wa Mungu, Baba Mtakatifu Francisko amehamasisha.
Kutokana na hilo ndipo kunazaliwa hatua ya tatu ya uekumene ambao upo tayari kama hali halisi awali ya yote sehemu mahalia. Hii ni kutokana kwamba waamini wengi mara nyingi wa nchi za mashariki ya Kati na hata wale ambao wamehamia Magharibi wanaishi tayari na uekumene katika maisha yao ya kila siku katika familia zao, kazini, na mambo yao ya kika siku. Na wanafanya uzoefu mara nyingi pamoja na uekumena wa mateso, katika umoja wa ushuhuda kwa jina la Kristo na hata kufikia gharama ya maisha. Kwa hiyo, uekumene wa kitaalimungu unapaswa kutafakari si tu juu ya tofauti za kidogma zilizotokea huko nyuma, bali pia uzoefu wa sasa wa waamini wetu. Kwa maneno mengine, mazungumzo juu ya mafundisho yangeweza kitaalimungu kuendana na mazungumzo ya maisha yanayoendelea katika mahusiano ya ndani na ya kila siku ya Makanisa yetu, ambayo yanaunda mahali halisi ya kitaalimungu . Katika suala hilo, ili kuongeza ujuzi zaidi wa kindugu, Papa Francisko amefurahia mpango wao unaolenga kuhamaisha ziara za mafunzo ya mapadre vijana na watawa kwa kila Makanisa.
Wiki tatu zilizopita alipata furaha ya kupokea ujumbe uliofika mjini Roma, kwa mwaliko wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo, kukutana na Kanisa Katoliki. Hii ndiyo njia, ya kukutana kidugu, kusikiliza, kushirikishana na kutembea kwa pamoja. Na ni vyema kushirikisha vizazi, vilivyo hai katika jumuiya za mahalia katika njia ya Makanisa yote ili mazungumzo juu ya mafundisho yaendelee pamoja na mazungumzo ya maisha. Katika muktadha wa ubatizo, uchungaji na mahalia, na maelekezo matatu ya kiekumene ndiyo kwa upande wa Papa Francisko anafikiri ni muhimu katika safari kuelekea umoja kamili. Papa amesema hatua nyingine inayofuata ya mazungumzo itajikita juu Bikira Maria kwa mafundisho na katika Maisha ya Kanisa. Lakini kuanzia sasa, Papa amesema inawezekana kusali pamoja na maneno ya sala ya zamani sana. “Tunaukimbilia ulinzi wako mzazi Mtakatifu wa Mungu. Usitunyime tukikuomba katika shida zetu, utukoe kila tuingiapo hatarini ewe bikira Mtukufu na mwenye baraka”.