Papa amepokea barua na hati za utambulisho wa Balozi wa Congo
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 3 Juni 2022 amepokea barua na hati za utambulishi wa Balozi wa Jamhuri ya Congo kuwakilisha nchi yake Vatican, Bwana Rigobert Itoua . Alizaliwa mnamo tarehe 20 Aprili 1947 huko Brazzaville. Ni baba wa familia na watoto sita.
Mafunzo
Bwana Rogobert mnamo 1969 alipata Diploma ya Shule ya sekondari kutoka Seminari ya Mtakatifu Jean de Brazzaville. Alipata pia Leseni ya Fasihi ya Kisasa kutoka Kituo Kikuu cha Mafunzo ya Juu huko Brazzaville mnamo 1973 na Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Mahusiano ya Kimatafa huko Cameroon mnamo 1983.
Nyadhifa
Ameshika nyadhifa zifuatazo: Profesa katika Chuo cha Lumumba (1973 - 1977), Mkuu wa Idara ya Asia, MAE (1978 - 1980); Mwambata wa Kidiplomasia katika ofisi ya Urais wa Jamhuri (1983 - 1990); Mshauri, Ubalozi nchini Cuba (1990 - 1995); Naibu Katibu Mkuu nchini mwao, Mkuu wa Idara ya Huduma za Jumla, MAE (1997 - 1998); Naibu Katibu Mkuu, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Nchi Mbili, MAE (1998 - 2005); Mshauri, Ubalozi nchini China (2005 - 2010); Balozi, Mkurugenzi wa Baraza la Mawaziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano na Congo Nje ya Nchi (2018 - 2022).