Tafuta

Shambulizi katika Kanisa la Mtakatifu Francis huko Owo nchini Nigeria. Shambulizi katika Kanisa la Mtakatifu Francis huko Owo nchini Nigeria. 

Nigeria,Papa:vurugu hazisemekani,amani ishinde chuki

Kwa njia ya telegram iliyotiwa saini na katibu wa Vatican,Kardinali Parolin,Papa Francisko anaelezea ukaribu wake wa kiroho na Jimbo la Ordo na kuomba kuombea mioyo ya wale ambao wametekeleza kile kinachoitwa mauaji ya Pentekoste iongoke.Kardinali Matteo Zuppi,Rais wa Baraza la Maaskofu Italia(CEI),katika barua kwa Jimbo la Nigeria anaelezea upendo wa Makanisa ya Italia na anathibitisha:"Uovu hautakuwa na neno la mwisho!"

Na  Angella Rwezaula – Vatican.

Ni shambulio la kutisha, ambalo Papa alihuzunishwa sana na ambayo yanaonekana maneno ya kwanza katika  telegram yake iliyotiwa saini na katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, ambapo Papa Francisko anamwelekeza Askofu Jude Ayodeji Arogundade, wa jimbo la Ondo, Jimbo ambalo ni sehemu ya Owo iliyopo nchini mali, ambapo Kanisa la Mtakatifu Francis Xaver lipo katika eneo la shambulio la kikatili na  ambapo takriban zaidi ya watu 23 walipoteza maisha yao Dominika tarehe 5 Juni 2022, wakiwemo watoto wawili na Makumi ya waamini waliojeruhiwa wakiwa kanisani.

Mauaji katika kanisa katoliki nchini Nigeria, uchungu wa Papa

Papa Francisko kwa maana hiyo anawahakikishia ukaribu wake wa kiroho kwa wale wote ambao wameathiriwa na kitendo hiki cha ukatili usio na mfano, na baadaye anaombea roho za marehemu  huruma ya Mungu na kuomba uponyaji na faraja ya kimungu kwa waliojeruhiwa na wale wanaoishi kwa huzuni kwa ajili ya wapendwa wao. Kutoka kwa Papa ndipo pia anasali kwa ajili ya uongofu wa wale ambao wamepofushwa na chuki na vurugu, ili waweze kuchagua njia ya amani na haki. Katika Telegramu iliyoelekezwa kwa askofu wa Ondo inahitimishwa kwa baraka za Mungu za faraja na nguvu na huku akitoa mwaliko kwa waamini kuendelea kuishi ujumbe wa Injili kwa uaminifu na ujasiri.

Hata hivyo tayari, Baba Mtakatifu Dominika alikuwa ameungana  na maumivu ya jumla, wakati maelezo ya tukio hilo yakifafanuliwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican, Dominika mchana tarehe 5, Juni 2022. Msemaji wa Vyombo vya habari Dk. Matteo Bruni alikuwa amesema kuwa: "Papa Francisko anawaombea waathirika na nchi, iliyoathiriwa kwa uchungu wakati wa kusherehekea, na kuwakabidhi wote kwa Bwana, ili aweze kutuma Roho wake kuwafariji.

Kardinali Zuppi: ‘Uovu hautakuwa na neno la mwisho’

Hata rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia, Kardinali Matteo Zuppi, katika barua yake alitaka kueleza ukaribu na rambirambi kutoka kwa  maaskofu wa Italia kwa Askofu  Jude Ayodeji Arogundade.  Aliandika Kardinali  Zuppi wanavyoguswa na mamivu yao, huku wakiwaombea wale ambao wameuawa uhuruma ya Baba na faraja kutoka kwa Roho Mfariji kwa familia zao. Kwa maana hiyo  Kardinali anasisitiza jinsi Dominika  katika mahubiri ya Misa ya Pentekoste, Papa alikumbuka kwamba “Roho Mtakatifu anatualika kamwe tusipoteze kujiamini na kuanza upya daima: kuinuka! kusimama! Daima anatupatia ujasiri: Na anatushika  mkono: inuka!  Kama Mkirene tunashiriki janga la kile kilichotokea, tukibeba uzito wa Msalaba pamoja nao, kwa ufahamu kwamba njia yetu daima itaangazwa na mwanga wa Ufufuko. Rais wa CEI anahitimisha barua hiyo hivi: "Uovu hautakuwa na neno la mwisho! Hata kama giza na kifo vinaonekana kuifunika dunia, tuna hakika kwamba nguvu ya maombi na zawadi ya imani itaondoa mawingu".

TELEGRAMU YA PAPA KWA WATHIRIKA WA MASHAMBULIZI NCHINI NIGERIA
07 June 2022, 10:28