Tafuta

Nia ya sala ya Papa kwa mwezi Juni 2022:kuombea familia

Katika ujumbe kwa njia ya video wa nia ya sala ya Papa kwa mwezi Juni 2022 inayosambazwa na Mtandao wa Kiamataifa wa Sala ya Papa,inajikita na Mada ya Familia.Papa FRancisko anasema:"Tusali kwa ajili ya familia kikristo ulimwenguni kote ili kwa ishara za dhati waishi kwa shukrani ya upendo na utakatifu wa maisha kila siku”.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Katika ujumbe kwa njia ya video wa Papa Francisko kwa mwezi Juni 2022 wa nia ya sala ambayo anaikabidhi kwa Kanisa zima Katoliki ulimwenguni kote, kupitia Mtandao wa Sala Kimataifa wa Papa, Baba Mtakatifu anajikita na mada ya ‘Familia’. Ni katika Muktadha wa maandalizi ya Mkutano wa X wa Familia Ulimwenguni, unaotarajia kuanzia tarehe 22 hadi 26 Juni 2022. Kwa maana hiyo Papa Francisko anawaalika wakatoliki wote kusali kwa ajili ya familia hizo.

Hakuna Familia kamilifu 

Papa Francisko katika ujumbe huo kwa njia ya video anabainisha: "Familia ni mahali ambamo tunajifunza kuishi. Hapa ni kuishi na vijana zaidi na wazee zaidi. Na kwa kukaa pamoja, vijana, wazee, watu wazima, watoto, kwa  kubaki wameungana katika tofauti zao, tunainjilisha kwa mfano wetu wa maisha.” Baba Mtakatifu Francisko aidha amesisitiza kwamba: “kiukweli  hakuna familia iliyo kamilifu. Daima kuna “lakini”. Lakini halijitokezi lolote. Hakuna haja ya kuogopa makosa; lazima kujifunza kutokana nayo, ili kuweza kwenda mbele”.

Mungu yuko pamoja nasi

Baba Mtakatifu amesema: “Tusisahahu kuwa Mungu yupo pamoja nasi; katika familia, kwenye mitaa, katika mji tunamoishi, yuko pamoja nasi. Yeye anahangaika sisi, anabaki nasi kila wakati katika kuyumba yumba kwa mtumbwi uliotikiswa na bahari: tunapogombana, tunapoteseka, tunapokuwa na furaha, Bwana yupo hapo na anatusindikiza, anatusaidia, anatusahihisha”.

Tuwaombee familia Kikristo ulimwenguni

Papa Francisko akiendelea na ujumbe huo kwa njia ya video amesema kwamba: “Upendo katika familia ni safari binafsi ya utakatifu kwa kila mmoja wetu. Na ndiyo maana nimechagua kama kauli mbiu ya Mkutano wa Familia ulimwenguni kwa mwezi huu. Tuwaombee familia Kikristo ulimwenguni kote, kwa ajili ya kila mmoja na kwa ajili ya familia ili kwa ishara za dhati, waishi kwa furaha ya upendo na utakatifu wa maisha kila siku”, amesisitiza Papa Francisko ujumbe kwake kwa njia ya video kwa lugha ya kihispania.

Niza ya Papa kwa Mwezi Juni 2022 ni kwa ajili ya kuombea Familia
Niza ya Papa kwa Mwezi Juni 2022 ni kwa ajili ya kuombea Familia
NIA YA SALA YA PAPA KWA MWEZI JUNI 2022
02 June 2022, 16:35