Tafuta

Papa Francisko: Haki Jamii nchini Equador inaweza kupatikana kwa njia ya majadiliano yanayosimikwa katika ukweli na uwazi; ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Papa Francisko: Haki Jamii nchini Equador inaweza kupatikana kwa njia ya majadiliano yanayosimikwa katika ukweli na uwazi; ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. 

Machafuko Nchini Equador: Haki Jamii: Majadiliano Katika Ukweli

Papa anapenda kuonesha uwepo wa karibu kwa wananchi wa Equador katika kipindi hiki chenye matatizo na changamoto nyingi. Anawaalika watu wote kuwa na kiasi. Wajifunze kwamba, ni kwa njia ya majadiliano katika ukweli hapo ndipo, amani jamii inaweza kupatikana. Kipaumbele wapewe wananchi wanaosukumizwa pembezoni mwa vipaumbele vya jamii pamoja na maskini,

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Nchi ya Equador katika miezi ya hivi karibuni, imejikuta ikitumbukia katika machafuko ya kisiasa na ghasia za kijamii, kiasi hata cha kutoweka kwa misingi ya amani na haki jamii. Kumekuwepo na maandamano makubwa nchini humo ili kupinga kupanda kwa gharama ya maisha kutokana na mfumuko wa bei za nishati ya mafuta na chakula. Hali hii imepelekea kushuka kwa hali ya maisha. Katika hali na patashika hii nguo kuchanika, waandamanaji wamekuwa wakipambana na mkono wa chuma. Wananchi wa Equador wanadai nafuu ya maisha, ruzuku ya serikali katika pembejeo za kilimo ili waweze kujikwamua na umaskini wa hali na kipato; pamoja na kusitisha urejeshaji wa mikono ambayo wananchi wengi walikopa lakini kwa sasa wanashindwa kurejeshesha kutokana na hali ngumu ya uchumi. Wananchi wanaitaka Serikali ipige rufuku uchimbaji wa madini kwenye maeneo ya watu asilia kwani, uchimbaji huu, umekuwa ni chanzo kikuu cha umaskini na maafa kwa watu mahalia.

Machafuko ya kisiasa nihatari kwa misingi ya haki, amani na upatanisho nchini Peru
Machafuko ya kisiasa nihatari kwa misingi ya haki, amani na upatanisho nchini Peru

Wananchi wengi wameathirika sana kutokana na Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19, hali ambayo imepelekea maafa makubwa kwa watu na mali zao; ukosefu wa fursa za ajira pamoja na kuendelea kuporomoka kwa uchumi kila kukicha. Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 25 Juni 2022 alisikitika kusema kwamba, anafuatilia kwa uchungu mkubwa, yale yanayoendelea kujiri nchini Equador. Baba Mtakatifu anapenda kuonesha uwepo wa karibu kwa watu wa Mungu katika kipindi hiki chenye matatizo na changamoto nyingi. Anawaalika watu wote kuwa na kiasi. Wajifunze kwamba, ni kwa njia ya majadiliano katika ukweli na uwazi tu, hapo ndipo, amani jamii inaweza kupatikana. Kipaumbele cha kwanza wapewe wananchi wanaosukumizwa pembezoni mwa vipaumbele vya jamii pamoja na maskini, kwa kuheshimu utu, na haki msingi za kijamii. Taasisi mbalimbali nchini Equador ziheshimiwe kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Equador Amani Jamii

 

28 June 2022, 15:22