Tafuta

2022.05.19 Papa alikutna na Wakurugenzi waariri wa Magazeti ya Kijesuit 2022.05.19 Papa alikutna na Wakurugenzi waariri wa Magazeti ya Kijesuit  

Wahariri wa majarida ya Kijesuit wamekutana na Papa Francisko

Katikati ya mazungumzo yao kulikuwa na mada ya vita vya Ukraine,maisha ya Kanisa na njia ya sinodi inayoendelea.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Wahariri kumi wa jarida la Kijesuit wamepokelewa mnamo tarehe 19 Mei 2022 mjini Vatican na Papa Francisko. Haya ni majarida ya kiutamaduni ya Ulaya wa Jumuiya ya Yesu ya Wajesuit: Stimmen der Zeit (Ujerumani), Choisir (Uswisi), Signum (Sweden), Razón y fe (Hispania), Brotéria (Ureno), Deon (Poland), A Szív (Hungaria), Viera huko život (Slovakia), ‘Thinking Faith’, Imani ya Kufikiri (Uingereza) na La Civiltà Cattolica (Italia). Wahariri watatu ni watu walei, wakiwemo wanawake wawili (kwa majarida ya Uswisi na Kiingereza) na wengine walikuwa ni watawa wa Kijesuit.

Wakurugenzi Waariri wa Magazeti ya Kijesuit wamekutana na Papa Francisko
Wakurugenzi Waariri wa Magazeti ya Kijesuit wamekutana na Papa Francisko

Mkuu wa Jumuiya ya Yesu, Padre Arturo Sosa Abascal, pia alishiriki katika Mkutano huo. Zaidi ya saa moja ya mazungumzo yalikuwa ni  mtindo wa kawaida wa kindugu na wa moja kwa moja, kwa mujibu wa maandishi ya Padre Antonio Spadaro, mkurugenzi wa Gazeti La Civiltà Cattolica katika tweet yake. Hakukuwa na hotuba, ya Papa lakini mazungumzo  yalikuwa rahisi na yasiyo rasmi, yenye maswali na majibu. Kwa maana hiyo  walizungumza hasa juu ya vita vya Ukraine na hali ngumu ambayo ulimwengu unapitia, lakini pia juu ya maisha ya Kanisa, ya mchakato wa sinodi wa sasa na lengo la magazeti hayo. Wakurugenzi hao wako Roma kwa ajili ya mkutano wa siku tatu. Ripoti ya mahojiano  hayo ya mkutano itachapishwa hivi karibuni na Gazeti la Kijesuit La Civiltà Cattolica na majarida ya nchi zingine.

20 May 2022, 11:02