Tafuta

Dhoruba kali Dhoruba kali  

Uchungu wa Papa kwa sababu ya majanga ya asili Canada na Michigan

Baba Mtakatifu Francisko ametuma salamu za rambi rambi zilizotiwa saini Kardinali Parolin, Katibu wa Vatican kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Canada Askofu Mkuu Raymond Poisson kwa sababu ya waathirika wa dhoruba kali ambalo limeikumba hivi karibu Kusini Mashariki mwa Canada na Marekani na telegramu kwa Askofu Jeffrey J. Walsh wa Jimbo la Gaylord kutokana na kimbunga.

Vatican News

Dhoruba kali Kusini Mashariki mwa  Canada,na Kimbunga katika mji wa Michagan Marekani, ni majanga mawili ya asili ambayo kwa bahati mbaya yamesababisha vifo na zaidi uharibifu mkubwa sana.  Katika matukio hayo mawili yaliyo wakumba watu, Papa Francisko kupitia Kardinali  Parolin, Katibu wa Vatican, amefanya ziwafikie sala zake na mshikamano wake kupitia Telegram mbili zilizo elekezwa: kwanza kwa  Rais wa Baraza la Maaskofu Nchini Canada, Askofu Mkuu Raymond Poisson, na pili kwa  Askofu Jeffrey J. Walsh wa Jimbo la Gaylord, Michigan nchini Marekani  waliokumbwa na dhoruba.

Wanaoteseka anawaombea

Maeneo yalikumbwa zaidi nchini Canada ni katika Wilya za  Ontario  na Québec, ambazo zina watu wengi katika Nchi, mahali ambapo dhoruba ya masaa mawili, ilitokea Jumamosi mchana 21 Mei 2022 katika eneo, kwa upepo mkali zaidi ya km 130 kwa saa, na kuwaua watu 8 na ambao kwa   salamu za rambi rambi, Papa Fransiko anawaombea na vile vila kwa wale wote ambao wanateseka na athari hizo akiwasindikiza kwa baraka kwa namna ya pekee kwa ajili ya mamlaka ambao waaendelea kutoa usadizi wa lazima.

Jumuiya ndogo imepigishwa magoti

Tukio la janga la asili pia linatazama mji wa Gaylord, huko Michigan Kaskazini  Marekani mahali ambazo siku chache zilizopita, kimbunga cha nguvu kilikumba Jumuiya ya  watu karibia elfu nne, kwa kuua mtu na kuwajeruhi zadi ya watu 40 , wakati kinapitia na kupeperusha paa za nyumba na kuangua miti haya nguzo za  umeme. Hata kwa wao Baba Mtakatifu Francisko, amebainisha kuhuzunika kwa kile kilichotokea, na kuonesha mshikamano kwa wote  ambao wamekumbwa na mkasa huo wa kiasilia, na kuomba Baraka iwashukie waliojeruhiwa, waliolundikana na wale ambao wanatoa msaada kwa ajili ya  na wakati huo huo kumpunzika kwa Amani waliopoteza maisha.

26 Mei 2022, 15:51