Tafuta

Mauaji yaliyofanyika katika shule moja huko Texas Mauaji yaliyofanyika katika shule moja huko Texas 

Texas,Papa Francisko:Ni wakati sasa wa kusitisha utumiaji silaha kiholela

Mara baada ya Katekesi yake,Papa Francisko amekumbuka,mauaji yaliyotokea katika shule ya msingi huko Texas nchini Marekani na kijana mmoja:“ Nimeumia moyoni,tujitoe sote ili majanga ya namna hii yasitokee tena.Kardinali Cupich wa Chicago:"sasa ni lazima tuchukue hatua ili kulinda vijana,haki ya kubeba silaha haitakuwa muhimu zaidi kuliko maisha ya binadamu."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu mara baada ya katekesi yake kwa waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro  Jumatano tarehe 25 Mei, ametoa ameonesha masikitiko yake kuhusu mauaji katika shule ya msingi ya Uvalde yaliyogharimu jumla ya maisha ya watu 21 ambamo kuwa watoto 19 na walimu wawili. Hili ni tukio la pili katika historia ya Marekani kutokea  shuleni . kwa maana hiyo Papa amesema :“Umefika wakati wa kusema vya kutosha kusitisha utumiaji silaha kiholela. Sote tujitume kwa sababu majanga kama haya yasiweze kutokea tena”.  Aliyechukua hatua hiyo ni kijana mmoja ambaye baadaye aliuawa na polisi, ambaye alifyatua risasi madarasani baada ya kumjeruhi bibi yake aliyejaribu kumzuia.

“Nimehuzunishwa na mauaji ya shule ya msingi ya Texas. Ninawaombea watoto, watu wazima waliouawa na familia zao. Ni wakati huo huo kuacha ununuzi wa silaha kiholela. Tufanye kazi kwa bidii, ili majanga kama haya yasitokee tena.” Amesema Papa.

Kardinali Cupich: Tunalia lakini tunatenda

Sauti ya maaskofu wa Marekani ilisikika mara moja, hasa Kadinali Blase Cupich, askofu mkuu wa Chicago, ambaye alilaani sheria za kumiliki silaha. “Lazima tulie na kuzama katika uchungu, alisema kardinali katika taarifa yake  lakini lazima tuwe tayari kuchukua hatua katika kukabiliana na kile kinachoonekana kuwa cha kukata tamaa kisichoweza kushindwa. Miaka kumi imepita tangu mauaji ya Sandy Cook, pia shule ya msingi, ambapo waathirika 20 kati ya 26 walikuwa ni watoto. Akikumbuka hilo na misiba mingine mingi iliyotokea nchini Marekani katika miaka ya hivi karibuni, Kardinali alijiuliza: “Tuna tumaini gani kwa watoto wetu? kwa kufanya tu kile ambacho jamii inasema ni vizuri kwao: kwenda shule? Na kufikia kujiuliza kama wana wakati ujao? Askofu Mkuu wa Chicago baadaye alitoa mfano wa utafiti wa Northwestern Medicine wa 2021, ambao uligundua kuwa umarufuku wa kusitisha  silaha za mashambulizi ilizuia risasi 10 za molekuli katika miaka 10 ambayo ilikuwa inatumika. Watafiti pia walibainisha kuwa kama ingeendelea  kutumiak marufuku hiyo katika miaka iliyofuata, ingeweza kuzuia ufyatuaji risasi mwingine wa hadharani (30)ambao uliua watu 339 na kujeruhi wengine 1139”, alibainisha.

Tuna silaha nyingi kuliko watu

Kardinali Cupich, akiungwa mkono na maaskofu wote wa Marekani, aliomba kila mtu kufikiria kuwa mzazi na mtoto katika shule hiyo, na baadaye akasema “Fikiria kuweza kuwazika. Marekani imejaa silaha. Tuna silaha nyingi zaidi kuliko watu, alisema tena. Ingawa hii haijawahi kuwa hivyo kila wakati, ufyatuaji risasi wa watu wengi umekuwa ukweli wa kila siku huko Marekani leo hii. Kwa kuhitimisha amesema Kardinali Cupich Haki ya kubeba silaha kamwe haitakuwa muhimu zaidi kuliko maisha ya binadamu kwani  watoto wetu pia wana haki. Na viongozi wetu waliochaguliwa wana wajibu wa kimaadili kuwalinda”.

25 May 2022, 16:20