Tafuta

Ujumbe wa Papa FRancisko wa siku ya Wazee Duniani Ujumbe wa Papa FRancisko wa siku ya Wazee Duniani 

Siku ya Wazee Duniani 2022:Wazee ni wasanii wa mapinduzi ya huruma

Katika ujumbe wa Siku II ya Wazee Duniani ambayo inaangukia tarehe 24 Julai,Papa Francisko anashauri kugeuka kuwa walimu wa mtindo wa kuishi kwa amani na umakini kwa wadhaifiu huku kwa kulinda ulimwengu na kutazama uzee kama kipindi cha sala kwa ajili ya uongofu wa mioyo.Parokia na Jumuiya zitimize wajibu wa huruma kwa kuwatembelea wazee walio peke yao na katika majengo ya kutunza wazee.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ni kipindi cha majaribu ambayo ulimwengu unaishi, hasa kwa janga, dhoruba isiyo tarajiwa na vurugu, kuanzia na vita, ambavyo vinadhuru amani na maendeleo kwa ngazi ya ulimwengu na kuwa tishio la dhati. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko anabainisha katika Ujumbe wake wa  Siku II ya Wazee, Duninia kwa kwama 2022 na kutoa angalisho linaloibuka la katotazama majanga mengi na mitindo iliyoenea ya vurugu ambayo inatishia familia ya binadamu na nyumba yetu ya pamoja. Moja ya vurugu hizi amethibtisha mara nyingi ni kusahau wazee, kuwabagua, kufikia kuwa wao hawana nguvu za kuzalisha tena.  Kauli mbiu aliyochaguliwa kuongoza Siku hii itakayofanyika mnamo tarehe 24 Julai inatoka katika Zaburi ya 92: “Kwa  wazee watazaa matunda tena". Haya ni maneno ambayo yanakwenda kunyume kulinganisha na ulimwengu unavyofikiria katika umri huo wa maisha na kufuatia na tabia ambazo baadhi ya wazee wengi wanakwenda mbele na tumaini kidogo na bila kusubiri lolote la wakati ujao.

Uzee unaogopesha

Papa Francisko katika ujumbe wake wa siku ya Wazee Duniani anakumbusha kuwa kwa walio wengi uzee unaogopesha kwa sababu unazingatiwa kama ugonjwa na kupelekea kuepukwa kwa kila aina ya mawasiliano na wazee. Suluhisho mara nyingi ni ile ya kuwapeleka katika miundo ya utunzajia ambayo inabeba mzigo kwa kuwakumbatia kwa namna moja tusema wa utamaduni wa kutupa na ambao unaruhusu kutembea katika njia zilizotenganishwa kati yetu na wao, Papa amebainisha. Lakini kiukweli, maisha marefu kwa mujibu wa  mafundisho matakatifu ni baraka na wazee sio watu wa kupisha mbali. Bali ni ishara hai ya wema wa Mungu ambayo yanatoa maisha yao kwa wingi. Kwa kuongezea hilo "Heri nyumba ambayo inalinda Mzee, heri familia inayoheshimu babu na bibi  zake". Kwa upande wa Papa, amesisiriza kuwa umri huu ni vigumu kuelewa, kwa sababu hayuko tayari kuukubali na kwa sababu mipango ya usaidizi hutolewa, lakini sio mipango ya kweli ya usaidizi.

Tusiangalia makunyanzi bila kuona upeo

Tunaangalia makunyanzi ili kuficha, lakini hatuoni upeo, kwa hivyo utamaduni  wenyewe wa kutupa unaingizwa ndani mwake. Papa ameeleza kuwa Zaburi, inakuja kuokoa kwa sababu ni katika kumtumaini Bwana ndipo tutapata nguvu za kuzidisha sifa. Tutagundua kwamba kuzeeka sio tu kuzorota kwa asili ya mwili au kupita kwa wakati na kuepukika, lakini ni zawadi ya maisha marefu. Kuzeeka sio hukumu bali ni baraka. Papa Francisko kwa maana hiyo ametoa  ushauri namna ya kuelekeza uzee uli hai hadi kufika mtazamo wa kiroho kwa njia ya usomaji wa Neno la Mungu kila siku, sala ya kila siku,  utamaduni na sakramenti na ushiriki wa Liturujia. Kumwilisha uhusiano na Mungu na wengine amesisitiza ndio njia, hasa kwa kutoa upendo kwa walio karibu na hata kwa maskini na wanaoteseka. Yote hayo yataweza kusaidia, kutohisi watazamaji tu katika tamasha la ulimwengu, bila kuwa na kizuizi, na kubaki katika dirisha. Kinyume chake kwa kunoa akili zetu za kutambua uwepo wa Bwana, tutakuwa kama mizeituni yenye majani mabichi katika nyumba ya Mungu na  tunaweza kuwa baraka kwa wale wanaoishi karibu nasi, anasisitiza Baba Mtakatifu.

Wazee wanaitwa kutoa mchango wa mapinduzi ya huruma

Katika ujumbe wake ambao Papa mara nyingi ametumia 'sisi', kwa kuelekeza wazee, babu na bibi, ili kusisitiza juu ya utume ambao wao wameitwa kutimiza, yaani kutoa mchango muhimu kwa ajili ya mapinduzi ya huruma, mapinduzi ya kiroho, ya  kuishi kama walio mstari wa mbele. Kuwa wasanii kwa njia ya sala ndiyo anaelekeza Papa Francisko  ili kusindikiza kilio cha uchungu kwa anayeteseka na ambaye anaweza kuchangia kubadili mioyo iliyosononeka kwa kuruhusu kila mmoja amtambue ndugu mwingine. Kwa maana hiyo kuwa washairi wa sala ambacho ni kielelezo kikubwa cha kwaya kinasaidiwa na sifa na maombi kwa jumuiya ambayo inafanya kazi na kupambana katika kambi za maisha. Baba Mtakatifu Francisko amefafanua kuwa: “Na sisi, babu na bibi na wazee, tuna jukumu kubwa: kuwafundisha wanawake na wanaume wa wakati wetu kuona wengine kwa uelewa sawa na mtazamo wa huruma ambao tunageuka kwa wajukuu wetu. Tumeuheshimu ubinadamu wetu katika kuwajali wengine na leo tunaweza kuwa mabwana wa maisha ya amani na makini kwa walio dhaifu”. 

Mwito wa kulinda moyo kama Mtakatifu Yosefu

Papa Francisko katika ujumbe wake amebainisha jinsi  ya kulinda hata watoto wanaoteseka ambapo amesema, "moja ya matunda ambayo tunaitwa kutoa ni  kulinda ulimwengu. Kulinda moyo wetu kama alivyokuwa akifanya Mtakatifu Yosefu, Baba mpole na mkarimu, kwa wadogo wa Ukraine, wa Afghanistan, wa Sudan Kusini… Ufahamu huu, unatokana na kujua kuwa: “hatuwezi kujiokoa binafsi, furaha ni mkate tunaokula pamoja”. Kwa maana hiyo babu, bibi na wazee wanaitwa kutoa ushuhuda kwa wale walio katika udanganyifu wa kufanikiwa tofauti na wengine. Wote, hata aliye dhaifu zaidi, anaweza kuifanya: kujiruhusu sisi wenyewe kutunzwa mara nyingi na watu wanaotoka nchi nyingine ni mtindo na njia ambayo inadhihirisha kwamba sio tu kuishi pamoja kunawezekana, lakini ni lazima".

Mwaliko wa kusherehekea siku hiyo kwa kutembelea wazee wapweke 

Kwa kuhitimisha ujumbe huo, Baba Mtakatifu ametoa mwaliko wa kusherehekea Siku ya Wazee duniani pamoja,kwa kukaribisha parokia na jumuiya kuwatembelea nyumbani au katika makazi ambako wazee hao ni wageni kwa sababu urafiki unaweza kuzaliwa kutokana na kukutana.  Kwa maana hiyo : “Tuhakikishe kuwa hakuna mtu ayakayeishi peke yake siku hiyo. Kuwatembelea wazee wenye upweke ni kazi ya huruma ya wakati wetu! Tumwombe Mama Yetu, Mama wa Huruma, atufanye sisi sote kuwa wasanii wa mapinduzi ya huruma, ili tukomboe ulimwengu pamoja kutoka katika kivuli cha upweke na upepo wa vita.

UJUMBE WA PAPA WA SIKU YA WAZEE DUNIANI

 

10 May 2022, 15:56