Tafuta

Katekesi ya Papa 4 Mei 2022 Katekesi ya Papa 4 Mei 2022 

Papa:tukabidhi Bikira Maria kwa ajili ya Amani ya Ulaya na Ulimwengu

Wakati wa salamu zake kwa makundi mbali mbali mara baada ya katekesi yake,Papa Francisko amewaalika kusali kila siku Rosari Takatifu katika mwezi Mei,kwa kumwomba Bikira Maria kwa mara nyingine tena kwa ajili ya bara la Ulaya na ulimwengu mzima.Amekumbusha siku kuu ya Jasna Góra nchini Poland kwamba mwenye heri Kardinali Wyszyński,aliwafundisha kujikabidhi kwa Maria katika vipindi vigumu zaidi vya historia yao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Franisko hawezi kuinuka kwa sababu goti lake  linalomfanya ateseke linamlazimisha kukaa kwenye kiti, lakini angependa asalimie kila mtu iwezekanavyo na kusema hivyo, akiomba msamaha kwa mara nyingine tena mwishoni mwa katekesi yake   kwa matumaini ya kuweza kupona ili asimame na kuwa karibu sana na watu. Lakini kwa hakika angependa awasindikize na ishara ya moyo, ambayo inamsukuma kwa kila hali kuomba ili kwamba mgogoro na shida, za ulimwengu zilizoletwa na vita, ziiishe na kuacha kutafuta sayari kwa kumtazama Bikira Maria ambaye kwa mwezi huu ni muafaka kumwomba kwa bidiii sana maana ni mwezi wa kusali Rosari Takatifu.

Salamu mara baada ya katekesi ya Papa 4 Mei 2022
Salamu mara baada ya katekesi ya Papa 4 Mei 2022

Papa Francisko kwa maana hiyo amewaomba wasali kwa maamombezi ya Bikira Maria kwa nia zao binafsi na zile za Kanisa na  kwa ajili ya amani ya ulimwengu. Mwaliko huoameutoa akizungumza na wanaozungumza lugha ya kijerumani lakini pia hata kwa makundi mengine ya ambapo amerudia kuwaomba wasali. Kwa mfano nchini Polabd, tarehe 3 Mei wamefanya siku kuu ya Bikira Maria Malkia wa Nchi hiyo.

Salamu mara baada ya katekesi ya Papa 4 Mei 2022
Salamu mara baada ya katekesi ya Papa 4 Mei 2022

Papa amesema: kwa ajili ya ‘Jasna Góra’ mmemkubuka mwenye heri Kardinali Wyszyński, ambaye aliwafundisha kujikabidhi kwa Maria katika vipindi vigumu zaidi vya historia yenu. Kwa kufuata mfano wake, jikabidhi kwa Bikira Matakatifu hatima yenu ya Nchi na amani kwa ajili ya Ulaya”.

Salamu mara baada ya katekesi ya Papa 4 Mei 2022
Salamu mara baada ya katekesi ya Papa 4 Mei 2022

Hatimaye, silaha ya kizamani na mpya kwa kukumbuka waamini wa lugha ya kireno na kusali rosari kila siku kwamba: “Tumeanza  tu mwezi wa Mei, ambao kiutamaduni onawaalika watu wa Kikristo kuzidisha ishara zao za kila siku za ibada kwa Bikira Maria. Siri ya amani na ujasiri wake ilikuwa ni uhakika huu: “hakuna lisilowezekana kwa Mungu”. Tunahitaji kujifunza hili na Mama wa Mungu; tuwe na shukrani kwake kwa kusali rozari kila siku.

BAADA YA KATEKESI SALA YA PAPA KWA AJILI YA ULAYA NA ULIMWENGU
04 May 2022, 17:17