Papa, Wabudha wa Mongolia:Amani ni shauku ya mwanadamu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko amekutana na wawakilishi viongozi wa Wabudha kutoka Mongolia, Jumamosi tarehe 28 Mei 2022. Amewakaribisha viongozi hao i wakiongozwa na Mwenyekiti wa wao ambaye ni Balozi wa Vatican huko Ulaambaatar Askofu Mkuu Giorgio Marengo. Papa amepongeza uhusiano wa kirafiki na Kanisa Katoliki kwa kuhamasisha uelewa na ushirikiano wa Pamoja na hatimaye katika kujenga jamii ya amani. Mkutano huo ni katika fursa ya kutimiza miaka 30 ya uwepo wa Ubalozi wa Vatican katika nchi yao na kama vile uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Vatican na Mongolia. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba Amani leo hii ni matamanio ya ubinadamu. Kwa njia ya mazungumzo kwa ngazi zote ni dharura ya kuhamasisha utamaduni wa amani na kutotumia nguvu. Mazungumzo hayo lazima yatoe mwaliko kwa wote kukataa vurugu za kila aina, zikiwepo vurugu dhidi ya mazingira. Papa amebainisha kuwa kwa bahati mbaya hali hiyo inaendelea kuzuka katika dini kwa kutumia na kuhalilisha vurugu na chuki.
Lakini Yesu na Budha walikuwa wajenzi wa amani na wahamasishaji wa kutotumia vurugu. Hata Yesu aliishi kipindi cha vurugu. Yeye alifundisha kuwa uwanja wa kweli wa mapambano ambayo yanakabiliwa kwa vurugu na amani ni ndani ya moyo. Yeye alihubiri bila kuchoka upendo wa Mungu ambao unapokea na kusamehe na alifundisha mitume wake wapende adui zao (Mt 5,44). Alionesha njia ya kutotumia vurugu na amani na hatimaye hadi msalabani akahitimisha amani na kuharibu uadui (Ef 2,14-16).
Baba Mtakatifu Francisko akitazama Budha amesema kuwa Ujumbe wake msingi ulikuwa ule wa kutotumia vurgu na amani. Alifundisha kuwa ushindi unaacha nyuma chuki, kwa sababu anayeshindwa anateseka. Anaacha kila aina ya wazo la ushindi na kushindwa na kuishi katika amani na furaha (Dhammapada, XV, 5, 201). Alisisitiza zaidi kuwa kujishinda binafsi ni njia nzuri zaidi ya mengine; ni bora jujishinda mwenyewe kuliko kushida mapambano elfu dhidi ya watu (VIII, 4 [103]).
Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo amesema katika ulimwengu wa vita, viongozi wa kidini kwa dhati ambao wamesimika mizizi katika mafundisho yao ya kidini, wanao wajibu wa kutoa chachu kwa ubinadamu kuwa na utashi wa kukataa vurugu na kujenga utamaduni wa amani. Hata kama uwepo wa waamini katoliki katika Nchi yao ni wa muda mfupi lakini idadi yao ni yenye maana ambayo inajikita kwa kijua kuhamasisha utamaduni wa kukutana, kwa kufuata Mwalimu na Mwanzilishi aliyesema “pendaneni kama nilivyowapenda mimi”.
Mongolia ina utamaduni wa muda mrefu wa amani ya kuishi na dini nyingi. Ni matashi ya Papa kuwa historia ya kizamani ya maelewano katika utofauti inaweza kueendelea leo hii kwa njia ya kuendeleza uhuru wa kidini na kuhamaisha mipango ya pamoja kwa ajili ya wema wa pamoja. Uwepo wao leo hii ni ishara hai ya matumani. Kwa sababu hiyo Papa amewaalika waendeleze mazungumzo ya kidugu na mahusiano mema na Kanisa Katoliki katika nchi yao kwa ajili ya amani na maelewano (Yh 15,12). Kwa maana hiyo ameomba kuongeza nguvu kwa urafiki kwa ajili ya wote. Kwa kuhitimisha , ni matarajio ya Papa kwamba ziara yao Roma inaweza kuwa ya furaha ana shauku ya uzoefu. Na kuwa na uhakika kwamba mkutano wao na wajumbe wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini yatawapa fursa ya kuvumbua njia ya kuhamasisha kwa kima mazungumozo kati ya Wabudha na Wakristo nchini Mongolia na katika kanda yote.