Tafuta

2022.05.19 Papa ameèokea hati za utambulisho wa Mabalozi wapya wa  Burundi, Pakistan,Falme za Uarabunu na  Qatar. 2022.05.19 Papa ameèokea hati za utambulisho wa Mabalozi wapya wa Burundi, Pakistan,Falme za Uarabunu na Qatar. 

Papa kwa mabalozi wapya:bado kuna migogoro mingine mingi inayoendelea ulimwenguni

Alhamisi tarehe 19 Mei 2022 Papa Francisko,amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wasio wakazi wanaoziwakilisha nchi zao mjini Vatican.Hao ni kutoka Burundi,Pakistan,Falme za Urabuni, na Qatar.Katika hotuba yake.Papa amebainisha"pamoja na vita vya Ulaya Mashariki,haipaswi kusahaulika kwamba kuna migogoro mingine mingi inayoendelea ulimwenguni kote ambayo haizingatiwi katika vyombo vya habari.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 19 Mei 2022 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wasio wakazi wanaoziwakilisha nchi zao mjini Vatican. Mabalozi hawa wanatoka Pakistan, Falme za Urabuni, Burundi na Qatar na amewaomba kufikisha salamu na pongeza zake kwa wakuu wao wa nchi pamoja na kuwahakikisha maombi yake kwa ajili yao katika shughhli zao muhimu za kutoa huduma. Hata kama hakuna wakati muafaka, kwa hakika Papa amesema kwamba wameanza utume mpya katika kipindi maalum kigumu. Amekumbusha mara ya mwisho alivyo kutana na wenzao mwezi Januari iliyopita na kwamba   familia ya kibidamu ilikuwa angalau inaanza kupumua kutokana na kujikomboa taratibu na balaa la Uviko. “Ilionekana hatimaye tunaanza kurudia kwa maana ya kawaida licha ya kizingatia somo ambalo limepatikana kwa miaka miwili”. Baadaye wingu jeusi limeshuka Ulaya Mashariki, kwa kukumba moja kwa moja au kinyume ulimwengu mzima.

Papa amkutana na mabalozi wapya waliowakilisha hati na nyaraka za utambulisho
Papa amkutana na mabalozi wapya waliowakilisha hati na nyaraka za utambulisho

Baada ya kufanya uzoefu wa vita mbili za ulimwengu, na tishio la kinyuklia wakati wa vita baridi, pamoja na kuongezeka kwa heshima kwa jukumu la sheria za kimataifa na kuundwa kwa mashirika ya kimataifa ya kisiasa na kiuchumi yaliyozingatia uwiano wa jumuiya ya kimataifa, watu wengi waliamini kwamba vita vya Ulaya vinabaki kumbukumbu ya mbali. Na tulifikiria watoto ambao wangeuliza mama zao: “Mama, vita ilikuwa nini?”. Lakini haikuwa hivyo! Papa amesema. Walakini,  Papa ameongeza kusema kama tulivyoona katika kilele cha janga, hata katika janga la ukubwa huu, ubinadamu bora zaidi unaweza kuibuka. Labda kuliko wakati mwingine wowote, njia za kisasa za mawasiliano zimetikisa dhamiri zetu kwa kutoa picha zenye nguvu na nyakati fulani, za kuteseka na kifo. Picha hizo pia zimehimiza hali ya mshikamano na udugu, ambao umesababisha nchi nyingi na watu binafsi kutoa msaada wa kibinadamu. “Ninafikiria hasa zile nchi ambazo zinakaribisha wakimbizi kutokana na mzozo bila kujali gharama. Tumeona familia zikifungua nyumba zao kwa wanafamilia wengine, marafiki na hata wale wasiowajua.”

Papa amkutana na mabalozi wapya waliowakilisha hati na nyaraka za utambulisho
Papa amkutana na mabalozi wapya waliowakilisha hati na nyaraka za utambulisho

Baba Mtakatifu Francisko ameongeza: “Wakati huo huo, haipaswi kusahaulika kwamba kuna migogoro mingine mingi inayoendelea ulimwenguni kote ambayo haizingatiwi kidogo au kutozingatiwa kabisa, hasa katika vyombo vya habari. Baba Mtakatifu amesema, “sisi ni familia moja ya kibinadamu na kiwango cha hasira kinachooneshwa, msaada wa kibinadamu unaotolewa na hisia ya udugu inayohisiwa kwa wale wanaoteseka haipaswi kutegemea jiografia au maslahi ya kibinafsi. Kwa sababu ikiwa kila mtu ana heshima isiyoweza kuondolewa, ikiwa kila mwanadamu ni kaka au dada yangu, na ikiwa kweli ulimwengu ni wa kila mtu, haijalishi kama mtu alizaliwa hapa au anaishi nje ya mipaka ya nchi yake. (Ndugu wote, 125).  Hii inatumika sio tu kwa ajili ya vita na migogoro ya vurugu, lakini pia kwa hali nyingine za ukosefu wa haki ambazo zinakumba familia ya binadamu: mabadiliko ya tabianchi, umaskini, njaa, ukosefu wa maji safi, upatikanaji wa kazi za heshima na elimu sahihi, kwa kutaja machache tu”.

Papa amkutana na mabalozi wapya waliowakilisha hati na nyaraka za utambulisho
Papa amkutana na mabalozi wapya waliowakilisha hati na nyaraka za utambulisho

Papa amewahakikishia kuwa Vatican inaendelea kufanya kazi kwa njia nyingi ili kukuza suluhishi za amani katika hali ya migogoro na kupunguza mateso yanayosababishwa na matatizo mengine ya kijamii. Inafanya hivyo kwa usadikisho kwamba matatizo yanayoathiri familia nzima ya kibinadamu yanahitaji itikio la umoja kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, ambamo kila mshiriki hufanya sehemu yake. Kwa maana hiyo Mabalozi, wana jukumu la upendeleo katika suala hilo. Wao wanajua vyema kwamba vita daima ni kushindwa kwa ubinadamu na ni kinyume na huduma muhimu wanayofanya katika kujaribu kujenga utamaduni wa kukutana kupitia mazungumzo na kuhamasisha maelewano kati ya watu, pamoja na kuzingatia kanuni bora za sheria za kimataifa. Huduma yao si rahisi hata kidogo, lakini pengine hali za ukosefu wa usawa na ukosefu wa haki zinazoshuhudiwa katika ulimwengu wa leo zinasaidia kuthamini kazi yao hata zaidi, Papa Francisko amesisitiza. Licha ya changamoto na vikwazo, hatupaswi kamwe kupoteza matumaini katika jitihada za kujenga dunia ambayo udugu na maelewano ya pande zote hutawala na migogoro kutatuliwa kwa njia za amani. Kwa kuhitimisha, Papa amesema kuwa  mwanzoni mwa utume wao mpya, anawatakia mema na kuwahakikishia ushirikiano kwa upande wa Ofisi za Vatican  ili kukabiliana na masuala husika ya pamoja. Kwa moyo amewabariki kwa baraka ya hekima na ya amani juu yao, familia zao na wahudumu wao wa kidiplomasia.

Papa amkutana na mabalozi wapya waliowakilisha hati na nyaraka za utambulisho
Papa amkutana na mabalozi wapya waliowakilisha hati na nyaraka za utambulisho
19 May 2022, 16:59