Papa kwa Familia Kikristo:Njia ya kuhudumia ni mazungumzo na kusikiliza
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na wasomaji wa Gazeti la kila Juma la Familia Kiristo akiwashukuru kuwa leo hii wanawakilisha familia kubwa ya Kristo. Sio utani wa maneno, bali gazeti katoliki hili limeenea sana nchini Italia na linatimiza miaka 90, hivyo ni kama bibi mwema ambaye ameona mengi na kupata hekima. Yote hayo yalianza na roho ya kitume ya Mwenyeheri Padre Giacomo Alberione, Yeye alifikiria gazeti la kupeleka katika familia maono ya kikristo katika uhalisia, mada kubwa za ulimwengu na za Kanisa. Na mpango huo unawahusisha familia nzima ya Paulo ambayo inajumuisha mpadre katika mwongozo na uhariri, watawa, ndugu hasa katika hatua ya ufundi wa uchapishaji, watawa wa kike walionea katika jumuiya zinazojikita kwenye maduka ya vitabu, na wale wote ambao wanahamasika katika maparokia. Lakini ushiriki unajipanua kwa haraka katika waandishi, wataalam katika kambi zote.
Padre Alberion tayari aliwaambia mapadre vijana mnamo mwaka wa 1915 kuwa “Kupanda mawazo mazuri ili watoe matendo mema: hii ndiyo kazi ya maana. Mawazo ya kidini, mawazo ya kijamii, mawazo ya kiuchumi, mawazo ya wema, mawazo ya usafi” [...]. Tunapojua kwamba wazo linaweza kufanya mema, kwamba ukweli unaweza kufanya gazeti kuvutia, itakuwa muhimu kuwasiliana nao: ni talanta ambayo Mungu hutoa: na tuifanye kuzaa matunda “(Rej. Taalimungu ya Kichungaji, 340). Baba Mtakatifu Francisko amesema wasomaji ni urithi wa kweli wa gazeti kama la Familia ya Kikiristo. Na kiukweli, mwongozo, utahariri na mgaazeti daima yamekuza mawasiliano na watu, ule uhusiano ambao unapaswa kupyaishwa hata katika mafunzo ya kidigitali ambayo tunapitia.
Padre Alberione alikuwa akisema: “Tambulisha sinema kwa parokia na ufanye usajili wa majarida ya Kikatoliki. Gazeti la Kikatoliki ni kama ziara ya Mungu katika nyumba (Mahubiri kwa Wachungaji, kitabu VII, 1981, 318). Huo umekuwa ndio msingi wa uhariri wa Paulo kuwa makini kwa uhusiano kama ufunguo wa zoezi la kuwasiliana, na mitandao kama mahali pa kuunda ushirikiano wa maana na unaofaa; kwa kutazamia kutafuata mitindo mipya ya uwepo na matendo, yanayohusiana si tu kwa vyombo lakini zaidi kwa utamadui na mtindo mpya wa mawasilianao; na kwa huduma ya watu wote wa Mungu, hasa wanaumeana wanawake ambao wanaishi pembezoni leo hii. Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba huo ndiyo umekuwa daima unafaa na unaopaswa kupyaishwa na kwa mujibu wa mwelekeo wa uinjilishaji. Leo hii inafunguliwa mbele yetu njia mbili: ya kwanza ile ya udugu na njia ya ikolojia fungamani. Lakini mitindo inabaki kuwa ile uele ya mazungumoza na kusikiliza ambayo inaruhusu kukuza mahusiano.
Baba Mtakatifu amesema, mazungumzo ni muhimu kuelewa kuwa hata yenyewe hayawezi kupungumzwa kama moja ya mabadilisho ya takwimu au ya ahabri, na ambapo uhusiano na mwingine hauwezekani kukatishana. Hayo wanayajua vizuri. Huwezi kucnyachnga mawasiliano na ishara ya mazungumzo au kubadilisha, au kwa ujume tu wa mawasiliano ya kweli. Mawasilani ni zoezi la kina zaidi ambalo linafanya utoke nje binafasi. Kushinda kujitosheleza kwa kutazama kuelekeza upendo mpana ni muhimu katika wakati huu wa mabadiliko ya kipindi. Ili kuweza kujua anayezaungumza utume wake na kukaribia mwasilishaji lazima afanya safari ya kutoka nje, kuwa kubalisha, ikiwa lazima na mienendo na kialili. Hiyo ndiyo njia iliyoonesha na Mababa wa Mtaguso wa II wa Vatican, baadaye Mtakatifu Paulo, Mtakatifu Yohane Paulp wa II, lakini kabla ya hapo mfano ulikuwa wa Mtakatifu Paulo kwa kutangaza Injili alikuwa anaunda uhusiano na jumuiya.
Mwelekeo huo unakwenda kwa njia hii wazi kwa mada ijayo ya Mkutano Mkuu wa Makuhani wa na Ndugu wa Jumuiya ya Mtakatifu Paulo. Ka maana hiyo “ Jiruhusu mgeuzwe kwa kufanya upya njia yenu ya kufikiri" (Rm 12: 2). Walioitwa kuwa mafundi wa muungano ili kutangaza kinabii furaha ya Injili katika utamaduni wa mawasiliano. Papa amesema wataanza katika Siku ya Mawasiliano Ulimwenguni, siku iliyotamaniwa na Mtakatifu Paulo VI, ambaye ukumbusho wake wa kiliturujia hufanyika siku hiyo hiyo. Kwa kukutana pamoja hapo Papa amesema tuombe kwa ajili ya wakati huo muhimu Wapaulini wote ; na tunaomba kwamba Familia ya Kikristo na majarida yao mengine, vitabu, televisheni, mitandao na shughuli za uundaji nchini Italia na ulimwenguni daima zifanywe upya kadiri ya Injili kwa bidii ya mtume Paulo.