Tafuta

2022.05.14 Papa Francisko amekutana na Wajimbe wa Kijiji cha Ulimwengu kilichohifadhiwa kwa walio pembezoni. 2022.05.14 Papa Francisko amekutana na Wajimbe wa Kijiji cha Ulimwengu kilichohifadhiwa kwa walio pembezoni. 

Papa Francisko:kijiji cha de François kinatoka nje ya mfumo wa ukawaida

Papa Francisko amekutana na wajumbe wa “Village de François”,kilichoanzishwa na Étienne Villemain,eneo la kikanisa asilia ambalo linashuhudia jinsi Injili inavyoweza kuangazia kila maisha katika nyanja zake mbalimbali,ikimweka mtu katika maelewano na mazingira na kueneza udugu kwa umakini pekee kwa walio dhaifu zaidi na kwa uhusiano kati ya vizazi.Kwa njia hiyo mahusiano ya kujenga binadamu ni msingi kwa kila mtu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko akianza hotuba yake washiriki wa wakazi wa Kijiji cha François, aliyokutana nao mjini Vatican Jumamosi tarehe 14 Mei 2022 amesema “Wakati Étienne Villemain, ambaye alileta mpango huu pamoja na watu wengine wengi, aliniambia juu yake kwa mara ya kwanza, sikuweza kujizuia kumwambia kwamba nilikuwa na wasiwasi juu ya kile ambacho Roho Mtakatifu angeweza kumwongoza”.  Kwa kuendelea akasema “Na tazama, sasa ninafurahi kuona kwamba mpango unaendelea mbele! Kijiji cha François ni mahali pa kikanisa ambacho kinatoka nje ya mfumo wa kawaida, ambao hutoa kitu kingine; ni Kanisa kama hospitali ya kambini, ambayo inajishughulisha zaidi na wale wanaoteseka kuliko kutetea masilahi yao wenyewe, wakichukua hatari ya mambo mapya ili kuwa waaminifu zaidi kwa ajili ya Injili.

Papa akutana na Wajumbe wa Villagge de Francois'
Papa akutana na Wajumbe wa Villagge de Francois'

Kwa kufafanua ulimwengu kama kijiji, Papa amebainisha kwamba imekuwa jambo la kawaida na linatoa wazo la ukaribu na uhusiano kati ya wakazi wake wote. Walakini, amebainisha kwamba, kuna watu wengi walioachwa kwenye ukingo wa kijiji hiki kinachojulikana. Na kwa maana hiyo ni matumaini ya Papa kwamba Kijiji cha de François kitasaidia kugundua tena kile kijiji cha kweli ni: kitambaa cha uhusiano thabiti wa kibinadamu, katika kusaidiana, kwa uangalifu kwa wale wanaohitaji, katika kuishi pamoja kwa vizazi na katika kujali, kuheshimu kazi ya Uumbaji unaotuzunguka.

Papa akutana na Wajumbe wa Villagge de Francois'
Papa akutana na Wajumbe wa Villagge de Francois'

Papa Francisko ameweka wazi juu ya uzoefu unaoishi katika Kijiji cha François, ambapo lengo lao la kuoanisha vipengele mbalimbali vya ukweli kama vile kuheshimu mazingira na maisha ya binadamu katika safari yake yote, sala, udugu na mahusiano. Na amesisitiza umuhimu kwamba binadamu kwa ujumla wake apendwe na kuingizwa katika mtandao wa mahusiano yenye kuimarisha na kujenga. Kijiji cha François, kimeendelea kuwa abasia ya zamani ya Kitrappist, ukumbusho kwa wenyeji kuweka katikati ya maisha yao, pamoja na unyenyekevu na kazi, maendeleo ya maisha ya ndani, ambayo ni, uhusiano na Yesu.

Papa akutana na Wajumbe wa Villagge de Francois'
Papa akutana na Wajumbe wa Villagge de Francois'

Papa amethibitisha “Katika Injili kwa mujibu wa Mtakatifu Yohana, anasema: “Mimi ndimi njia, ukweli na uzima". Yeye binafsi alipitia kile wanachofanya katika Kijiji cha François kwani alikuwa dhaifu, katika mikono ya mama yake na msalabani; alifanya kazi kama fundi; aliishi kwa mdundo wa majira na asili; alikulia katika kijiji ambapo vizazi vilichanganyika; alisali, alisamehe na kumpenda jirani yake. Baba Mtakatifu Francisko amewakabidhi wale waliokuwapo kwa Yesu kuwa kielelezo na msukumo katika mpango wao   na katika maisha yako ya kila siku, akiwahakikishia katika kuwasindikiza  kwa njia ya sala.

 

14 May 2022, 15:20