Tafuta

2022.05.14 Papa amekutana na Wajumbe wa Chama Cornelia de Lange 2022.05.14 Papa amekutana na Wajumbe wa Chama Cornelia de Lange   (Vatican Media)

Papa Francisko:Watu wa kijitolewa ni mfano wa utamaduni wa mshikamano

Baba Mtakatifu Francisko amewakaribisha na kuwashukuruchama cha kujitolea Cornelia de Lange,kinachosaidia watu walioathirika na ugonjwa adimu wa kijeni pamoja na familia zao.Papa amesema upendo na huruma hufanya ulimwengu kuwa wa kibinadamu zaidi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 14 Mei 2022 amekutana na Chama cha Kujitolewa kiitwacho Cornelia de Lange ambacho kinajikita kusaidia ugonjwa wa vinasaba ambao huwasumbua wale walioathiriwa na matatizo makubwa na hivyo kuhitaji kile ambacho watu wa kujitolea huhakikisha msaada na uelewa ili kuhakikisha kwamba wagonjwa na familia zao hawajiruhusu kuzidiwa na vikwazo wanavyokutana navyo njiani. Papa Francisko kwa maana hiyo akiwasalimu na kuwakaribisha amesema: “Mfano wa utamaduni wa mshikamano, ambao, kwa kuhudumia kwa kujitolea wanaoteseka, unaonesha sura ya Kikristo ya jamii”.

Papa amkutana na wajume wa chama cha kujitolea Cornelia de Lange
Papa amkutana na wajume wa chama cha kujitolea Cornelia de Lange

Papa Francisko amefurahi na kuwakaribisha huku akianzia na Mheshimiwa Vincenzo Placida, mwishoni mwa safari yake ndefu, ambayo ilimpeleka kufika Roma ili kuongeza ufahamu wa umma juu ya ugonjwa wa Cornelia de Lange. Ugonjwa huu wa nadra wa maumbile ambao husababisha usumbufu na matatizo makubwa kwa wahusika walioathirika na kwa familia zao.

Papa amkutana na wajume wa chama cha kujitolea Cornelia de Lange
Papa amkutana na wajume wa chama cha kujitolea Cornelia de Lange

Papa Francisko ametoa shukrani  zake kwa watu wa kujitolewa wa shirika lao, wanaosimama kidete karibu na kaka  na dada walio dhaifu zaidi kwa hangaiko, wakiwaunga mkono wale wanaowatunza. Utamaduni wa mshikamano unaonesha kikamilifu ushiriki katika ujenzi wa jamii ya kidugu, ambayo katikati yake ni utu. Kujitolea kunahusisha mwelekeo msingi wa sura ya Kikristo ya Mungu na mwanadamu na kwa maana hiyo ya  upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani.

Papa amkutana na wajume wa chama cha kujitolea Cornelia de Lange
Papa amkutana na wajume wa chama cha kujitolea Cornelia de Lange

Yesu, katika Injili, anatoa mwaliko wa kumpenda Mungu kwa moyo wetu wote na jirani kama sisi wenyewe tunavyojipenda (rej. Mk 12:29). Ni upendo wa Mungu unaotufanya tutambue katika wenzetu  kuwa kaka au dada wa kukaribishwa. Na kwa sababu hiyo hiyo wao wanaojitolea, wanapofanya kazi ya hisani, wanachangia kutoa sura ya kibinadamu zaidi na zaidi ya Kikristo kwa jamii yetu, Papa amebainisha.

Papa amewaomba wawe mashuhuda wa wema na huruma! Wadumu kwa utulivu na nguvu katika kazi yao, wakikabiliana na magumu ambayo wanaweza kukutana nayo kwa roho ya umoja na kuweka kila wakati msingi wa kusudi kuu la kujitolea kwao: ambayo ni, huduma kwa jirani yao. Kwa kuhitimisha amewahakikishia sala zake na Baraka  zake na kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

14 May 2022, 15:27