Papa:vita ni udanganyifu na udugu hujenga amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 30 Mei 2022 amekutana na wawakilishi wa Kiyahudi kutoka ‘B’nai B’rith International’, ambalo ni Shirika la Kimataifa la Kiyahudi lililoanzishwa mjini New York, Marekani na kwamba hatimaye wameweza kukutana mara baada ya janga la uviko lililowazuia mara kadhaa kukutana nao kwa miaka miwili. Taasisi yao ni ya kihistoria kwa muda mrefu wa uhusiano na Vatican, tangu nyakati za kuchapishwa kwa Waraka wa Mtaguso wa wa Pili wa Nostra aetate. Katika hilo wao wamejikita kutangaza kati ya ubinadamu. Papa amesema kwamba Watu wanaohitaji wana haki ya kupata msaada na mshikamano kutoka kwa jumuiya inayowazunguka hasa wana haki ya matumaini. Ikiwa uwajibu wa kutunza unatazama wote, basi huo unastahili zaidi hasa kwa Wayahudi na Wakristo, kwa sabu kusaidia wenye kuhitaji ina maana ya kufanya uzoefu wa utashi wa Aliyejuu ambaye anasema katika zaburi “hulinda wageni, hutegemeza yatima na mjane (Zab 146:9), yaani, hutunza aina zote dhaifu za kijamii, na watu waliotengwa zaidi.
Kuwasidia walio wa mwisho maskini, wagonjwa ndio njia ya dhati kwa ajili ya kuhamasisha zaidi udugu. “Kiukweli, kufikiria migogoro mingi na misimamo mikali hatari, ambayo inahatarisha usalama wa wote, ni lazima ieleweke kwamba mara nyingi sababu kubwa ya hatari inawakilishwa na umaskini wa nyenzo, wa elimu, wa kiroho, ambao unakuwa ardhi yenye rutuba ya kuongeza chuki, hasira, na itikadi. Papa Francisko amebainisha jinis ambavyo tunaishi katika kipindi ambacho amani imehatarishwa katika sehemu nyingi ulimwenguni, mitazamo ya ubinafsi na ya utaifa, inayoendeshwa na masilahi ya ubinafsi na uroho wa kupata faida, inaonekana kuchukua nafasi zaidi na zaidi. Lakini hii inaongeza hatari kwamba, mwishowe, ni utu wa mwanadamu unaopotezwa na kukanyagwa. Ili kuzuia kuongezeka kwa uovu, ni muhimu kukumbuka siku za nyuma, kukumbuka vita, kukumbuka Ubaguzi dhidi ya Uyahudi, na ukatili mwingine mwingi. Kumbu kumbu yetu ya pamoja ya kiroho inathibitisha katika kurasa za Maandiko Matakatifu na kuturejesha katika tendo la kwanza la vurugu, kuhusu Kaini aliyemuua kaka yake. Ndipo Bwana akamwambia Kaini: “Yuko wapi Abeli kaka yako? Naye akajibu: “Sijuhi. Kwani mimi ni mlinzi wa kaka yang? (Mw 4,9). Hakujali, kwani vurugu daima ni kama msindikizaji wa mabaya na sintofahamu.
Papa Francisko wa kutazama neno la ‘Yuko wapi Kaka yako’ amesema “ni muhimu kuchangamotishwa na swali hilo na kulirudia mara nyingi. Hatuwezi kubadilisha ndoto ya Mungu, iliyofanywa na ulimwengu wa ndugu, katika ulimwengu watoto wamoja, walio na vurugu na sintofahamu. Mbele ya vurugu, mbele ya sontofahamu, kurasa za maandiko matakatifu yanatupatia upendo wa udugu kwa changamoto ya mwingine. Uaminifu tulio nao kwa ubinadamu wetu unapimwa juu ya udugu, unapimwa juu ya mwingine. Katika hilo inashangaza katika Biblia, maswali makubwa ambayo Mwenyezi alimkabili mwanadamu tangu mwanzo”. Papa Francisko ameongeza kusema kwamba “Ikiwa anamuuliza Kaini kwamba “Kaka yako Yuko wapi”, kwa Adamu alikuwa amemuuliza “Huko wapi” (Mw 3,9). Hizo wapi zinajiunganishwa kwa sababu huwezi kujipata wewe mwenyewe bila kutafuta ndugu, huwezi kupata familia bila kukumbatia jirani. Hiyo ni jambo jema linalotusaidia, kwa sababu kila mmoja wetu, kila tamaduni ya kidini, na kama kila jamii ya kibinadamu, kuna hatari ya kukusanya hasira na kuongezeka dhidi ya wengine, na kufanya kwa jina zaidi kwa kutumia maneno matakatifu.
Ni kishawishi cha uwongo wa vurugu, ni uovu uliojikunyata kwenye mlango wa moyo (taz. Mwa 4:7). Ni udanganyifu wa kufikiri kwamba migogoro hutatuliwa kwa vurugu na vita. Badala yake, vurugu daima huzalisha vurugu zaidi, silaha huzalisha kifo na vita kamwe sio suluhisho bali ni tatizo, na kushindwa. Kwa sababu hii simulizi ya Kitabu cha Mwanzo kinabainisha kwamba “Bwana akamwekea Kaini ishara, ili mtu ye yote asije akampiga” . Hapa kuna mantiki ya Mbinguni: kuvunja mzunguko wa vurugu, msunguko wa chuki, na kuanza kulinda kila mmoja. Ni matashi ya Baba Mtakatifu kwamba wanaweza kuendelea na nia hiyo, kuendelea kuwalinda dada na kaka, hasa walio dhaifu na waliosahaulika. Na zidi tunaweza kuifanya kwa pamoja: tunaweza kufanya kazi kwa uchache zaidi, kwa amani, kwa haki, kwa ulinzi wa uumbaji.
Siku zote papa amesema amekuwa akipendezwa kwa moyo kuhamasisha na kuimarisha mazungumzo ya Kiyahudi na Kikatoliki, kama mtoto, kwa sababu yeye alikuwa na marafiki wa Kiyahudi shuleni; mazungumzo yanayojumuisha nyuso zinazokutana, za ishara thabiti za udugu. “Tusonge mbele pamoja, kwa misingi ya maadili ya kiroho ya pamoja, kutetea utu wa binadamu dhidi ya vurugu zote, kutafuta amani. Na Mwenyezi atubariki, ili urafiki wetu ukue na tushirikiane kwa manufaa ya wote”.