Papa Francisko:uzee ni kipindi cha hekima katika jamii chovu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika mwendelezo wa Katekesi yake Papa Francisko Jumatano tarehe 25 Mei 2022 amerudi katika mada ya uzee kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Amefanya hivyo kwa kukumbuka kurasa za Biblia za Mhubiri zinazohoji Usiku usio na uhakika wa maana ya kuishi kwamba “Kila kitu ni ubatili, kila kitu ni ukungu, kila kitu ni moshi, kila kitu ni utupu. Kauli hizi ni matunda ya elimu ya maisha ambayo imejitenga na shauku ya haki, ambayo hukumu ya Mungu ni mdhamini, ameelezea Papa Francisko, na katika uso ambao mhubiri mwenyewe anaonesha njia ya kutokea ambayo anaeleza kwamba: “Mche Mungu na uzishike amri zake, kwa maana hapa ndipo yupi mtu mzima”.
Kwa uhalisia Papa Francisko amefafanua,kwamba Mhubiri anafichua juu ya udanganyifu wa kujua yote yanayozalishwa kutokuwa na uwezo wa utashi. Ni ubatili wa maarifa bila imani na bila maadili, udanganyifu wa ukweli bila haki ambapo wamonaki wa mapokeo ya kale ya utamaduni wa Kikristo waliita uvivu. Ni moja ya majaribu ya wote, lakini pia ya zamani, Papa amesisitiza. Sio tu uvivu au unyong’onyevu, lakini ni kujisalimisha kwa maarifa ya ulimwengu bila shauku zaidi ya haki na matokeo yake. Lakini upungufu wa maana na nguvu unaofunguliwa na ujuzi huu, ambao unakataa wajibu wote wa kimaadili na upendo wote kwa ajili ya mema halisi, hufungua mlango kwa uchokozi wa nguvu za uovu, ambao ni nguvu za sababu ya kiwazimu, iliyofanywa kwa upuuzi kupindukia wa itikadi.
Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba “kiukweli, pamoja na maendeleo yote yaliyofikiwa, pamoja na ustawi wote uliofikiwa, tumekuwa jamii ya uchovu”. Amewaomba wafikirie kidogo juu ya hilo, kwamba sisi ni jamii ya uchovu. Ilitubidi kuzalisha ustawi ulioenea na tulivumilia soko la afya lililochaguliwa kisayansi. Ilitubidi tuweke kikomo kisichoweza kushindwa cha amani, na tunaona vita vikali zaidi dhidi ya watu wasio na ulinzi. Sayansi inaendelea, bila shaka, na hiyo ni nzuri, Lakini hekima ya maisha ni kitu kingine kabisa, na inaonekana kukwama. Kwa upande wa Papa Fransisko “tunakabiliwa na sababu isiyofaa na isiyowajibika ambayo inaondoa nguvu ya uwajibikaji hata juu ya dhamiri ya ukweli. Sio bahati kwa bahati mbaya kwamba msimu wetu ni wa habari za uwongo, imani potofu za pamoja na ukweli bandia wa kisayansi. Na inashangaza katika utamaduni huu wa ujuzi, wa kujua mambo yote, hata ya usahihi wa ujuzi, upotofu wa uchawi mwingi umeenea, lakini uchawi wa utamaduni wa walioelimika.
Papa Francisko amedokeza kuwa uchawi kama huo, unaongoza kwenye maisha ya ushirikina. Lakini katika uzee unaweza kujifunza kutokana na hekima ya kejeli ya Mhubiri, ufundi wa kudhihirisha udanganyifu uliofichwa kwenye pazia la ukweli wa akili usio na mapendo kwa ajili ya haki, katika wazee matajiri wa hekima na ucheshi wanaona nini kinaweza kuwasaidia vijana. Wazee huwaokoa vijana kutoka katika majaribu ya ujuzi wa kusikitisha wa ulimwengu bila hekima ya maisha. Hao ndio watakaopanda njaa na kiu ya haki kwa vijana. Papa ameongeza kwa kujiweka katikati kwamba ujarisi kama wao wazee ndiyo unapaswa kwenda mbele. Hii ni kwa sababu wao wana utume mkubwa sana duniani. Lakini, wasitafute kimbilio katika dhana hiyo ambayo ni kidogo siyo thabiti, si ya kweli, bila mizizi, kwa kusema wazi katika uchawi wa maisha.
Mbele ya ukweli ambao kila kitu kinachukuliwa kuwa kimekusudiwa bure, Papa Francisko amebainisha, njia ya kutojali kwamba inaweza kuonekana kwetu pia kuwa suluhisho la pekee la kukatishwa tamaa kwa uchungu. Hii inaweza kutokea katika msimu wowote wa maisha na hata zaidi katika uzee. Walakini, ni muhimu kupitia shida kama hiyo ili kuelewa kwamba"utamaduni unaodhania kupima kila kitu na kuendesha kila kitu huishia kutoa udhalilishaji wa pamoja wa maana, kudhoofisha upendo, kukandamiza mema pia. Kwa hakika, Papa Francisko amesisitiza kwamba ,ukiwa umefunikwa na sayansi, lakini pia usio na hisia na uadilifu sana, utafutaji wa kisasa wa ukweli umejaribiwa kuacha kabisa shauku ya haki. Kwa hakika sababu mpya ya kijinga inayojumuisha maarifa na kutowajibika imeibuka, na ambayo kwa kutuondoa kutoka kwa maadili inaonekana mwanzoni kuwa chanzo cha uhuru, na nguvu amesisitiza Papa, lakini hivi karibuni inageuka kupooza kwa mwili na nafsi. Walakini, enzi ya tatu inaweza kufungua njia mpya. Kwa upande wa Papa Francisko amebainisha mwamba ufunguo wa kila kitu ni uvumilivi wa uzee: “Ikiwa wazee, ambao sasa wameona kila kitu, huweka shauku yao ya haki, basi kuna matumaini ya upendo, na pia kwa imani amehitimisha”.