Papa Francisko:Ushirikishaji ni dawa dhidi ya utamaduni wa kutojali
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu 30 Mei 2022 amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Kike na kiume waitwao ‘Maskini wahudumu na Maskini, na wahudumu wa Mungu Mpaji liliundwa na Mtakatifu Yohane Calabria ambao wamehitimisha Mkutano wao ulioongozwa na mada: “Unabii wa Umoja”. Ni matarajio yake Papa Francisko kwamba wanaweka tayari kwenye matendo ya dhati hayo waliyoanzishwa. “Umoja wetu unazaliwa na unakuzwa awali ya yote kutokana na kuwa na uhusiano na Mungu utatu, kama inavyoneshwa katika Maandishi ya Mtakatifu Yohane yanayosikia katika kipindi cha Pasaka. Na unajionesha baadaye katika matendo ya dhati ya udugu, na katika roho ya familia, ambapo kama karama yao na mtindo wa sinodi ambao wao wamejikita nao na tayari ni mchakato wa Kanisa zima.
Papa amesema ni vizuri kuona Mashirika mawili ya kitawa wakiwa pamoja na kwa uwepo wa baadhi ya walei ambao wameshiriki kwa ari Mkutano mkuu ili kuonesha nguvu ya utambulisho wao na ushiriki wao. Kwa njia hiyo hata huo ni unabii wa umoja. Padre Calabria papa amsema kama ilivyo hata kwa watakatifu Wote alikuwa ni Nabii. Aliwaachia urithi Mkubwa na wao wanapaswa kuundeleza. Safari ambayo walifanya imeleta matunda na sio kitu kingine zaidi ya kutazama leo hii mchakato ambao Mungu anawalekeza. Mwanaume aliyeingia ndani ya Kanisa la wakati wake, alitambua kujibu mahitaji ya kwenda pembezoni mwa maisha, ili kuonesha uso wa kibaba na umama wa Mungu. Kwa kusoma kwa uaminifu ule ubunifu, na kutafuta njia mpya ili kutumiza ndoto ya Mungu katika jumuiya zao za kidini, Papa amesisitiza.
Kutokana na hilo Papa amesisitiza kwamba kwa kuhamasisha pamoja kwa imani maskini katika mapaji inawafanya kuwa mafundi wa utamaduni wa mpaji, ambao ni dawa dhidi ya utamaduni wa sintofahamu, ambapo kwa bahati mbaya Papa ameelza kwamba umeenea kwa kasi katika jamii, na kwa maana hiyo, “si kusubiri mvua kutoka angani ili kuleta suluhisho la matatizo na mali ambazo tunahitaji. Hapana. Kinyume chake inahitaji kutafuta kufanana katika Roho Mtakatifu, na Baba Yetu wa Mbinguni kwa kututunza sisi viumbe vyake hasa wale walio wadhaifu zaidi, na wadogo”. Hii ina maana ya kushirikishana na wengine kile kidogo tulicho nacho kwa sababu hasikose yeyote kitu cha lazima. Ni tabia ya utunzaji ambayo ni muhimu sana ili kupinga utamaduni wa kutupa na kubagua.
Papa Francisko amehimiza mantiki ya ushirikishanaji ambao ni sehemu ya unabii wa umoja wanaopenda kutembea pamoja. Amewakumbusha wawe na kumbu kumbu ya baba na bibi, katika utoaji wa msaada hasa walipokuwa wakifika wageni au mtu yeyote kubisha hodi mlangoni akitafuta msaada. Walitoa uji na ugali. Na huo ndio ulikuwa mtindo wa dhati wa kushirikishana. Hawapaswi kuwaazia dunia ya kuishi au kukimbilia mambo tasa yaliyopita, lakini kwa sababu ya kuchota yale yenye thamani kuu, akili ambayo inamega mkate huku ikibariki Mungu Baba, kwa matumaini kwamba mkate huo utatosha kwa ajili yetu na kwa ajili ya wenye kuhitaji. Ndivyo alivyofanya Yesu Kristo katika muujiza wa kushirikishana kwa mikate na samaki. Leo hii kuna haja ya wakristo ambao wanajua kuhudumia kwa kipawa ili kutimiza ushirikishaji.
Baba Mtakatifu amewatakia kwa maombezi ya Mtakatifu Yohane Calabria mwanzilishi wa shirika na mfano wake uwaongoze katika njia hiyo. Watafute daima kujifungua na kupokea mapya na mtindo wa Mungu alio ota ndoto kwa ajili yao. Akili yao ya kisindiza na udugu viwafanye wajihusishe sana katika huduma kwenye shirika lao na familia nzima ya shirika. Na wakumbuke daima sehemu za pembezoni ambamo Bwana anawatuma na ndizo kambi za kutangazia upendo wa Mwenyeenzi Baba kwa mtindo wa ukaribu, upole na huruma.
Papa Francisko aidha ameendelea kutoa ushauri na kuwaonya “Ninawahimiza kuthamini utajiri wa miito mbalimbali mliyo nayo ndani ya familia yenu: wanaume na wanawake watawa na walei, katika ushirika wa tofauti na kuishi wito mmoja wa ubatizo kwa uthabiti na shauku. Na mjisikie kuwa wabebaji wa karama ambayo ni karama kwa ajili ya Kanisa, na ambayo hukua kwa kadiri mnavyoiishi na kuishiriki. Hii inawapatia furaha: kutoa ushuhuda wenu kwa urahisi, kwa unyenyekevu lakini kwa ujasiri, bila ya wastani; na juu ya yote ningesema kuwa na hisia kubwa ya ubinadamu. Kuna hitaji kubwa la ubinadamu! Na pia miongoni mwenu, katika jumuiya zenu. Ninaona kuwa jambo baya sana katika jumuiya ni wakati mwelekeo huo wa ubinadamu unapokosekana. Na moja ya mambo yanayoharibu umoja huo wa kibinadamu, wa ubinadamu, ni masengenyo: tafadhali mue makini.
Kamwe msisengenye kuhusu wengine. Ikiwa una shida na dada au kaka, nenda umwaambie usoni. Na kama huwezi kumwambia usoni, umezee. Lakini usiende unapanda mahangaiko ya kuumiza na kuharibu. Masengenye ni sumu mbaya ya kifo. Na mara nyingi ni mtindo katika jumuiya. Kwa maana hiyo msifanye hivyo na uhakika kwamba haitatokea! Lakini ninasema hivyo kwa sababu muweze kuwa makini. Papa Francisko akiongeza amesema “ Ingekuwa vyema ikiwa kutoka Katika Mkutano katika kila mmoja wenu akafanya azimio la kutozungumza kamwe kuhusu mwingine awe wa kike na kiume. Nikipata shida ninamwambia usoni. Lakini nikiona siwezi kwa sababu anataaruki kidogo, bsi nitamwambia mkuu wa shirika ambaye anaweza kusuluhisha, lakini msiende mbali na kupanda mahangaiko ambayo ni mabaya kwenu.”