Papa Francisko:ujumbe kwa kongamano la kimataifa Adamu
Na Angella Rwezaula – Vtican.
Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 19 Mei 2022 amewatumia ujumbe washiriki wa Kongamano la Kimataifa ‘Adamu’ katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana katika fursa ya kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa Taaasisi ya Saikolojia. Kwa maana hiyo amewatumia salamu za moyo akiwatakia mkutano wao uwe na ufanisi na ameelezea utambuzi hai kwa kile ambacho kianzishwa na wasanifu wa taaluma hiyo. Taasisi ya saikolojia ilizaliwa chini ya usasisho wa kikanisa ulioanzishwa na Mtaguso wa II wa Vatican ambao ulikuwa unashauri: “Katika huduma ya kichungaji, sio tu kanuni za taalimungua, bali pia uvumbuzi wa sayansi za kiulimwengu, katika nafasi ya kwanza ya saikolojia na sosholojia, zinajulikana vya kutosha na kutumika, ili waamini waongozwe kwenye maisha safi na ya kukomaa zaidi kwa imani (rej Gaudium et spes, 62). Katikati ya karne iliyopita Papa amebanisha wao walipokea changamoto hiyo kwa kupeleka mbele kwa ujasiri, mchakato wa nidhamu ya utunzaji kichungaji kwa waamini katika uwanja wa utafiti na idadi kubwa ya machapisho iwe katika hatua za kichungaji na pia mafunzo.
Mtakatifu Ignatius kuhusu utunzaji binafsi
Baba Mtakatifu katika ujumbe huo amesema kwamba kama kitengo cha kitaaluma cha Chuo Kikuu cha Gregoriana tayari wamefunza zaidi ya wanaume na wanawake nusu elfu katika sayansi na sanaa ya utunzaji wa kibinafsi, kutoka katika tamaduni nyingi kwenye mabara tofauti. Wao, kwa upande wake, kwa kushirikiana na Taasisi yao, katika miongo ya hivi karibuni wametoa takriban vituo kumi na tano maalum vya waundaji, katika maeneo mbalimbali ya Afrika, Amerika ya Kusini, Asia na Ulaya. Kwa kufuata kanuni za Mtakatifu Ignatius kuhusu utunzaji binafsi, walifunza wataalam wenye uwezo wa kufungamanisha kiroho na kisaikolojia katika shughuli za kitume na kielimu katika mantiki mbali mbali, kiografia na kiutamaduni katika Kanisa.
Kongamano linakabiliana na changamoto kwa mada ya “Adamu huko wapi?
Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kwamba mkutano huo hautazami kutafakari juu ya wakati uliopita, tu lakini kwa kukaribisha urithi msingi, umetazamia kukabiliana na changamoto za wakati ujao. Kwa kuongozwa na mada ya “ Adamu huko wapi? (Mw 3,9) katika hali ya sasa ya ulimwengu Papa amesema linasikika kwa nguvu sana , swali hili, kwetu, linatung’uta na kutualika kufanya tafakari ya kina katika dhamiri na kwa ajili ya uongofu. Leo hii dunia inapitia mzozo mkubwa wa kianthropolojia (taz. Evangelii gaudium, 55), mgogoro wa maana ambao Kanisa lina wajibu wa kujibu ipasavyo na kwa ufanisi. Kabla ya macho yetu kumezwa tena na janga kubwa la vita, ambalo ni matokeo mabaya zaidi ya uharibifu wa kibinadamu, wa mtu binafsi na wa kimfumo, ambao hauchukuliwi kwa uzito vya kutosha na haujatibiwa vizuri na kutokomezwa kabisa. Kwa maana hiyo, mbele ya swali hilo ni umuhimu kujifunza kukataa maovu, kuwakomboa waliojeruhiwa au kuudhiwa katika utu wao na hitaji la haraka la kuwafunza watu wenye uwezo wa kuunda wafundaji kwa maandalizi thabiti ya kianthropolojia, na Kanisa linaendelea kutarajia, kutoka katika Taasisi hiyo, huduma bora inayotokana na ujuzi wa saikolojia na michango ya kitaalimungu na kifalsafa.
Hitaji la upyaisho kwao jitihada ya utafiti, ya mafunzo na utunzaji wa watu
Utume wao ni katika huduma ya kuhamasisha hadhi na mchakato unaoendelea wa uinjilishaji, unaopatikana kwa kutafsiri zawadi kuu ya Ukombozi iliyokamilishwa na Bwana Yesu Kristo katika ukamilifu wa uwepo wa mwanadamu. Baba Mtakatifu Francisko anawatakia kwamba maadhimishi ya miaka 50 ya Taasisi ya Saikolojia ya Chuo Kiukuu cha Kipapa cha Gregoriana, ipyaishe kwao jitihada ya utafiti, ya mafunzo na utunzaji wa watu. Na hivyo wao wako katika huduma ya Kanisa linalotoka nje kuelekea pembezoni mwa maisha ya wanaume na wanawake wa leo hii, katika utofauti wa tamaduni zao, lakini wanaounganishwa na hitaji la msaada na mwamko wa kukabiliana na magumu na changamoto za maisha. Amewashukuru kwa mchango huo, ambao uanaendana na utume hasa wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, katika huduma ya Utume wa Kanisa. Bwana awabariki na Mama Maria awalinde.