Papa Francisko:Ndoto ya Mungu ni familia moja katika nyumba ya
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tumeitwa kujenga familia ya binadamu ndiyo kauli mbiu inayoongozwa Ujumbe wa Papa Francisko katika Siku ya Kuombea Miito Duniani itakayoadhimishwa tarehe 8 Meo 2022 katika Dominika ya Nne ya Pasaka. Ujumbe wa Papa una fufungu vifuatavyo: Kuitwa kuwa wa kwanza katika utume, kuwa walinzi wa wengine na kazi ya uumbaji, kupokea mtazamo wa Mungu, kuitwa kujibu mtazamo wa upendo na ubunifu wa Mungu na kuitwa kwa ajili ya kujenga ulimwengu wa kidugu. Katika ujumbe huo. Papa anasema kwamba katika wakati wetu pepo za barafu za vita na ukandamizaji bado zinavuma na mara nyingi tunashuhudia matukio ya ubaguzi, na kama Kanisa tumeanzisha mchakato wa sinodi: tunahisi uharaka wa kutembea pamoja kwa kukuza mwelekeo wa kusikiliza, ushiriki na kushirikishana. Pamoja na wanaume na wanawake wote wenye mapenzi mema, tunataka kusaidia kujenga familia ya binadamu, kuponya majeraha yake na kuitayarisha kuelekea mustakabali bora zaidi. Kwa mtazamo huu, katika Siku ya 59 ya Kuombea Miito Duniani, ninapenda kutafakari pamoja nanyi maana pana ya “wito” katika muktadha wa Kanisa la Sinodi linalomsikiliza Mungu na ulimwengu.
Kuitwa kwa ajili ya kuwa mstari wa mbele katika utume
Baba Mtakatifu Francisko kwa ujumbe huo amebainisha kwamba Sinodi, mchakato wa kutembea pamoja ni wito msingi kwa ajili ya Kanisa na ni kwa ajili tu katika upeo huo, inawezekana kugundua na kuthamanisha miito mingine, karama na huduma. Na wakati huo huo tunajua kuwa Kanisa lipo kwa ajili ya uinjilishaji, kutoka ndani binafasi, na kutawanya mbegu za Injili katika historia. Zaidi ya hayo katika utume huo, ni uwezekano hasa wa kujiweka katika makakti wa mantiki zote za kichungaji na kabla ya hayo kuwahusisha wanafunzi wote wa Bwana. Kwa hakika, “kwa sababu ya Ubatizo uliopokelewa, kila mjumbe wa Watu wa Mungu amekuwa mfuasi mmisionari (rej. Mt 28,19). Kila mbatizwa na kwa kila aina ya kutenda kwake katika Kanisa na kwa uwezo wa elimu ya imani yake ni jambo halisi la uinjilishaji (Evangelii gaudium,120). Lazima kujitazama kwa mtindo ambao unatengenishwa Makuhani na Walei kwa kuzingatia wale wa kwanza kama wahusika wakuu na watendaji wa mwisho, na kupeleka mbele utume wa kikristo kama Watu wamoja wa Mungu, Walei na Wachungaji pamoja. Kanisa lote ni jumuiya ya uinjilishaji.
Kuitwa kuwa walinzi wa mmoja na mwingine na kazi ya uumbaji
Neno wito, halipaswi kueleweka kwa maana finyu, kwa kuwatazama wale ambao wanafuata Bwana katika njia maalum ya wakfu. Lakini wote tunaitwa kushiriki katika utume wa Kristo wa kuunganisha ubinadamu uliotawanyika na kupatanishwa na Mungu. Kwa ujumla, kila mtu binadamu, kabla ya kufanya uzoefu na mkutano na Kristo na kukumbatia imani ya kikristo, anapokea zawadi ya maisha ya wito msingi ambao kila mmoja wetu ni kiumbe aliyetamaniwa na kupendwa na Mungu na ambaye Yeye alipata wazo moja pekee na maalum kutoka katika cheche za kimungu ambaye anaishi katika maisha yetu, kwa kuchangia kufanya kukua ubinadamu unaoongozwa na upendo na kukaribishana mmoja na mwingine. Tunaitwa kuwa walinzi wa mmoja na mwingine katika kujenga uhusiano wa maelewano na wa kushirikisha kutibu majeraha ya kazi ya uumbaji ili usiharibiwe uzuri wake. Kwa hakika kuwa familia mmoja katika mshangao wa nyumba yetu ya pamoja ya uumbaji, katika maelewano na mambo yake mengi. Katika maana pana, si ya kipekee lakini hata kwa watu, jumuiya na mashirika mengine mengi yana miito
Kuitwa kupokea mtazamo Mungu hata kupitia kizingiti cha kifo
Katika wito huu mkuu wa pamoja umeingizwa mwito hasa ambao Mungu anautekeleza kwetu, kufikia uwepo wetu kwa Upendo wake na kuuelekeza kwenye lengo lake kuu, kwa utimilifu ambao unapita hata kizingiti cha kifo. Mungu alipenda hivyo kuona na kutazama maisha yetu. Michelangelo Buonarrot alikuwa anasema kwamba “kila Kipanda cha jiwe ndani mwake kuna sanamu na ni juu ya mchongaji kuigundua” . Ikiwa hiyo inaweza kuwa mtazamo wa msanii, Mungu anaweza kufanya zaidi akitutazama hivyo. Kwa mfano msichana wa Nazareth alimwona Mama wa Mungu; kwa mvuvi Simoni mwana wa Yona alimwona Petro, mwamba ambao inaweza kujenga Kanisa; kwa mtuza ushuru Levi alimwona kama mtume na Mwinjili Matayo; kwa Sauli, mtesaji mgumu wa Wakristo alimwona Paulo, Mtume wa watu. Daima mtazamo wake wa upendo unatufikia, unatugusa, unatupa uhuru na kutubadili ili tuweze kuwa watu wapya. Huu ni mwendo wa kila wito kwamba tuweze kufika mtazamo wa Mungu ambaye anatuita. Wito kama isemwavyo kwamba kuwa utakatifu sio uzoefu maalum uliochaguliwa kwa walio wachache tu.
Kama ilivyo hata kuwa na utakatifu wa mlango wa karibu(Gaudete et exsultate, 6-9), kwa namna hiyo Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kwamba hata wito ni kwa ajili ya wote, kwa sababu wote wanatazamwa na wanaitwa na Mungu. Msemo wa Mashariki ya mbali unasema kwamba: “Mwenye hekima, kwa kutazama yai, anajua kuona tai; kwa kutazama mbegu anaona mti mkubwa; kwa kutazama mdhambi anajua kuona mtakatifu”. Na ndivyo Mungu anavyo tutazama, kwa kila mmoja anaona ile nguvu, ambayo imevungwa na kisichojulikana na sisi wenyewe na wakati wa maisha yetu yote anatenda bila kuchoka kwa sababu tunaweza kujikita katika huduma ya wema wa pamoja. Wito unazaliwa namna hiyo anasisitiza Papa na kwamba, shukrani kwa sanaa ya Mungu mchongaji ambaye kwa mikono yake anatuumba, kwa sababu hiyo ni sisi ambao tunapaswa tufanye iwe kazi nzuri ambayo tunaitwa kuifanya na kuwa. Kwa namna ya pekee Neno la Mungu ambaye anatupa uhuru dhidi ya ubinafasi ni uwezo wa kujitakasa, kutuangaza na kutuunda tenda. Tujiweke kwa maana hiyo katika usikivu wa Neno, ili kujifungulia katika wito ambao Mungu anatukabidhi! Na tujifunze kusikiliza hata kaka na dada wa imani, kwa sababu ushauri wao na katika mifano yao unaweza kujificha mpango wa Mungu ambao unatuelekeza njia mpya daima za kupitia.
Tunaitwa kujibu mtazamo wa upendo na ubunifu wa Mungu
Mtazamo wa upendo na ubunifu wa Mungu unatufikia kwa namna yote ya kipekee katika Yesu. Katika kuzungumza na kijana tajiri, mwinjili Marko anabainisha kuwa “ Yesu alimtamza na akampenda (Mk 10,21). Kwa maana hiyo kwa kila mmoja wetu anaweza kuwa na mtazamo huo kamili wa Yesu wa upendo. Baba Mtakatifu Francisko anaomba kwa hakika kujiachia ili kuguswa na mtazamo huo na kuacha yeye atupeleke zaidi yetu! Na tujifunze kutazamana hata mmoja na mwingine kwa namna ambayo kwa watu tunaoishi nao na kukutana nao waweze kuhisi amepokelewa na kugundua kuwa kuna mtu ambaye anawatazama kwa upendo na anawaita kukuza nguvu zao zote. Tunapopokea mtazamo huo maisha yetu yanabadilika amebainisha Baba Mtakatifu. Yote yanageuka kuwa mazungumzo ya wito kati yetu na Bwana, lakini hata kati yetu na wengine. Mazungumzo ambayo yanaishi kwa kina yanatufanya kuwa sisi daima jinsi tulivyo, katika wito wa kikuhani ili kuwa chombo cha neema na cha huruma ya Kristo; katika wito wa maisha ya kitawa ili kumsifu Mungu na kuwa nabii wa ubinadamu mpya.
Kwa ujumla ni kila wito na huduma ya Kanisa, ambayo tunaitwa kutazama wengine na ulimwengu kwa macho ya Mungu, kwa kuhudumia wema na kueneza upendo na matendo na kwa maneno. Baba Mtakatifu Francisko katika hilo amependa kutaja uzoefu wa Dk. José Gregorio Hernández Cisneros. Wakati alikuwa anafanya kazi kmaa daktari huko Caracas nchini Venezuala alipenda kuwa mfransikakani sekulali. Baadaye kabisa akafikiria kuwa mmonaki na kuhani, lakini afya yake ikamzuia. Alitambua kwa maana hiyo kwamba wito wake ulikuwa ni taaluma ya kimatibabu, ambapo alitumia muda wake kwa namna ya pekee kusaidia maskini. Tangu wakati huo alijikita kabisa bila kujibakiza kusaidia wagonjwa waliokuwa wameambukizwa na janga la mafua yaitwayo Spagnola, lililokuwa limeenaa ulimwengu. Alikufa baada ya kugongwa na gari wakati anatoka dukani kununua madawa kwa ajili ya mzee mgonjwa wake. Ni mfano unaoonesha nini maana ya kukaribisha wito wa Bwana na kujikita nao kikamilifu na alitangazwa kuwa mtakatifu mwaka mmoja uliopita.
Kuitwa kwa ajili ya kujenga ulimwengu wa kidugu
Kama Wakristo, hatujaitwa tu, yaani, kila mmoja wetu anachangamoto binafsi kwa wito wake, bali pia ameitwa. Sisi ni kama vipande vidogo vidogo vya kutengeneza urembo( mosaic), vizuri yatari ikiwa vinachukuliwa kimoja kimoja, lakini ambacho kwa pamoja kinaunda picha. Tunang'aa, kila mmoja, kama nyota katika moyo wa Mungu na katika anga la ulimwengu, lakini tumeitwa kuuunga makundi ya nyota ambayo yanaelekeza na kuangaza njia ya ubinadamu, kuanzia na mazingira tunamoishi. Hili ndilo fumbo la Kanisa: katika uthabiti wa tofauti,lenyewe ni ishara na chombo cha kile ambacho wanadamu wote wanaitwa kuwa. Kwa hili Kanisa lazima liwe zaidi na zaidi la sinodi: lenye uwezo wa kutembea pamoja katika maelewano ya utofauti, ambapo wote wana mchango wao wenyewe wa kutoa na wanaweza kushiriki kikamilifu. Baba Mtakatifu Francisko amesema tunapozungumzia wito haihusu tu kuchagua hili au mtindo wa maisha, wa kuchagua maisha binafsi ya kuishi huduma fulani au kufuata mtindo wa karama inayovutia katika familia ya kitawa au harakati au jumuiya ya kikanisa.
Baba Mtakatifu Francsiko amebainisha kwamba hii ni kutimiza ndoto ya Mungu, ishara kubwa ya ule udugu ambao Yesu alikuwa nao katika moyo aliposali kwa Baba kuwa: “Ili wote wawe na Umoja” (Yh 17,21). Kila wito katika Kanisa na kwa maana pana hata katika jamii, inahitaji lengo la pamoja, la kufanya kusikika kati ya wanaume na wanawake wa umoja ule wingi na utofauti wa zawadi ambapo Roho Mtakatifu peke yake ndiye anajua kuzitimiza. Papa Francisko amesisitiza kuwa Mapadre, watawa, watu waliokwa wakfu, waamini walei katika safari na tufanye pamoja, kwa ajili ya kushuhudia kwamba familia kubwa ya kibinadamu, ya umoja katika upendo na sio ya kufikirika, lakini ni mpangao kwa ajili ya Mungu ambaye alituumba. Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu Francisko mesema “Tusali kwa sababu Watu wa Mungu katikati ya matukio ya majanga ya kihistoria, yanndane daima zaidi na wito huu. Tuombe nuru ya Roho Mtakatifu ili kila mmoja wetu aweze kupata nafasi yake na kujitoa yeye mwenyewe katika muundo huo mkubwa.