Tafuta

2022.05.22 Sala ya Malkia wa Mbingu 2022.05.22 Sala ya Malkia wa Mbingu  (VATICAN MEDIA)

Papa Francisko:Maisha ni zawadi ya Mungu sio wema wa kuchezea

Papa Francisko akisalimia waliofanya maandamano jijiji Roma kwa ajili ya Utetezi wa maisha amesema " tuchague maisha kwa sababu ni matakatifu na yasiokiukwa na atuweze kunyamazisha sauti za dhamiri.Amesema hayo mara baada ya tafakari na sala ya Malkia wa Mbingu kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican Dominika Mei 22.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika salamu za Papa Francisko Dominika tarehe 22 Mei 2022 ambapo pia ilikuwa ni siku kuu ya Mtakatifu Rita wa Cascia, amewasalimia washiriki mjini Roma kwa ajili ya maandamano ya kitaifa, yaliyoongozwa na kauli mbiu “Tunachagua Maisha”. Papa Francisko amewashukuru kwa kujitolea kwao katika kupendelea maisha na kutetea pingamizi la dhamiri, mazoezi ambayo mara nyingi hujaribu kuweka kikomo.

Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu

Baba Mtakatifu amebainisha kuwa “Kwa bahati mbaya, katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko katika mawazo ya pamoja  na leo tunazidi kuwa na mwelekeo wa kufikiria kuwa maisha ni bora kwa uwezo wetu wote, kwamba tunaweza kuchagua kuendesha, kuzaa au kufa tunavyopenda,  kama vile ni matokeo ya uchaguzi wa mtu binafsi”. Kwa kuongezea: “Tukumbuke kwamba maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu! Daima ni takatifu na hayawezi kukiukwa,na hatuwezi kunyamazisha sauti ya dhamiri.”

22 May 2022, 14:50