Tafuta

Papa kwa wanakipaimara:salini bila kuchoka&hifadhi nguvu ya roho mliyopokea

Papa Francisko amewasalimu vijana wa kipaimara kutoka Jimbo Kuu la Genova wakiwa katika hija yao jijini Roma.Papa amezungumzia kuhifadhi nguvu ya Roho Mtakatifu waliyoipokea na kama zawadi na umuhimu wa kuishi kidugu na kwenda mbele kama jumuiya katika Kanisa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi, tarehe 21 Mei 2022 amekutana na vijana wa kipaimara kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Genova Italia, wakiwa katika hija yao Jijini Roma. Akianza kuzungumza nao, Papa amewauliza maswali na kutoa majibu: “Wanasema kwamba Kipaimara ni sakramenti ya kuaga, kijana anapata Kipaimara na kuondoka Kanisani, ni kweli?"  na tena “ikiwa mara tu wanapofika kwenye sakramenti ya kipaimara kuwa na uwezekano wa kuondoka Kanisani ni kweli”. Hata hivyo jibu la vijana lilikuwa ‘hapana’,  kwa mwitikio wa wale vijana wote waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Marta, Vacan  ulimtia moyo Papa Fransisko, na kwa sababu hiyo akawafafanulia kwamba  ni jambo kubwa kubaki.

Papa amekutana na wanakipaimara kutoka Jimbo Kuu la Genova,Italia
Papa amekutana na wanakipaimara kutoka Jimbo Kuu la Genova,Italia

Kwa nguvu ya Kipaimara Papa amesema “ tunasonga mbele, tunakwenda mbele si tu katika Kanisa, bali katika maisha yetu wenyewe, ya kila mmoja wetu, kwa sababu Kipaimara hututayarisha kuwa watu wema, raia wema,  na Wakristo wema.  Na hivyo endeleeni”. Papa akiendelea amebainisha, kuwa: “Kipaimara ni zawadi, ambayo inapaswa kutunzwa, ambayo haipaswi kufungwa kwenye droo, lakini ambayo inapaswa kuwekwa moyoni, kwanza kwa sala, tukimwomba Bwana atupatie nguvu ya kwenda mbele, ambaye anahifadhi nguvu hii ya Roho Mtakatifu na ambayo sisi sote tumepokea”. Na “ombeni kila wakati kwa sababu Bwana alisema kwamba mkiomba, niwatawapatia”. Hata hivyo, Papa Fransisko ameonya: lakini mtu anasahau kuomba”, na kutataja methali noja ya Genova isemayo “asiyelia hana chuchu,  asiyelia hanyonyi maziwa katika chuchu akiwa na maana kwamba ni lazima kuomba na kusisitiza kwani Bwana atusikilize na atupatie nguvu za kusonga mbele.

Nguvu ya urafiki na ukarimu

Papa Fransisko akiendelea kuzungumza na vijana hao, amejikita katika suala la urafiki, kwa sababu amesisitiza tena “ndani ya Kanisa mtu yuko katika jumuiya”, akitoa kwa mfano “safari iliyowaleta Roma, jambo ambalo litawasaidia kusonga mbele”. Kwa maana hiyo Papa amezungumza na watoto, hao kwa kurudia maneno juu ya ujasiri na kusonga mbele, sala na jumuiya, maisha ya jumuiya, na kuhakikisha kwamba wanaelewa, na kisha kuwakumbusha sifa nyingine muhimu kuwa Kuwa mkarimu. Papa amesema “ukarimu wa kujitoa sisi wenyewe, kila mmoja wetu, kwa jamii, kwa mwingine. Wanasema kwamba ukarimu sio fadhila ya watu wa Genova”, lakini yeye hajuhi... “Lakini huu ni ukarimu wa pesa: Kwa maana wanasema wagenova ni wabahili”; kwa kuongeza hata yeye ana damu ya Kujenova kwa upande wa mama yake, na kwa maana hiyo anawaelewa vizuri…

Papa amekutana na wanakipaimara kutoka Jimbo Kuu la Genova,Italia
Papa amekutana na wanakipaimara kutoka Jimbo Kuu la Genova,Italia

Lakini ukarimu, daima unahitajika Papa amesisitiza. Kusaidia wengine na kuishi katika jamii. Sala, kwenda mbele katika jamii na ukarimu. Papa kwa kuhitimisha ameomba tena radhi kwa sababu mwanzoni mwa hotuba yake alianza amechelewa kufika kwa dakika 35, amewaaga kwa kuwabariki na kwa sala ya Bikiria Maria Mama Yetu na kuwatakia wasonge mbele kama kaka na dada na kama marafiki wazuri.

21 May 2022, 17:25