Tafuta

“Vita vinafanywa hivyo kujaribu silaha tulizo zitengeneza”(Mahojiano ya Papa na Gazeti la Corriere della Sera).   “Vita vinafanywa hivyo kujaribu silaha tulizo zitengeneza”(Mahojiano ya Papa na Gazeti la Corriere della Sera).  

Papa Francisko kwa Gazeti la Corriere della Sera:Niko tayari kukutana na Putin,Moscow

Papa Francisko akizungumza na Mkurugenzi Luciano Fontana wa Gazeti la jioni liitwalo:Corriere della Sera amesema:“Mimi nahisi kwamba awali ya yote kabla ya kwenda Kiev,ninapaswa niende Moscow.Jambo wazi ni kwamba ardhi hiyo inajaribu silaha.Vita vinafanya kazi hiyo:kujaribu silaha ambazo tumetengeneza”.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko akitaka kuonesha ukweli wa kutoweza kuinuka kusalimiana na Luciano Fontana na Fiorenza Sarzanini ambao ni mkurugenzi na  naibu wake wa ‘Corriere della Sera’,  yaani Gazeti la kila jioni ambaye aliwapokea katika nyumba ya Mtakatifu Marta jijini Vatican kwa mahojiano ambayo gazeti hilo limechapisha jioni tarehe 2 Machi 2022, alisema: “Nina mshipa uliochanika, nitafanyiwa upasuaji kwa njia ya upenyezo na tutaona. Nimekuwa hivi kwa muda mrefu, siwezi kutembea. Wakati mmoja mapapa walikuwa wakitembelea viti kwa kusaidiwa. Pia kuna maumivu kidogo, na unyonge.”

Papa tangu mwanzo wa vita ameingilia kati kwa ajili ya upatanisho

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika juu ya mada ya vita nchini Ukraine ambapo tangu mwanzo yeye ameweza kutoa wito wake tangu siku ya kwanza mnamo tarehe 24 Februari iliyopita na hadi sasa imekuwa shughuli za kuingiliwa kati, kuanzia na simu kwa Zelensky, kutembelea ubalozi wa kirussi, ili ujumbe wake uweze kumfikia mara moja rais Putin. “Nilimuomba Kardinali Parolin, baada ya siku ishirini za vita ili aweze kufikisha ujumbe wangu kwa Putin na mimi nilikuwa tayari kwenda huko Moscow. Kwa hakika ilikuwa lazima, kwamba kiongozi huyo aweze kuruhusu ufunguzi wa dirisha. Hatujapata bado jibu na tunaendelea kusisitiza hata ikiwa ninaogopa kuwa Putin hawezi na hapendi kufanya mkutano huo wakati huu. Lakini ubaya huo unawezekanaje husiweze kuhusimamisha? Miaka ishirini na tano iliyopita huko Rwanda tuliishi jambo kama hilo.”

Vita vinafanywa kujaribu silaha tulizozitengeneza

Kwa maneno ya Papa Francisko pia tafakari ya sababu za vita na juu ya biashara ya silaha ambayo kwa Papa daima inabaki kuwa kashfa inayopingwa na wachache. Papa Francisko amezungumza juu ya hasira iliyowashwa labda, kutokana na kusikika kwa NATO kwenye mlango wa Urussi ambapo ilisababisha kiongozi huyo kujibu vibaya na kuibua mzozo. “Sijuhi namna ya kujibu kwa sababu niko mbali sana, kwa swali la kama ni sawa kuwapa Waukraine”. Na kwa kufikiria amesema: “jambo la wazi ni kwamba silaha zinajaribiwa katika ardhi hiyo. Vita vinaendeshwa ili kujaribu silaha tulizozalisha”. Warussi sasa wanajua kuwa mizinga haitumiki sana na wanafikiria mambo mengine. Vita vinapiganiwa kwa hili: kujaribu silaha ambazo tumezalisha”. Wachache wanapinga biashara hizi, badala yake zaidi inapaswa kufanywa zaidi na zaidi na Papa anataja kusimamishwa huko Genova kwa msafara wa kubeba silaha kwenda Yemen na ambapo wahudumu walichagua miaka miwili au mitatu iliyopita kuacha. Na tena huko Moscow Papa anatafuta uwezekano wa kuweza kufanya pamoja na patriarki Kirill wa Kanisa la Kiorthodox.

Hakuna safari ya Kiev iliyopangwa kwa sasa ni kwenda Moscow

Kwa kuelezea juu ya juhudi zilizofanywa au zinazopaswa kufanywa ili kukomesha kuongezeka kwa vurugu, Papa Francisko amefafanua kwamba: “Siendi Kiev kwa sasa. Ninahisi sihitaji kwenda huko. Kwanza lazima niende Moscow, kwanza nikutane na Putin. Lakini mimi ni kuhani pia, nifanye nini? Ninafanya niwezavyo. Ikiwa Putin atafungua mlango” .... Na ametaja juu ya mazungumzo yake kwenye mtandao wa zoom kwa dakika 40 aliyofanya tarehe 15 Machi iliyopita na uhalalishaji wa vita vilivyotajwa na Kirill, na amerudia kuelezea juu ya kuharishwa kwa mkutano uliokuwa umepangwa mwezi Juni huko Yerusalemu ambapo katika mahojiano hayo Papa Francisko amesema: “Nilimsikiliza na nikamwambia: sielewi chochote kuhusu hili. Ndugu, sisi sio viongozi wa serikali, hatuwezi kutumia lugha ya siasa, bali ya Yesu, sisi ni wachungaji wa watu wale wale watakatifu wa Mungu, kwa hili tunapaswa kutafuta njia ya amani, kukomesha ufyatuaji risasi za silaha. Patriaki hawezi kujigeuza kuwa kijana wa kutumikia Putin. Nilikuwa na mkutano uliopangwa pamoja naye huko Yerusalemu mnamo Juni 14. Ingekuwa kwa mara ya pili kuonana uso kwa  uso, ambapo hapakuwapo na kitu chochote kinachohusiana na vita. Lakini sasa yeye pia amekubali, kusimamisha maana ishara hiyo isingeweza kueleweka.

Ulimwengu ulio katika vita kwa maslahi ya kimataifa

Mtazamo wa Papa Francisko aidha unaongezeka tena kuzungumzia haki za watu katika ulimwengu ulio katika vita, kwamba “vita vya tatu vya dunia, mara nyingi viliibuka na kuogopwa. Sio kengele”, amebainisha, lakini “utekelezaji wa mambo kama vile: Siria, Yemen, Iraq, na katika Afrika ni vita moja baada ya nyingine. Kuna vipande vya maslahi ya kimataifa katika kila kukicha. Mtu hawezi kufikiri kwamba nchi huru inaweza kupigana vita na nchi nyingine huru. Huko Ukraine inaonekana kuwa ni watu wengine walioanzisha mzozo huo. Kitu pekee ambacho kinalaumiwa kwa Ukraine ni kwamba waliitikia huko Donbass, lakini tunazungumzia miaka kumi iliyopita. Hoja hiyo ni ya zamani. Bila shaka ni watu, wanao onesha uimara na jasiri”.

Kashfa ya msalaba: hakuna utashi wa kutosha kwa ajili ya amani.

 Katika suala la njia ya Msalaba, Papa amerudia kutazama Njia ya Msalaba iliyofanyika siku ya  Ijumaa Kuu iliyopita katika magofu ya kizamani ya Colosseo  na maombi kwa upande wa Ukrane ambapo yalisababisha kusimamishwa kusoma tafakari katika kituo cha kumi na tatu, kilichoongozwa na mwanamke wa Kirussi na wa Kiukreni. Papa Francisko ameelezea juu ya mazungumzo aliyokuwa nayo na Msimamizi wa Sadaka ya Kitume Kardinali Krajewski, ambaye wakati wa Pasaka alikuwa  huko Kiev kwa mara ya tatu aliyokuwa ametumwa na Papa tangu mwanzo wa mzozo huo.  Papa alisema: “Nilimpigia simu Krajewski ambaye alikuwepo huko na akaniambia: acha, usisome sala hiyo. Wako sahihi hata kama sisi hatuelewi kabisa. Basi nilibaki kimya. Wao wana unyeti kwa sababu wanahisi kushindwa au watumwa kwa sababu katika vita ya pili ya dunia walilipa gharama kubwa sana. Watu wengi waliokufa, ni watu mashahidi. Lakini pia tuwe makini kwa kile kinachoweza kutokea sasa huko Transnistria ”. Lakini tarehe 9 Mei inaweza kuwa ndiyo mwisho wa yote. Kutoka na mkutano na Waziri Mkuu wa Hungaria Viktor Orbán, mnamo Aprili 21 iliyopita mjini Vatican, Papa amesema amefahamu kwamba: “Warussi wana mpango. Kwa njia hiyo pia tungeelewa kasi ya kuongezeka kwa vita hivyo siku hizi. Kwa sababu sasa sio Donbass tu, ni Crimea, ni Odessa, inachukuliwa bandari ya Bahari Nyeusi kutoka Ukraine na ndiyo yote. Sina matumaini lakini lazima tufanye kila ishara inayowezekana ili kukomesha vita”, amesema Papa.

Italia, CEI: Natafuta kardinali mwenye mamlaka ambaye anataka ubunifu

Hatimaye, mtazamo wa Papa Francisko, katika mazungumzo na hao wakuu wa Gazeti la Corriere della Sera, umetazama Italia, siasa tangu rais Napolitano hadi Mattarella na uhusiano mzuri sana na Waziri Mkuu Mario Draghi, ambaye amemfafanua kuwa ni “mtu wa moja kwa moja na rahisi”. Na tena “heshima” kwa Emma Bonino, hata kama hashiriki mawazo yake “lakini anajua Afrika kuliko mtu yeyote yule”. Kisha marekebisho katika mji wa Vatican na Kanisa la Italia yakingojea rais mpya wa Baraza la maaskofu kwamba “Mojawapo wa mambo ninayojaribu kufanya ili kupyaisha Kanisa la Italia ni kutobadili maaskofu kupita kiasi”. Kardinali Gantin alikuwa anasema kuwa askofu ni mchumba wa Kanisa, kila askofu ni mchumba wa kanisa kwa maisha yote. Wakati kuna tabia ni nzuri. Hii ndiyo sababu ninajaribu kuwataja makuhani, kama ilivyotokea huko Genova, Turin, Calabria. Ninaamini huu ni upya wa Kanisa la Italia”. Kwa jina atakalochagua mkuu wa maaskofu, katika mkutano ujao wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI), amefafanua: “Ninajaribu kutafuta mtu ambaye anataka kufanya mabadiliko mazuri. Ninapendelea awe kardinali, awe na mamlaka. Na kwamba ana uwezekano wa kuchagua katibu, ambaye anaweza kusema kwamba ninataka kufanya kazi na mtu huyu”.

MAHOJIANO YA PAPA NA MKURUGENZI WA GAZETI LA CORRIERE DELLA SERA
03 May 2022, 14:30