Tafuta

Papa amekutana na wanafunzi na maprofesa wa Chuo Kikuu cha Macerata. Papa amekutana na wanafunzi na maprofesa wa Chuo Kikuu cha Macerata. 

Papa:Kuna haja ya mazungumzo katika ulimwengu uliozoea kubagua

Papa Francisko akizungumza na Jumuiya ya Chuo Kikuu kutoka Macerata Italia,amehamasisha kuchukua njia ya mazungumzo ili waweze kuzaa matunda mema katika ulimwengu uliozoea njia za kubagua.Amekumbuka Padre Matteo Ricci,mwalimu wa makutano.Na amewakabidhi changamoto hasa za kukutana na fahamu tofauti na mtu na sio kujaza kichwa tu bali kuzaa maelewano ya kibinadamu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na maprofesa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Macerata, Italia,Jumatatu tarehe 9 Mei 2022. Katika hotuba yake amesema alivyoshangazwa na uwakilishi  wa hotuba ya  Chuo chenye upeo mpana wa urafiki kati ya Mashariki na magharibi: mkutano kati ya tamaduni tofauti; janga la vita, janga la uhamiaji na hata kutaja maneno ya Seneca! (Lucius Annaeus Seneca kijana (karibu 4 KK - 65 BK), alinajulikana sana kama Seneca, na alikuwa mwanafalsafa wa Kirumi wa Stoiki, mwanasiasa, mwigizaji na mtunzi kutoka enzi za baada ya Agostiniani ya fasihi ya Kilatino). Baba Mtakatifu akifafanua kuhusu  amani amesema kwa hakika Chuo Kukuu ni chuo cha ulimwengu na ndivyo kinapaswa kuwa mahali pa ufunguzi, wa akili, maono ya fahamu, maono ya maisha, ya ulimwenyi na wa historia. Kwa asili kuanzia na matarajio msingi ya mafunzo ya kina na njia kwa muktadha wa nidhamu, lakini pia ufunguzi daima wa fahamu za ulimwengu na za binadamu ambaye ndiye fungamani.

Papa amekutana na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Macerata Italia
Papa amekutana na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Macerata Italia

Papa amesema  upeo huo, ni mara mbili ikiwa tunafikiri kwamba kila mtu, kwa hiyo kila mwanafunzi anayevuka kizingiti cha chuo kikuu na kuhudhuria kwa miaka michache, kila mmoja wao  anakuwa binafsi na pia katika  ulimwengu. Katika chuo kikuu, kwa maana hiyo ulimwengu wa aina mbili unakuana: ulimwengu wa maarifa, na ule wa mwanadamu; sio wa mtu wa kawaida, ambaye hayupo, lakini hasa wa mtu huyo, wa yule kijana, mvulana na msichana, na historia yake na utu wake, ndoto zake na sifa zake za kiakili, maadili, kiroho ..., mipaka yake.  Kila mtu ni ulimwengu, ambao ni Mungu pekee anayejua kikamilifu, kwa heshima isiyo na kifani. Hii Baba Mtakatifu Francisko amesema, inaweza kuwa  ni changamoto ya chuo kikuu: ya kuleta pamoja nyanja hizi mbili, ile ya ulimwengu  na kibinafsi, ili waweze kufanya mazungumzo,na kutokana na mazungumzo haya ndipi ukuaji wa ubinadamu unakuwapo. Ukuaji kwanza kabisa wa mwanafunzi mwenyewe, ambaye ameundwa, hukomaa katika maarifa na uhuru, katika uwezo wa kufikiria na kutenda, kushiriki kwa umakini na ubunifu katika maisha ya kijamii na kiraia, na umahiri wake wa kitamaduni na kitaaluma.

Papa amekutana na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Macerata Italia
Papa amekutana na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Macerata Italia

Papa amekumbuka tafakari ya Mtakatifu John Henry Newman kuhusu chuo kikuu, ambapo anaandika kuw:  Katika mazingira ya chuo kikuu kijana anaunda tabia ya kiakili ya maisha, ambayo sifa zake ni uhuru, haki, utulivu, kiasi na hekima, na anaongeza kusema: “Ningeonesha hii kama matunda maalum ya elimu iliyotolewa na chuo kikuu, ikilinganishwa na maeneo mengine au njia za kufundisha, na hili ndilo lengo kuu la chuo kikuu katika huduma ya wanafunzi wake (Wazo la chuo kikuu, 1873, V, 1). “Wazo hili la chuo kikuu sio na  halihusiani na kile ambacho kielelezo kilitazama  na kujaza vichwa vyetu na vitu ... badala yake: Ni mtu mzima ambaye lazima ahusike hapo, utashi wake  na jinsi ya kuhisi sio tu ya kufikiri na pia njia ya kutenda. Kuna maelewano ya kibinadamu, bila kufikiria chuo kikuu kama kiwanda cha ubongo ambacho basi hawajui la kufanya kwa mikono yao au kwa moyo ... Wazo hili la kibinadamu la chuo kikuu ni muhimu”, Papa amesisitiza.

Papa amekutana na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Macerata Italia
Papa amekutana na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Macerata Italia

Papa amesema kwamba “Ukuaji huu wa binadamu wa watu unaweza kuwa tu na matokeo chanua kwa jamii. Kwa hivyo, kuwekeza katika mafunzo, shule na vyuo vikuu ni uwekezaji bora kwa mustakabali wa nchi. Tunajua hili, mara nyingi tunasikia likirudiwa, lakini maamuzi thabiti hayafanywi kila wakati”. Kipengele kingine ambacho Papa amesisitiza,  na ambacho kiliguswa pia na Gambera cha Chuo ni kile cha kukutana kati ya tamaduni tofauti. “Tunajua vizuri kwamba hii sio moja kwa moja. Haitoshi kuwaleta pamoja maprofesa na wanafunzi kutoka asili tofauti. Tunahitaji kuendeleza utamaduni wa kukutana. Na hakika chuo kikuu ni mahali pazuri pa kufanya hivyo. Macerata palikuwa mahali pa kuzaliwa kwa bingwa mkuu wa utamaduni Padre Matteo Ricci”.

Papa amekutana na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Macerata Italia
Papa amekutana na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Macerata Italia

Yeye anasifika, si kwa sababu tu ya  mambo aliyoanadikaa  ni kwa sababu ya kuwa mtu wa kukutana, mtu wa utamaduni wa kukutana, mtu aliyepita zaidi ya kuwa mgeni, akawa raia wa kwa sababu raia wa watu kwa sababu huu ni utamaduni wa kukutana. Na hakika chuo kikuu ni mahali pazuri pa kufanya mkutano huu. Macerata palikuwa mahali pa kuzaliwa kwa bingwa huyu maarufu. Amewapongeza Baba Mtakatifu si kwa sababu ya kulinda na kuhifadhi kumbukumbu yake na kuhamasisha  masomo juu yake, lakini  kwa kujaribu kusasisha mfano wake wa mazungumzo ya kitamaduni.  Papa ameongeza kusema kwamba kwa sasa kuna haja kubwa sana leo hii katika ngazi zote, kuchukua njia hii kwa lengo kuu la njia ya mazungumzo! “Wakati mamlaka za ulimwengu zimezoea njia ya kutengwa, utamaduni wa kutupa na kumbe kinachohitajika ni njia ya mazungumzo. “Lakini je ni lazima  kupoteza muda na mazungumzo?”. Ameuliza swali, Papa na kujibu: Ndio, poteza wakati kwa sababu hiyi basi ndiyo inazaa matunda kwa njia kubwa na nzuri zaidi”.

HORUBA YA PAPA KWA JUMUIYA YA CHUO KIKUU CHA MACERATA ITALIA

 

09 May 2022, 15:39