Papa Francisko:kujichafua mikono katika pembe za dunia sio sadaka ni udugu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuishi karibu na watu katika mitaa, kuunganisha wahamiaji katika jamii, si kwa ajili ya upendo tu, lakini pia kukabiliana na vipindi vya baridi vya upungufu wa idadi ya watu na kufungulia uchumi wa Kikristo, ambao ni jumuiya na unashirikishwaji na watu. Ni tafakari ya Baba Mtakatifu katika mkutano na wawakilishi viongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Mshikamano unaowakutanisha watu wa kidini ambao wameshiriki mjini Davos, katika Kongamano Uchumi Dunia linaloendelea, na wamejadili uongozi na ushirikishwaji wa kijamii wa watu walio katika mazingira magumu zaidi. Papa Fransisko kwa maana hiyo kwa kikundi cha Mfuko wa Mshikamano Kimataifa, amewatia moyo kuwa karibu na jamii iliyotupwa na kwamba Wakristo wengi sana wana mioyo michafu kwa ubinafsi na halo ni kama toleo jipya la Ufarisayo wa kale zaidi hivyo ni muhimu kuendelea kuelekeza katika uchumi wa jamii.
Papa Francisko amezungumza hayo Jumatano tarehe 25 Mei 2022 na kusema kwamba “Ninapenda watu ambao wanaishi pembezoni kwa sababu Yesu alikwenda pembezoni: Alikwenda huko kuonesha Injili. Na kwamba sehemu za pembezoni zinaweza kuwa za mwili, lakini pia za roho kwa sababu kuna watu ambao wana mali kidogo lakini wana roho zilizoharibiwa. Mtindo wa Mungu ni ukaribu, na kuna watu wengi wanaohitaji ukaribu huo. Kwenda pembezoni, kwenda kutafuta watu wasiohesabika, walioachwa na jamii ni kwa sababu tunaishi katika utamaduni wa ubadhirifu, na watu wanatupwa kwa njia hiyo ni kwenda huko kama Yesu alivyofanya”.
Papa Francisko ametoa mifano mingi na kusema kwamba “Misemo hiyo ya kidini iwe ni ya makutaniko au ni Wakristo wanaojitenga ili kutunza imani wanaotaka kuwa na roho safi, lakini hawana ukaribu, pengine watakuwa na roho safi; lakini wana mioyo michafu ubinafsi na kwamba hili ni toleo la upya la Ufarisayo wa zamani zaidi”. Papa Fransisko amejikita suala wahamiaji, na kurudia vitenzi vinne msingi vinavyorejea kwao vya kukaribisha, kusindikiza, kuhamasisha na kuunganisha. Kwa maana hiyo amesema “, tunahitaji kufanya njia ya ushirikiano katika jamii: Sio kazi ya upendo tu, na wahamiaji, kuwaacha huko, hapana. Ni kuwachukua na kuwaunganisha, na elimu, na upangaji wa kazi na mambo haya yote” .
Katika kukumbuka mkasa wa Zaventem (shambulio kwenye uwanja wa ndege wa Brussels na vifo 11 vilivyodaiwa kufanywa na shambulizi la kiitikadi linalojiita la Kiisilamu), lililofanywa na Wabelgiji vijana Papa Francisko amesema “watoto wa wahamiaji, wasiojumuishwa, waliowekwa kwenye pembenei, wanahitaji ujumuishwaji . Kwa sababu mhamiaji ambaye hajaunganishwa yuko katikati, nusu, na hatari. Ni hatari kwake, masikini, kwa sababu atakuwa mwombaji daima. Pia ni hatari kwa kila mtu. Kuunganisha, sio kuwa na wahamiaji kama kokoto kwenye viatu vyako, ambavyo vinakera”.
Papa Francisko amesema kuwa “Inabidi tujiangalie ili tuwaelewe wahamiaji, hii ndiyo elekezo kwa sababu wengi wetu ni watoto au wajukuu wa wahamaji, pia kwa kurejea kwetu wenyewe”. “Lazima tuangalie mizizi na pia kuangalia Ulaya ambayo ilifanywa na wahamiaji na ambayo leo hii kwa maendeleo makubwa inaihitaji msaada. Kwa sababu kuna majira ya baridi ya upungufu wa idadi ya watu, ambapo hakuna watoto, na kwa siku zijazo na kila wakati watu wanaokuja lazima waunganishwe.
Na upande hup Papa amewashukuru sana kwa kile wanachofanya na kwamba sio kutoa sadaka tu bali ni udugu. Papa Fransisko akizungumzia juu ya uchumi na lengo la Mfuko wa Kimataifa wa Mshikamano, ameonya kuwa uchumi lazima sasa ugeuzwe: Ni lazima tuhamie kutoka katika uchumi huria, kwenda katika uchumi unaoshirikishwa na watu, na kuelekea katika uchumi wa jamii. Na kazi ya kutosha inamefanywa juu ya hilo na wachumi vijana , wakiwemo wanawake. Hapo ametaja hatua zilizo mbele kwa kutifiria uchumi uliofanywa na Mariana Mazzucato, mwanauchumi wa Italia na msomi mwenye uraia wa Marekani, binti wa wahamiaji nchini Marekani na kwa wanawake wengine baadaye akaeleza kwa nini tunapaswa kufikiria juu ya uchumi usio na mizizi zaidi katika watu.
“Hatuwezi kuishi na muundo wa kiuchumi unaotokana na waliberali na wa mwanga, ma wala hatuwezi kuishi na mfumo wa uchumi unaotokana na ukomunisti. Tunahitaji uchumi wa Kikristo, na kwa maana hiyo tujikite na hilo. Na kwa hiyo, bila kutaka kukaa katika taratibu, Papa Fransisko amezindua wito wake akiomba kila mara kumwombea si dhidi ya”… : lakini pia wap kusonga mbele, kwa kuchafua mikono yao na amewaomba wathubutu kwani maeneo mengu ya Asia Kusini-mashariki, sehemu ya Afrika, sehemu ya Amerika ya Kusini. Ni maeneo mengi ambayo yamejeruhiwa mioyo.