Tafuta

2021.01.09 Papa> Pauline Jaricot 2021.01.09 Papa> Pauline Jaricot 

Papa Francisko Jaricot ni mwanamke jasiri kwa ajili ya utume

Papa Francisko mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana amekumbuka Mwanzlisho wa Matendo ya Utangazaji wa Injili, aliyetangazwa kuwa mwenyeheri Pauline Jariko huko Lyon nchini Ufaransa na Kardinali Tagle Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu kwa waamini na mahujaji waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Dominika tarehe 22 Mei 2022 amekumbusha jinsi ambavyo huko Lyion nchini Ufaransa alasiri Dominika alikuwa atangazwe mwenyeheri Pauline Maria Jaricot, Mwanzilishi wa Matendo ya Utume, kwa ajili ya kusaidia utume. Papa amesema kwamba mwamamke huyo mlei aliyeishi kabla ya nusu ya 1,800 alikuwa mwanamke jasiri, makini kwa ajili ya mabadiliko ya nyakati katika maono ya ulimwengu wa utume wa Kanisa.

Kwa kuongezea Baba Mtakatifu amesema kwamba mfano wake utoe chachu ya shauku ya kushiriki, kwa sala na kwa upendo, katika kueneza Injili ulimwenguni. Na hatimaye ameomba apigiwe makofu mwenyeheri huyo.

Hata hivyo Ibada ya misa takatifu hiyo iliadhimishwa na Kardinali Luis Antonio Tagle, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, ambaye katika mahubiri yake yaliyojikita katika upendo kwa Yesu, amekumbuka unyenyekevu wa Pauline Jaricot kwa Roho Mtakatifu aliyemhimiza kwa mawazo na mipango mipya, kwa ajili ya kueneza Injili na huduma kwa maskini. Katika hili alifuata utamaduni mkubwa wa kiroho, wa kimisionari na hata kijamii wa Kanisa la Lyon nchini Ufaransa .

Kardinali amesema kuwa walitafakari juu ya karama tatu: zawadi ya neno la Yesu, zawadi ya Roho Mtakatifu na zawadi ya amani kutoka kwa Yesu. Yeyote anayepokea zawadi hizi kwa furaha anapendwa na kumpenda Yesu, mmisionari wa Kanisa; kaka o dada wa maskini na chombo cha udugu na amani ya ulimwengu kote. Mwenyeheri Pauline Jaricot alikuwa na haya yote, kwa sababu alikaribisha karama za Mungu na kwa maana hiyo Kardinali ameongeza kusema “Sasa ni zamu yetu ”.

Maisha ya mwanamke huyo, kati ya mwisho wa karne ya kumi na nane na karne ya kumi na tisa, ni juu ya kutoa kwa walio wadogo zaidi. Miongoni mwa shughuli zake, msingi wa chama cha kiroho kiitwacho “Watengenezaji" na shirika la kikundi cha wasichana kumi, ambao kila mmoja alijitolea kuombea utume . Mnamo tarehe Mei 1822, Chama cha Kueneza Imani kilizaliwa rasmi. Miaka mia moja baadaye, Papa Pius XI alitambua moyo wake wa kimisionari na huduma kwa Kanisa la Ulimwengu kwa kutangaza Kazi ya Uenezaji wa Imani kuwa ya Kipapa.

22 May 2022, 14:38