Papa Francisko:imani sio jambo la wazee,inapaswa iheshimiwe
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko katika tafakari yake ya Kateseki Jumatano tarehe 4 Machi 2022, akiwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro, ameongozwa na somo kutoka Kitabu cha 2 Wamabakabayo 6,18.23-25. Kwa maana hiyo akianza tafakari amesema: “Katika mchakato wa safari ya katekesi hii kuhusu uzee, leo tunaingia kuona mtu wa kibiblia mzee mmoja kwa jina Eleazari, aliyeishi nyakati za mateso ya Antioko Epifane. Ni sura nzuri. Sura yake inatupatia ushuhuda wa uhusiano maalum ambao upo kati ya uaminifu wa uzee na heshima ya imani. Ni wa kujivunia sana. Akiendelea Baba Mtakatifu amependa kuzungumzia hasa heshima ya imani na si tu kwa udhati, kutangaza, wa uvumilivu wa imani. Heshima ya imani imekuwa mara kwa mara chini ya shinikizo, hata vurugu, ya utamaduni wa watawala, ambayo inataka kuidhalilisha kwa kuichukulia kama uvumbuzi wa kiakiolojia, au ushirikina wa zamani, ukaidi watafuta makosa ya wakati wa wanahabari na wengine.
Simulizi ya kibiblia inasimulia jinsi ambavyo wayahudi kwa sheria ya mfalme ililazimu kula nyama inayotolewa sadaka kwa miungu. Papa amewashauri kusoma barua hiyo kwa maana ni nzuri. Na ilipofikia zamu ya Eleazari mtu mzee ambaye mwenye kuheshimiwa sana na wote, karibu miaka 90 hivi, mwalimu wa sheria, maafisa wa sheria walimshauri adanganye kama vile anakula nyama. Papa ameongeza huu ni unafiki wa kidini. Kuna unafiki mwingi sana wa kidini, na wa kikuhani. Kwani walimwamba ufanye kinafiki na hakuna ambaye atajua. Na kwa kufanya hivyo angeweza kuokoka na wale walikuwa wakisema kwa niaba ya urafiki angekubali kwa ishara ya huruma na upendo. Unafiki wa kweli huo. Na zaidi ya yote walisisitiza kuwa ilikuwa ni ishara ndogo ya kujifanya anakula na ishara isiyo na maana.
Ni kitu kidogo lakini jibu la Eleazari ni zuri sana la kushangaza. Kiini ni chake ni kwamba kutoheshimu imani katika uzee, kwa ajili ya kupata maisha kidogo tu, hayawezekani kulinganishwa na urithi ambao unapaswa kuachwa kwa vijana, kwa kizazi kizima kitakachokuja. Ana akilia huyo Eliazari, amepongeza Papa. Mzee ambaye aliishi kwa urithi wa imani yake katika maisha yote, na sasa anapaswa eti adanganye imani yake kuadhibu kizazi kipya kwa kufikiria kuwa imani nzima ilikuwa ni udanyaifu, uwekezaji wa kijuu juu ambao unekweda kuwachwa kwa kufikiria kihifadhi undani. Na sio hivyo, alisema Eliazari. Papa ameongeza kusema kuwa tabia ya namna hiyo haiwezi kuheshimu imani na wala mbele ya Mungu.
Na matokeo ya kudharau kwa hili la nje iltakuwa mbaya kwa mambo ya ndani ya vijana. Lakini kuna uthati wa mtu huyo anayefikiria vijana! Anafikiria juu ya urithi wa baadaye, anafikiria juu yake kidogo. Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema kuwa hili ni nzuri hasa kwa wazee ambao wanaonesha kuwa na uamuzi stahiki na mahali pasipobadilishwa kwa ushuhuda huo. Mzee ambaye, kwa sababu ya udhaifu wake, alikubali kufikiria zoezi la imani kuwa lisilofaa, angefanya vijana waamini kwamba imani haina uhusiano wa kweli na maisha. Inaweza kuonekana kwao, tangu kuanzishwa kwao, kama seti ya tabia ambazo, ikiwa ni lazima, zinaweza kuigwa au kufichwa, kwa sababu hakuna hata moja ambayo ni muhimu sana kwa maisha.