Tafuta

2022.05.05 Papa amekutana na Washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Mama wakuu  ulimwenguni. 2022.05.05 Papa amekutana na Washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Mama wakuu ulimwenguni. 

Papa:kuhudumia,kusikiliza&kufunga majeraha ya ubinadamu

Ni lazima tujiweke kwa upya katika miguu ya wanadamu,ambapo nafasi halisi ya kitaalimungu inaundwa.Kwa hakika mtazamo huu utakuwa chanzo cha furaha na ukuaji.Kwa sababu ni kutoka hapo, yaani chini,kwamba kila mmoja wetu anaweza kusoma tena uzuri wetu na historia yetu.Papa ametoa mwaliko wa kutoogopa kutafuta kufanya huduma mpya na njia mpya za kutumia mamlaka kiinjili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuanzia tarehe 2 ulifunguliwa Mkutano Mkuu wa XII wa Umoja wa Kimataifa wa Mama wakuu inaofanyika jijini Roma unaudhuliwa na washiriki karibu 700 ambapo karibu 520 wako mjini Roma na wengine wanafuatilia kwa njia ya mtandao. Washiriki wametoka  katika nchi 71 ulimwenguni ambao wengu wao wanawakilishwa na Ulaya kutokana na kwamba ndiko kuna Nyumba mama. Hawa mama wakuu pia kutoka bara la Afrika hasa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,  Asia, India,  Amerika Kaskazini, Marekani, Amerika ya Kanisa na Kusini, Mexico na Brazil. Mada ya kuu ya mkutano wao ni Sinodi kwa kuwa na watoa mada kama 10 hivi ambapo kauli mbiu ilikuwa imegawanyika katika vipengele:Kuathirika, Mchakato wa Sinodi, Maisha ya Kitawa na Sinodi, Pembezoni, na Wito katika kufanya mabadiliko. Alhamisi tarehe 5 Mei  2022 washiriki hao wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko. Papa Francisko anawasili kwa kiti cha magurudumu kwenye Ukumbi wa Papa Paulo VI , kwa sababu ya maumivu ya goti ambayo yamekuwa yakimfanya ateseke kwa muda mrefu lakini ambayo hawaguweza kukatisha na wala kupunguza jitihada zake,  na ameweza kuzungumza na watawa hao bila kusoma akawakabidhi hotuba yake aliyokuwa ameitayarisha kwa lugha ya kihispania.

Papa amekutana na Umoja wa  Mama wakuu wa Mashirika ya kitawa
Papa amekutana na Umoja wa Mama wakuu wa Mashirika ya kitawa

Katika ujumbe wake alioukabidhi unakazia matukio mawili ya Biblia: kwanza Yesu akiosha miguu ya Petro  wakati wa kalamu kuu na Maria Magdalena aliyepata ukombozi mkubwa kwa kukutana kwake na Yesu. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba licha ya udhaifu, akijiweka kwa upya katika miguuni ya wanadamu na kutumikia Petro ilimbidi kubadili mawazo yake, akijiruhusu kutumikiwa. Na wakati Magdalena alichaguliwa kuwa mtume licha ya historia yake ya zamani. Kutokana na tafakari hizi mbili, ndipo hitaji limerejea katika mtazamo  hasa  kuhudumiana na kusikilizana kwa ajili ya ushiriki kamili wa kikanisa. Baba Mtakatifu amebainisha kwamba kanisa linajifunza kutoka kwa Mwalimu wake kwamba, ili liweze kutoa maisha yake, kwa kuwahudumia wengine, linaalikwa kutambua na kukubali udhaifu wake, na kuanzia hapo, kusujudu mbele ya udhaifu wa mwingine. Kwa mtazamo hu, pendekezo ni kuishi mamlaka kama huduma. Papa Francisko amebaki katika  vipengele vya udhaifu vinavyohusiana na maisha ya kuwekwa wakfu na miito ya kitawa na wala hakuacha kupunguza umuhimu wa watawa wanavyo wazia idadi ya wajumbe katika mashirika,  vile vile kutazama kazi na umuhimu wa kijamii, na kwa maana hiyo amesisitiza na kuwashauri watawa hao  kuwa na mtazamo chanya.

Papa amekutana na Umoja wa  Mama wakuu wa Mashirika ya kitawa
Papa amekutana na Umoja wa Mama wakuu wa Mashirika ya kitawa

Baba Mtakatifu anasema kwamba kuwa watumishi “si suala la utumwa.  Kujishusha haimaanishi kugeuka nyuma kwa majeraha ya mtu binafsi na kutofautiana, lakini kujifungua katika mahusiano, kwa kubadilishana ambayo hutufanya tustahili na kuponya, kama katika kesi ya Petro, na ambayo safari mpya na Yesu inaanza. Kimsingi, Papa Fransisko anaandika kwamba ni lazima tujiweke kwa  upya katika miguu ya wanadamu, ambapo nafasi halisi ya kitaalimungu inaundwa. Kwa mtazamo huo ndipo  utakuwa chanzo cha furaha na ukuaji. Kwa sababu ni kutoka hapo o, kutoka chini, kwamba kila mmoja wetu anaweza kusoma tena uzuri wetu  na historia yetu. Papa amesisitiza juu ya mwaliko wa kutoogopa kutafuta huduma mpya na njia mpya za kutumia mamlaka kiinjili. Kwamba sio utafiti wa kinadharia na kiitikadi  kwasababu  itikadi hukataa Injili, lakini utafiti unaoanzia kwenye miguu ya wanadamu waliojeruhiwa na kutembea pamoja na dada na kaka waliojeruhiwa, kuanzia na dada zao wa kijumuiya wanazoishi watawa hao.

Papa amekutana na Umoja wa  Mama wakuu wa Mashirika ya kitawa
Papa amekutana na Umoja wa Mama wakuu wa Mashirika ya kitawa

Katika mchakato wa sinodi  ili kuwa wajenzi wa umoja, Papa Francvisko amewaleza kwamba wasiogipe udhaifu wao. Papa amerudia kuhimiza tena kwa Wakuu, wa watawa hao huku akiwaalika kushiriki kikamilifu katika mchakato wa sinodi hivyo kulitajirisha Kanisa kwa karama zao wenyewe, lakini zaidi ya yote kwa kuamsha kazi ya sinodi ndani ya maisha yao ya jumuiya. Kwa sababu hiyo alisisitiza tena katika hotuba yake aliyoitoa kwa watawa, njia ni kuwa wajenzi wa umoja, na wafumaji wa mahusiano. Hii ni fursa ya kusikilizana, kuhimizana kuzungumza kwa lugha moja kunia mamoja,  kuuliza maswali kuhusu mambo muhimu ya maisha ya kitawa  ya siku hizi. Pia kuruhusu maswali yasiyopendeza yatokee. Na kwa maana hiyo amehimiza sana wasiogope udhaifu wao, na wasiogope kuwasilisha yote  kwa Yesu. Papa Francikos amekazia pia udharura wa huduma ya usindikizaji, ambapo hata walei wanaweza kushiriki katika mambo ya kiroho yanayomwilishwa na Taasisi mbali mbali.  Papa amesema ishara nzuri ya upyaisho huo wa sinodi lazima iwe ya utunzaji wa pande zote. Papa Francisko amehimiza tena, akifikiria hasa mikutano midogo midogo au yale ambayo ina mapungufu hadi kufikia hatua ya uendelevu mgumu.  Papa amesema “Jambo muhimu  ni kuwa na uwezo wa kutoa majibu ya uaminifu na ubunifu kwa Bwan”, amehitimisha.

Papa amekutana na Umoja wa  Mama wakuu wa Mashirika ya kitawa
Papa amekutana na Umoja wa Mama wakuu wa Mashirika ya kitawa

Hata hivyo kabla ya mkutano huo  kwa mujibu wa Sr. Jolanta Kafka, ambaye ni  Rais wa UISG, alieleza kwamba:“kuna njia nyingi za kufanya sinodi ionekane: mkutano wetu, kwa mujibu wa maudhui na mbinu, ni uzoefu wa sinodi ndani ya maisha ya kitawa”. Kwa maana hiyo yeye binafsi alikuwa na matumaini ya kweli kuweza kuishi nafasi iliyobahatika ya kusikiliza, ya utafiti pamoja na Roho Mtakatifu. Kujadili jinsi wanavyochangia katika mchakato wa sinodi katika Kanisa, jinsi wanavyoweza kuhimiza usikilizaji wa kina katika mtindo wa sinodi na jinsi ya kuingia katika msukumo wa utambuzi wa jumuiya kama Kanisa, wakitambua udhaifu kama tabia ya kawaida ya kibinadamu. Tangu kuanza Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa mashirika  (UISG) umetoa  muafaka wa mahali pa kukutanika kwa Wakuu hao katika muktadha wa kikanisa. Wakiwa na washiriki kutoka ulimwenguni, lengo lao  ni kujenga madaraja na mitandao ili kuunda mikakati mipya na ushirikiano ambao unawaruhusu wanawake watawa kuwasiliana katika umbali wa kijiografia na tofauti wa lugha  na kiutamaduni, ili waweze kuwa katika umoja wao kwa wao na kwa pamoj. kujenga jumuiya ya kimataifa. Wanachama wake ni zaidi ya mama Wakuu Wakuu 1900, ambao mama wakuu wako katika nchi 97  ulimwenguni kote.

05 May 2022, 16:24