Papa Francisko alikutana na maaskofu wa Italia katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu
Jumatatu 23 Mei,alasiri umefunguliwa Mkutano Mkuu wa 76 wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI)kwa kukutana na Papa katika Ukumbi wa Paulo VI,jijini Vatican ambao utafungwa Ijumaa tarehe 27 Mei na ambao utapelekea uteuzi wa Rais mpya Baraza la Maaskofu Italia ambaye atathibitishwa na Papa Francisko.
Vatican News
Katika Ukumbi wa Paulo VI, mnamo tarehe 23 Mei 2022 alasiri, Baba Mtakatifu Francisko aliwakaribisha Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) katika Ukumbi wa Paulo VI jijini Vatican kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 76 unaofanyika huko Hilton karibu na Uwanja wa Ndege, Roma, kuanzia tarehe 23 -27 Mei 2022 kwa kuongozwa na juu mada: "Kusikiliza masimulizi ya Watu wa Mungu. Mang’amuzi ya kwanza: ni vipaumbele gani vinavyojitokeza katika Mchakato wa safari ya Sinodi?".
Mazungumzo yao , kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican yalidumu kama masaa mawili. na Uchaguzi wa rais wa CEI na mkutano wa waandishi wa habari mnamo 27 Mei 2022.
24 May 2022, 10:48