Tafuta

Papa Francisko kwa Enac:anga inakutana,anga ya amani hata kwa nchini Ukraine

Papa amekutana katika Ukumbi wa Paulo VI na mameneja na wafanyakazi wa Shirika la Kitaifa la Usafiri wa Anga, ambalo lina jukumu la udhibiti wote wa usalama wa anga.Amesisitiza kuwa usafiri wa anga umechangia maendeleo ya ulimwengu kwa njia ya kufanya watu wa mbali kujulikana kati yao wenyewe,kuvunja vikwazo vya kitaifa. Lakini pia inatumiwa kama chombo cha kifo,kupitia milipuko ya angani,kama vita vya kutisha,Ukraine.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa 13 Mei 2022 amekutana na wakuu  na wafanyakazi wa  Mamlaka ya Shirika la Kitaifa ya Usafiri wa Anga  (ENAC)na kumshukuru Rais wao kwa kufafanua lengo la Mamlaka  Shirika hiyo. Wao ni sehemu ya sekta ya usafiri wa anga yenye nyanja nyingi, ambayo inastahili kutiwa moyo na kuungwa mkono, kwani ni miongoni mwa walioathirika zaidi na janga la UVIKO.  Usafiri wa anga wa kiraia umechangia maendeleo ya ulimwengu wa kisasa, kuwaleta watu wa mbali karibu na kila mmoja na kuwafanya wajulikane. Unaweka taaluma na miundo katika huduma ya kampuni ili kuhakikisha usalama wa ndege na abiria, wakati wa shughuli za angani na ardhini kwenye uwanja wa ndege. Shughuli hii, pamoja na kuwa chombo madhubuti cha kudhibiti na kudhibiti safari za ndege, imechukua sifa za rasilimali ya kijamii yenye thamani.

Papa alikutana na Wakuu na wafanyakazi wa  Mamlaka ya Shirika la Kitaifa ya Usafiri wa Anga  (ENAC)
Papa alikutana na Wakuu na wafanyakazi wa Mamlaka ya Shirika la Kitaifa ya Usafiri wa Anga (ENAC)

Baba Mtakatifu Francisko amefafanua kwamba kiukweli, kwa kazi yao inatoa huduma ya lazima kwa taifa na kwa raia wake, ikichangia kwa kiasi kikubwa kuendeleza wito wao wa Ulaya na kimataifa. Maelfu ya abiria wanaweza kufikia miji na nchi nyingine, kwa kazi, kwa utalii, kwa mahitaji ya familia, na hivyo kuleta pamoja tamaduni na mila mbalimbali. Kwa njia hiyo, ujuzi, ushirikiano na kubadilishana maelewano katika nyanja za kiutamaduni, kiuchumi na kidini hukuzwa zaidi. Kazi yao ni muhimu sana kwa maendeleo ya mahusiano haya ya kibinadamu na kijamii katika ngazi ya kimataifa! Ukikabiliwa na kishawishi cha mara kwa mara cha kurudi kuweka vizuizi vya kitaifa, inadhihirika hata zaidi kwamba kazi yao iko kwenye huduma ya kukutana na udugu.

Baba Mtakatifu Francisko aidha amezungumzia juu ya wasi wasi wa tofauti kabisa na mtazamo wa matukio ambayo usafiri wa anga unatumika kama chombo cha kukera, uharibifu na kifo. Kwa bahati mbaya, tunaona hili pia katika vita hivi vya kutisha nchini Ukraine, vinavyoangaziwa kila siku na milipuko ya mabomu ya angani. Tukikabiliwa na hali hii ya kutisha, matumaini kwamba anga daima ni anga za amani pekee yanasukuma mioyo yetu kwa nguvu zaidi, kwamba tunaweza kuruka kwa amani ili kuunda na kuimarisha uhusiano wa kirafiki. Usafiri wa anga ni urafiki, unakutana!”

Papa alikutana na Wakuu na wafanyakazi wa  Mamlaka ya Shirika la Kitaifa ya Usafiri wa Anga  (ENAC)
Papa alikutana na Wakuu na wafanyakazi wa Mamlaka ya Shirika la Kitaifa ya Usafiri wa Anga (ENAC)

Baba Mtakatifu pia ni wasiwasi wao kutekeleza mipango ya kutosha ya kuzuia ajali mbaya kwenye vyombo vya usafiri. Katika suala hili, anatumai kuwa Siku ya Kitaifa “Si ya kusahau”, iliyoundwa kukumbuka waathirika wa ajali mbaya ya Linate huko Milano Italia, itakuwa fursa ya kukuza uelewa kati ya mashirika yanayopenda usafiri wa anga juu ya umuhimu wa abiria na thamani ya kila mtu binafsi. Papa amewahimiza kuendelea na uteuzi huu wa kila mwaka, na amewapongeza kwa sababu wanajua jinsi ya kuiishi pia katika mwelekeo wa kidini, ambao kwao unapata marejeo yake katika Nyumba Takatifu ya Loreto, Mlinzi wao, ambao wao hasa wanajitolea.

Mama Maria, ambaye watu wa Kikristo wanamwabudu kwa upendo wa pekee katika mwezi huu wa Mei, anatufundisha kutembea katika maisha na miguu yetu juu ya ardhi, kushiriki furaha na mateso ya wale wanaotuzunguka; na wakati huo huo, daima kuweka kuinua mtazamao wetu hadi kwenye upeo wa mbingu, huku mioyo yetu ikiwa wazi kwa Mungu na neema yake inayotuokoa. Papa Francisko amerudia  tena kwao na kwa wenzo wote  kushukuru kwa shughuli wanayoifanya, akifahamu vyema jinsi ilivyo nyeti na inayochosha, hasa kwa hali ya ujasiriamali ya makampuni mbalimbali ya ndege, pale inapobidi kupunguza wafanyakazi au kuingia ubia na kampuni zingine, kwa maana hiyo ameomba lazima wawalinde watu ambao wanaweza kuachwa bila kazi mara moja. Kazi ni utajiri.

Papa Francisko alikutana na wakuu na wafanyakazi wa Shirika la Anga
Papa Francisko alikutana na wakuu na wafanyakazi wa Shirika la Anga

Na kwa hili, wamewahimiza kufanya kazi kati yao kwa roho ya mshikamano, uaminifu na urafiki, ili kukuza uhusiano wa pande zote ambao unawasaidia kukabiliana na nyakati ngumu kwa ujasiri. Papa amewakabidhi wao na familia zao kwa maombezi ya kinamama ya Mama Yetu wa Loreto na kuwabariki sana. Lakini pia wasisahau kusali kwa ajili yake.

13 May 2022, 19:28