Tafuta

2022.05.16Wakuu wa Vyuo vikuu vya Mkoa wa Lazio. 2022.05.16Wakuu wa Vyuo vikuu vya Mkoa wa Lazio. 

Papa Francisko:Elimu ya chuo kikuu isiwe ya kiitikadi bali yenye thamani!

Katika Mkutano na wakuu wa vyuo vikuu vya Umma vya Roma na Lazio,Papa Francisko ametafakari juu ya mafunzo ya kitaaluma,ambayo yanayotoa mwaliko wa kuacha kulalamika urithi wa kipindi cha ‘enlightenment’,mwanga bali katika upeo mpana, unaotoa mafunzo ya thamani ya amani kwa vijana zaidi ya mzunguko wa kiitikadi.

Na Angella Rwezaula  - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wakuu wa Taasisi za Kipapa na za kiserikali za vyuo vikuu Roma na Mko wa Lazio, waliounganika katika Uratibu wa Mkoa wa Vyuo Vikuu vya Lazio na wawakilishi wa Mkoa. Amewasalimu,Rais wao, Profesa Stefano Ubertini, Gambera wa Chuo Kikuu cha Turscia na kumshukuru kwa maneno yake ya uwakilishi kwa niaba ya wote. Kwa vyuo vikuu katika wakati huu wa kipekee wa kihistoria, vimekabidhiwa kazi kubwa ya uwajibikaji. Miaka ya janga la virusi, kuingia barani Ulaya vita vya tatu vya kidunia ambavyo vimeanza kugawanyika vipande vipande, na sasa utafikiri hatakuwa na masuala ya mazingira ulimwenguni, ongezeko la ukosefu wa usawa, vimeleta changamoto kwa haraka. Changamoto ambayo ina matokeo makubwa ya kiutamaduni, kiakili na kimaadili. Katika tukio hili liko mbele ya kizazi cha vijana tishio la haki  ya kukatisha tamaa, na mahangaiko, ya kupoteza imani, mbaya zaidi kuliko kulewa.

Ukweli ni kwamba tuko kwenye shida:mgogoro inafanya kukua

Papa Francisko ameongeza kusema “Lazima tujiambie ukweli: tuko kwenye shida. Na mgogoro sio jambo baya, sio mbaya: mgogoro ni mzuri, kwa sababu mgogoro unatufanya kukua, hutufanya kufanya chaguzi za kukua. Hatari ni wakati mzozo unapogeuka kuwa mzozo: mzozo unafungwa na kuharibu. Lakini lazima tujifunze kuishi katika shida, kama za sasa, na kuwapeleka mbele vijana ambao wako katika vyuo vikuu huku tukiwafundisha kuishi katika shida na kushinda machafuko. Hii ni moja ya mambo mazuri ambayo yanaweza kufanywa: jinsi ya kuishi na mgogoro na kuondokana na mgogoro huo, ili usigeuke kuwa migogoro”.

Papa kiendelea amesema “Lakini vijana hawapo kwa dhati na amani: elimu ya chuo kikuu cha binadamu na ulimwengu, na juu uthabiti. Wakati mwingine, baadhi ya vyuo vikuu, amefikiria baadhi ya vile anavyo vijua  kwamba huendeleza urithi wa chuo kikuu cha enzi za ‘enlightenment’  yaani mwanga ambacho ni kujaza kichwa na mawazo, kujazwa na ubongo na hii haisaidii. Ni lazima mtu aelimishwe kwa lugha ya kichwa, moyo na mikono, na hivyo aweze kukua katika jamii”.

Kipindi cha kuwekeza katika elimu

Kwa maana hiyo wakuu hao wanaiwaita katika uwajibikaji. Na kwa maana hii ndio wakati  mkuu  wa kuwekeza katika elimu. Mkakati wa kielimu kimataifa kwa maana hiyo upo unaendelezwa ambao ni mpango wa kazi ya pamoja katika ngazi ya sayari ambao unahusisha watu wengi, dini kubwa za taasisi za kimataifa, taasisi binfsi za kielimu. Papa Francisko amesema kwa kutia saini katika roho hiyo hati juu ya Udugu wa Kibinadamu huko Abu Dhabu mnao tarehe 4 Februari 2019, walithbtishwa  juu ya mafunzo fungamani yalivyo moyoni ambamo yanajikita katika kujitambua binafasi ndugu, kazi ya uumbaji na Muumba. Kiukweli, kuna mengi ya kufanya, ili kuhakikisha maendeleo ya kiteknolojia na kisayansi, bila shaka, lakini pia kuhakikisha uendelevu wake wa kibinadamu. Mabadiliko makubwa yanatuhitaji kutafakari upya mifano yetu ya kiuchumi, kiutamaduni na kijamii, ili kurejesha thamani kuu ya utu. Na neno lenyewe chuo kikuu huteua jamii, lakini pia wazo la muunganisho wa maarifa, katika utaftaji ambao hutoa ukweli na maana kwa mazungumzo kati ya wanaume na wanawake wote ulimwenguni.

Chuo Kikuu kinaweza kutoa huduma muhimu sana

Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba huduma ambayo chuo kikuu kinaweza kutoa kwa hivyo nimuhimu sana; ambapo vyuo vikuu wanavyowakilisha, kila kimoja kikiwa na sifa zake, wanaweza kutoa ili kufikiria upya na kurekebisha miundo ya maendeleo, kuleta pamoja nguvu bora za kiakili na maadili. Wanafunzi hawaridhiki na ukiritimba  na kutumia lakini pia wao hawaridhiki na marudio ya takwimu, hata na mafunzo ya ufundi bila upeo. Hii inaoneshwa, kwa mfano na uhamasishaji mkubwa wa wanafunzi wengi vijana wa mafunzo ya kidaktari (PhD) na watafiti juu ya uchumi, unaoratibiwa na maprofesa wa Vyuo Vikuu vyako, kwa lengo la kujenga majibu mapya na yenye ufanisi, kushinda uandikishaji wa zamani unaohusishwa na utamaduni tasa wa ushindani wa nguvu. Baba Mtakatifu amewaomba wasikose kuwa na jitihada za kusikiliza wanafunzi wote kike na kiume, wenzao: wasikilize hali halisi ya kijamii na kitaasisi, wale wa karibu na walio mbali kwa sababu chuo kikuu hakina mipaka: fahamu, utafiti, mazungumzo, na makabiliano yanaweza kushinda kila aina ya mipaka na kuwa uwanja wote.  

Ujasiri wa kufikiria mbali na kuwekeza katika elimu

Papa amesisitiza wasikose kuwa na ujasiri wa kufikiria mbali na kuwekeza, kuwa na maendeleo ya kibinadamu ya kazi na ya kijamii; kuwaunda hata kwa heshima, hshima binafsi, heshima kwa jirani, heshima ya uumbaji mbele ya Muumba. Katika kuhamasisha mafunzo mahiri na utafiti amewashauri wawe makini kwa sababu wote ambao wanastahili na hawana uwezo, wanaweza kufanya zoezi kamili katika haki yao ya masomo na mafunzo. Na pia kwa kupelekea mbele sifa ya jitihada za kukarimu wanafunzi, watafiti, walimu waathirika wa mateso, vita, ubaguzi katika Nchi tofauti za Ulimwengu, wanaweza pia kutoa chachu kwa aina nyinyi za utoaji huduma, katika jumuiya ili kuwa kipimo cha umaskini na pembezoni mwa maisha na kijamii, na waweze kutoa maana na thamani katika mafunzo yao ya chuo kikuu, na kamwe wasitenganisha katika maisha na ya watu na ya kijamii.

Kwa kurudi katika lengo la Taasisi ya kielimu, katika jitihada za mtaala, utafiti, mazungumzo na kukabiliana na jamii, Baba Mtakatifu anatumaini kwamba jumuiya zao zitaweza kuishi, kuwa za wazi, hai, karimu na wawajibikaji katika hali ya ushirikiano wa kuzaa matunda, kubadilishana na mazungumzo, kuthamanisha wote na kila mmoja. Wanaweza kusoma na kukabailiana mabidiliko hayo ya kipindi kwa tafakari na mang’amuzi bila hukumu za kiitikadi, bila woga au kukimbia au mbaya zaidi mfananisho.  “Na juu ya hilo Papa amependekeza wawe makini kwa itikadi. Itikadi huharibu kwa sababu hutuonesha njia moja tu na kufunga mtazamo wa ulimwengu wote. Itikadi huharibu ubinadamu wa mtu, huondoa moyo wake, huondoa uwezo wake wa ushairi, na ubunifu. Leo kuna mengi: lazima tuwe waangalifu tusije tukaingia katika mitazamo hii ya kiitikadi inayoharibu, na kuleta madhara mengi. Hata Kanisani tuna itikadi nyingi, wakati fulani, ambazo hazifanyi vizuri”.

Maandalizi ya Jubilei 2025

Baba Mtakatifu amekumbusha kwamba “Imesalia miaka michache tu kufikia Jubilei ya 2025. Tunakumbuka kwamba miaka mitatu tu baada ya maadhimisho ya Jubilei ya kwanza ya 1300 ‘Studium Urbis’ ilianzishwa, kana kwamba kuonesha kwa vitendo na kuthibitisha uhusiano wa asili kati ya Kanisa na taasisi ya chuo kikuu, mojawapo ya maneno ya kale zaidi na ya kushangaza zaidi ya ustaarabu wa Ulaya, ambayo baadaye ilikua na kuenea duniani. Uhusiano huo wa kale na ulioimarishwa, katika tofauti na ushirikiano, Papa amesisitiza kwamba wanaitwa wote  kuendeleza na kufikia katika ujenzi unaowajibika na endelevu wa njia za maendeleo. Kauli mbiu ya Jubilei ya 2025 “Mhujaji wa Matumaini iweze kwa namna hiyo kufafanua jitihada zao ule umakini wa kujieleza mtazamo shirikishi wa maisha, wa wema na wa udugu. Na ndiyo matashi ya Baba Mtakatifu kwao na shukurani kwa Kamati hiyo ya Uratibu Vyuo Vikuu vya  Mkoa wa Lazio. Amewasindikiza kwa baraka na kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake. Na ikiwa mmoja hasa kwa sababu hawezi na hata hajuhi au hajisikii basi amtakie mema kwa sababu anahitaji.

HOTUBA YA PAPA KWA WAKUU WA VYUO VIKOO LAZIO,ITALIA
16 May 2022, 16:38