Papa atangaza majina 21 ya Makardinali wapya
Na Angella. Rwezaula - Vatican.
Papa Francisko Dominika tarehe tarehe 29 Mei 2022, mara baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu amewatangazia waamini na mahujaji wote waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro majina ya Makardinali wapya wateule kutoka mabara tofauti ambao watasimikwa rasmi katika kikao cha Baraza la Makardinali mnamo Jumamosi tarehe 27 Agosti, ambapo tarehe 29 -30 Agosti watakuwa na Mkutano wa Makardinali wote ili kutafakari Katiba ya Kitume Praedicate evangelium. Papa Francisko akiendelea ametaja Majina ya Makardinali wateule:
Askofu Mkuu Arthur Roche -Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa.
Askofu Mkuu Lazzaro You Heung sik – Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makleri.
Akofu Mkuu Fernando Vérgez Alzaga L.C. – Rais wa Tume ya Kipapa ya Mji wa Vatican na Rais wa Utawala wa Serikali ya Mji wa Vatican.
Askofu Mkuu Jean-Marc Aveline - Jimbo Kuu Katoliki la Marseille (Ufaransa),
Askofu Peter Okpaleke - Jimbo katoliki la Ekwulobia (Nigeria).
Askofu Mkuu Leonardo Ulrich Steiner, O.F.M. - Jimbo Kuu Katoliki la Manaus (Brazil).
Askofu Mkuu Filipe Neri António Sebastião di Rosário Ferrão - Jimbo Kuu Katoliki la Goa na Damão (India).
Askofu Robert Walter McElroy – Jimbo katoliki la Mtakatifu Diego (U.S.A).
Askofu Mkuu Virgilio Do Carmo Da Silva, S.D.B. – Jimbo Kuu Katoliki la Dili (Timor Mashariki).
Askofu Oscar Cantoni - Jimbo Katoliki la Como (Italia).
Askofu Mkuu Anthony Poola - Jimbo Kuu Katoliki la Hyderabad (India).
Askofu Mkuu Paulo Cezar Costa - Jimbo Kuu Katoliki la Brasília (Brazil).
Askofu Richard Kuuia Baawobr M. Afr - Jimbo Katoliki la Wa (Ghana).
Askofu Mkuu William Goh Seng Chye - Jimbo Kuu katoliki la Singapore (Singapore).
Askofu Mkuu Adalberto Martínez Flores - Jimbo Kuu katoliki la Asunción (Paraguay).
Askofu Mkuu Giorgio Marengo, I.M.C. – Balozi wa Kitume wa Ulaanbaatar (Mongolia).
Pamoja na hao, wataungana na wajumbe wa Baraza la Makardinali wafuatao:
Askofu Mkuu Mstaafu Jorge Enrique Jiménez Carvajal - Jimbo Kuu Katoliki la Cartagena (Colombia).
Askofu Mkuu mstaafu Lucas Van Looy sdb - Jimbo Kuu Katoliki la Gent (Ubelgiji).
Askofu Mkuu Mstaafu Arrigo Miglio - Jimbo Kuu katoliki i Cagliari (Italia).
R.P. Gianfranco Ghirlanda sj, – Profesa wa Taalimungu.
Monsinyo Fortunato Frezza – Mwanasheria ya Kanisa wa Mtakatifu Petro.
Baba Mtakatifu amehitimishwa kwa kuwatakia Dominika Njema na kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.