Wito wa Papa kwa viongozi wa Sri Lanka ili kulinda na kuheshimu haki za raia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu ametoa wazo maalum kwa ajili ya watu wa Sri Lanka kwa namna ya pekee vijana ambao siku hizi wamesikika kilio chao mbele ya changamoto na matatizo ya kijamii na kiuchumi ya Nchi. Kwa maana hiyo anaungana na mamlaka ya kidini katika Nchi hiyo wakati wa kuhitimisha Katekesi yake kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro jijini Vatican tarehe 11 Mei 2022 kuwaomba mamlaka kufanya hivyo.
Papa metoa wito kwa sehemu zote zenye vikwazo ili kutunza tabia ya amani bila kuangukia katika vurugu. Kwa wote wenye mamlaka na majukumu kwa raia wasikilize shauku za watu kwa kuwahakikisha heshima ya haki za kibinadamu na uhuru wa kiraia.
Papa Francisko hakusahaku kumbuka na kukabidhi shauku, mawazo, mahangaiko ya Amani kwa Bikira Maria ambaye takumbukwa huko Fatima mnamo tarehe 13 Mei. Amekumbusha hayo wakati akiwasalimia waamini na mahujaji wa lugha ya kireno ambapo wazi ni kwa wote ambao siku hizi wanatembee kuelekea katika Madhabahu ya Bikira Maria wa Fatima wakipeleka kwa Mama furaha na wale wote ambao wanahangaika katika mioyo yao.
“Pamoja na kaka na dada hao hata sisi tukabidhi shauku za kweli za amani katika ulimwengu kwa Bikira Maria ili aweze kuwatazama wote kwa mtazamo wa kimama.”
Na katika salamu kwa wanaozungumza kijerumani, Papa amewaalika wasali Rosari kwa ajili ya amani ulimwenguni na ndiyo wito wake ambao unaweza kuleta ukaribu katika furaha na shida za wakati wetu. Katika kuwasalimia waamini wa Poland, Papa anakumbuka kwamba siku ya Jumatatu waliadhimisha “sherehe ya Mtakatifu Stanislaus, askofu na mfiadini mlinzi wa nchi yao”. Mtetezi huyu shupavu wa utaratibu wa kimaadili wa kimungu, hasa katika juma hili la kuombea miito, awapatie vijana wote karama ya utambuzi wa hekima wa njia ya uzima, ya kumkabidhi Kristo na uaminifu kwa tunu za Kiinjili.
Kwa upande wa lugha ya kiitaliano Papa Francisko halikusahulika wazo kwa ajili ya wazee , wagonjwa, vijana na wenye ndoa wapya. Mwezi huu kwa namna ya pekee kwa Mama Maria , amewaalika kufuata mfano wa Maria kwa kuamini maombezi ya umama wake.