Tafuta

2022.05.06 Ugonjwa wa  Fibromyalgia, shughuli ya kichungaji Jimbo la Roma 2022.05.06 Ugonjwa wa Fibromyalgia, shughuli ya kichungaji Jimbo la Roma 

Papa amewaombea wagonjwa wa Fibromyalgia ili wapate msaada

Mara baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu Papa amezungumza kwa takriban ya watu milioni mbili na nusu nchini Italia wanaosumbuliwa na Fibromyalgia,ugonjwa unaoathiri mfumo wa misuli na mifupa.Siku ya Fibromyalgia Duniani,huadhimishwa kila Mei 12,kwa lengo kujifunza kuhusiana nayo.Ni ugonjwa usiojulikana na usio na tiba.Kati ya 5 na 8% ya wanawake umri 30 hadi 40 wanaumwa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mawazo ya Papa Francisko yameelekezwa kwa wagonjwa Fibromyalgia wakati salamu za baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu wa kwa takriban ya watu milioni mbili na nusu nchini Italia wanaosumbuliwa na gonjwa ili waweze kupata msaada unaohitajika. Sababu halisi za fibromyalgia hazijulikani, uchunguzi unafanywa kwa kutenga (patholojia)asili nyingine, na hakuna tiba halisi, wala hatua za kuzuia. Kwa maana hiyo ni takriban watu milioni mbili na nusu nchini Italia wanaokabiliwa na ugonjwa huu ambao una sifa ya kuenea na maumivu ya mara kwa mara ya misuli na mifupa yanayohusiana na uchovu wa kudumu, ukakamavu, maumivu ya kichwa, usingizi, kupoteza kumbukumbu na mabadiliko ya hisia. Hawa wanajitambulisha kama “wagonjwa wasioonekana” kwa sababu ishara za ugonjwa huo hazitambuliki mara moja na wengine, lakini juu ya yote kwa sababu fibromyalgia nchini Italia bado haijatambuliwa na mfumo wa afya wa kitaifa, wakati unatambuliwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Siku ya kimataifa ya ugonjwa wa Fibromyalgia kila 12 Mei
Siku ya kimataifa ya ugonjwa wa Fibromyalgia kila 12 Mei

Lakini kuna jambo jipya ambalo linaashiria vyema: sheria ya hivi karibuni ya bajeti iliyopitishwa na serikali mwishoni mwa Desemba, imeanzisha mfuko wa utafiti, uchunguzi na matibabu ya fibromyalgia, na bajeti ya euro milioni 5 kwa mwaka wa 2022. Mafanikio ambayo ni matokeo ya kujitolea kwa wengi, vyama na madaktari, ambao hufanya kazi kila siku kwa ajili ya wagonjwa hawa. Walio mstari wa mbele ni Kanisa linalohimizwa na Papa Francisko ambaye tayari katika mkesha wa Siku ya Fibromyalgia Duniani 2021, Wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu kwa hakika alivuta hisia za taasisi na jumuiya. “Ninaelezea ukaribu wangu na ninatumaini kuwa na umakini kwa ugonjwa huu ambao hautazingatiwi wakati mwingine utaongezeka, alisema katika tukio hilo, wakati wa kulazwa hospitalini katika Hospitali ya Gemelli  na kwa kusisitiza alisema  “hakuna seti ya magonjwa A na seti ya Magonjwa B.

Siku ya kimataifa ya ugonjwa wa Fibromyalgia kila 12 Mei
Siku ya kimataifa ya ugonjwa wa Fibromyalgia kila 12 Mei

Jimbo la Roma, kupitia Ofisi ya Huduma ya Kichungaji ya Afya, inayoongozwa na Askofu Paolo Ricciardi, inawakilisha kinara katika umakini wa Fibromyalgia: kwa miaka kadhaa kumekuwa na eneo linalohusika na magonjwa ya mifupa na misuli (rheumatic) ambayo ni pamoja na aina hii ya watu ambao inawasikiliza na msaada kupitia meza maalum, ukurasa wa Facebook na kikundi cha watu binafsi, pia kuhamasisha shughuli za uhamasishaji juu ya ugonjwa huo katika parokia na vituo vya afya. Mkuu wa kitengo hicho ni Edith Aldama, muuguzi kitaaluma, ambaye binafsi anapitia hali ya Fibromyalgia. Akizungumza na maikrofoni za Radio Vatican ameelezea kazi yake na shughuli anazoratibu kwa ujumla eneo lote.

Eneo hili lilizaliwa kutokana na uzoefu wa mateso, magonjwa, na tulichotaka kuwapa watu hawa ni kukumbatiwa na Kanisa, kwa hiyo tumefungua kituo cha kusikiliza ambapo wagonjwa wanapokelewa kiukweli, kusikilizwa na watu wa kujitolea. Ni wagonjwa wa kujitolea, na ni muhimu kuelewa kwamba hatuwezi kukabiliana na ugonjwa peke yetu. Watu wengi wanahisi kutoeleweka nyumbani kwa sababu huu ni ugonjwa ambao dalili zake hazionekani. Unaweza kuona mtu mgonjwa na inaonekana kwake kwamba hana chochote, badala yake mtu huyo anateseka, hivyo wakati mwingine wagonjwa hawaeleweki nyumbani na katika jamii. Watu wengi hawawezi tena kufanya kazi walizokuwa wanafanya hapo awali, kwa hivyo kuachishwa kazi huanza, mizozo ya ndoa huchukua nafasi ndani ya familia. Tumekuwa na wagonjwa ambao wanatuambia historia zao wenyewe za maisha magumu kwa sababu maumivu ya muda mrefu hayahusishi mgonjwa tu, yanahusisha familia nzima.

Kile tunachofanya katika Kituo hiki pia ni kujaribu kuwa daraja: tumeshirikisha hospitali mbalimbali katika ngazi ya mkoa wa Lazio, kuanzia Gemelli ambapo katika kitengo cha  misuli na mifupa (rheumatology) kuna huduma kwa wagonjwa hawa na hivyo pia katika hospitali ya Mtakatifu Yohane wa Mateso  ambao anatuunga mkono kwa ufunguzi wa kliniki ili wagonjwa wapate msaada wa bure na kuepuka unyonyaji na dhuluma kwa ugonjwa huo. Bado haijatambulika, kwa bahati mbaya wagonjwa wengi hujikuta wakikimbilia kwenye hospitali binafsi, hivyo tunataka kuleta maono hayo ambayo Baba Mtakatifu anatufundisha na ndiyo umuhimu wa huduma za bure.

Aidha ametoa neno kumpongeza Baba Mtakatifu kwamba “tunamshukuru sana Papa kwa sababu ametupa matumaini. Maneno yake pia yamesongesha kitu katika ngazi ya taasisi, ya jamii, kwa mabadiliko. Alitoa msukumo mkubwa kwa kuzitaka taasisi hizo kuangalia ugonjwa uliosahaulika, hivyo maneno yake yalikuwa ni ishara kubwa ya ukaribu, yalikuwa ni kubembeleza kwetu. Kwa maana hiyo Siku ya Fibromyalgia Duniani huadhimishwa kila tarehe 12 Mei “kwa lengo la kuleta ufahamu na ujuzi wa ugonjwa huu na kile tunachojaribu kutoa ni mtazamo tofauti kwa heshima yake. Tunachotaka ni kufikia mioyo ya taasisi ili ugonjwa huu uingizwe katika viwango muhimu vya usaidizi, ili wagonjwa hawa wapate haki ya matibabu. Kwa hiyo siku hii ilizaliwa ili kuwapa watu hawa wote utu wao wenyewe.”

08 May 2022, 16:52