Papa atoa matashi mema kwa mama wote ulimwenguni na wale waliotangulia mbele
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa ajili ya Mama wote ulimwenguni, lakini pia hata mkasa uliotokea huko wa mlipuko ni mawazo ya Papa Francisko mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu, Dominika tarehe 8 Mei 2022 kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican. Baba Mtakatifu kabla ya hapo alikumbusha kutangazwa kwa Mwenyeheri mpya, Jumamosi tarehe 7 Mei 2022 huko Mtakatifu Ramòn, nchini Peru kwa mfiadini María Agostina Rivas López, aliyejulikana kama Aguchita, ambaye alikuwa ni mtawa wa Shirika la Mama Yetu wa Upendo wa Mchungaji Mwema, aliyeuawa kwa sababu ya chuki ya imani yake mnamo 1990.
Baba Mtakatifu Francisko amemfafanua kama, Shujaa, mmisionari pamoja na kutambua hatari ya maisha yake daima alibaki karibu na maskini, hasa wanawake asilia na wazalendo, kwa kushuhudia Injili ya haki na ya amani. Mfano wake uweze kutoa shauku ya kuhudumia kwa wote Kristo kwa imani na ujasiri. Papa kutokana na hilo ameomba kupiga makofi, kwa ajili ya mwenyeheri mpya.
Baba Mtakatifu Francisko baadaye amezungumzia kuhusu Siku ya 59 ya Maombi kwa ajili ya Miito, mwaka 2022 inayoongozwa na kauli mbiu: “Kuitwa kwa ajili ya kujenga familia ya binadamu. Papa amesema siku ambayo kila bara, jumuiya za kikristo zimwomba Bwana zawadi ya miito ya kikuhani, ya maisha ya kitawa, uchaguzi wa umisonari na maisha ya ndoa ambapo waamini wote wanapaswa kuhisi wabatizwa na ambao wanaitwa kufuata Yesu, kuitikia ndiyo na kumfuata ili kugundua furaha ya kutoa maisha, ya kuhudumia kwa furaha na shauku ya Injili.
Baba Mtakatifu amewaombea hata waathirika wa mlipuko wa moto siku za hivi karibuni katika Hoteli moja ya kihistoria ya Saratoga, katika mji mkuu Havana huko Cuba, ambapo watu 27 wamekufa na zaidi ya 80 kujeruhiwa. Papa amesema Kristo mfufuka awaongoze katika nyumba ya Baba na kuwapa nguvu familia zao.
Katika hitimisho la salamu zake Papa amekumbuka hata waamini na mahujaji wote waliokuwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro katika siku kuu ya Mama na kusema kwamba: “Tunawakumbuka kwa upendo mama zetu hata wale ambao hawapo tena nasi, lakini wanaishi ndani ya mioyo yetu. Kwa ajili ya Mama zetu ni sala zetu, upendo wetu na matashi yetu mema kwao”.