Papa kwa Kikosi cha Walinzi wa Uswiss:ushuhuda,mazungumzo&kuishi kidugu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kabla ya kula kiapo cha kikosi cha Walinzi wapya wa kipapa 36, Papa Francisko, Ijumaa tarehe 6 Mei 2022 amekutana na kikosi cha Walinzi wa Kipapa, ambapo amesema siku kuu yao ya kila mwaka na kiapo cha walinzi wapya kwa kawaida ni fursa nzuri kwa ajili ya kukutana na kuwakaribisha wazazi na familia ambao wanaungana nao katika wakati huo wa maana. Baba Mtakatifu amewakaribisha wote na kumshukuru Kanali Christoph Graf, na kamanda mkuu mpya amemkaribisha, Msimamizi wa Kikanisa chao, Maafisa na wasaidizi wao na kundi zima. Wazo kwa namna ya pekee kwa wanajeshi wapya ambao Papa amesema kwa kula kiapo watawekwa katika familia kubwa ya Walinzi wa Uswiss. Kwa kufanya hivyo wanakuwa tayari kujikita katika shughuli mahiri katika maisha yao na wakati huo huo yenye utajiri wa uwajibikaji katika moyo wa Kanisa la ulimwengu.
Historia ya Kikosi cha ulinzi wa Kipapa kutoka Uswiss
Baba Mtakatifu Francisko amesema katika maeneo hayo wao wataitwa kujikita katika huduma yao ambayo imejaa historia muhimu ya kishujaa kwa wahudumu wengi wa Makao Makuu ya Kitume, miongoni mwao wapo hata wa Kiswiss. Tangu kuanzishwa kwa Kikkosi cha Walinzi wa Uswiss, vijana wengi wametimiza shugHuli ya kipee ambayo hata leo hii bado inaendelea. Kwa jitihada ya ukarimu na amInifu, katika Mchakato wa karne, baadhi hawakukosa kukutana na majaribu magumu, hata kufikia kumwaga damu yao kwa ajili ya kumlinda Papa na ili kumwezesha atimizwa utume wake kikamilifu kwa kujitegemea. Kutokana na kujitoa kwao, walitimiza kile ambacho kinachoendelezwa kwa kanuni hadi sasa, kuhusu usalama wa Papa na makao yake.
Kuishi pamoja kidugu na kusali
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kuwageukia walinzi hao wapya wa kiswiss amesema wao wamechagua kujikita katika utume wa kipekee wa kikanisa; amewashauri waishi kama mashuhuda wa kikristo na kijumuiya. Shughuli yao kwa kawaida haitendeki kibinafsi bali kama jumuiya; na ndiyo maana wanaitwa “Muhimili wa Walinzi wa Kiswiss. Kwa maana hiyo wanaweza kutumiza ukuu huo wa kijumuiya kila siku, iwe kwa masaa na masaa, ambayo wakati mwingine sio rahisi katika huduma na iwe katika maisha yao ya kila siku binafsi katika kambi na ambayo yanatazama kuwa na muda wao binafsi na wa kuishi kwa pamoja katika kukutana na kusali. Kuishi katika huduma kwa hali ya jumuiya pia ni changamoto, kwa sababu inahusisha kuunganisha watu binafsi wenye haiba, tabia na hisia tofauti, lakini ambao wanajikuta wakitembea pamoja kwenye kipande cha barabara. Licha ya hayo, wazo la kuhudumia Kanisa, katika kiti cha Mfuasi wa Petro, inawakilisha nguvu ambayo inahusisha na kusaidia kukabiliana na vipindi vya shida ambazo haziwezi kuzuilika.
Maisha ya kiroho na kugundua mpango wa Mungu
Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo waweze kutoa daima umuhimu wa mafunzo stahiki. Juhudi za kujikita huko kwao ni muhimu ili kupata umahiri wa kutosha wa kitaaluma na kufaa. Lakini kabla ya yote kukaa jijini Roma kunapaswa kuthamanishwe kwa ajili ya kukua kama Wakristo. Papa amekumbuka maisha ya kiroho ambayo yanaruhusu kukugundua mpango wa Mungu kwa kila mmoja. Na wakati huo huo amewashauri wakuze uhusiano wa pamoja, uwe wa kutimiza majukumu yao wanayokabidhiwa pia hata na ule wakati wakiwa huru, kwa sababu uweze kuwa mtindo wa ndugu ambao wanakiri kuwa Wakristo. Mazungumzo ya wazi na kidugu wakati mwingine yanaweza kuwa magumu, na kazi lakini ni muhimu kwa ajili yao binafsi.
Kukumbuka kijana mwenzao Silvan Wolf
Baba Mtakatifu Francisko ametumia fursa hiyo kuwashukuru, Muhimili wote wa Walinzi wa Kipapa wa Uswiss kwa ajili ya shughuli yao na ushirikiano msingi wa kila siku, ambao wao ni mashuhuda wa moja kwa moja. Vatican inawategeme wao. Mji wa Vatican unajivunia uwepo wao katika eneo lake! Papa amependa kutumia mda mfupi wa uchungu na huzuni.Kwa sababu ya kumkumbuka mwenzao Silvan Wolf. Kwa bahati mbaya alikufa, huyo kijana mwenye furaha. Ajali ilimwondoka. Kwa ukimya Papa amependa akumbukwe na kusali kwa ajili ya kijana Silvan.... Amewakabidhi wao, familia zao, marafiki zao na wale wote ambao katika fursa hii ya kuweka kiapo wamekuja Roma, kwa maombezi ya Bikira Maria Mama wa Mungu, na kwa maombezi ya Wasimamizi wenza,Mtakatifu Martino na Mtakatifu Sebastiani, na Mlinzi msimamizi wa Shirikisho la Uswiss, Mtakatifu Nicola wa Flüe, Papa amewabariki kwa Baraka yake. Na amewaomba wasisahau kusali pia kwa ajili yake.