Tafuta

2022-05-31  Papa Francisko akiwa anasala Rosari mbele ya Sanamu ya Bikira Maria wa amani katika siku ambayo inahitimishwa mwezi wa Maria. 2022-05-31 Papa Francisko akiwa anasala Rosari mbele ya Sanamu ya Bikira Maria wa amani katika siku ambayo inahitimishwa mwezi wa Maria.  

Papa Francisko:hatima ya ulimwengu inaweza kubadilishwa na sala

Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu,Papa anaongoza sala ya Rozari kwa ajili ya Amani,ikiwa ni hitimisho la mwezi wa Bikira Maria.sala hiyo imefuatiliwa na madhabahu mengine duniani kukiwa na ushiriki mkubwa wa waamini wa Ukraine.Ombi kwa Bikira:hupatanisho wa mioyo iliyojaa jeuri na kisasi.Anyoshe mawazo yaliyopofushwa na hamu ya utajiri rahisi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ameanza na sala wakati wa kuanza sala ya “Rozari ya Amani” katka Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Roma, Jumanne jioni tarehe 31 Mei 2022,  saa 12.00 . Papa Francisko ameomba: "Siku ya leo ambayo  inahitimisha mwisho  wa mwezi uliowekwa kwa ajili yako tuko tena mbele yako, Malkia wa Amani, kukusihi: Utujalie zawadi kubwa ya amani, usitishe mapema vita ambavyo vimekuwa vikiendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi, na duniani kwa miongo kadhaa sasa, na ambayo sasa pia imevamia bara la Ulaya".

Papa akiomba kwa Mama Malkia wa Amani.
Papa akiomba kwa Mama Malkia wa Amani.

Katika siku ya sikukuu ya kiliturujia ya Bikira Maria Kumtembelea Elizabeth, waamini, familia na jumuiya nyingi zimekusanyika katika Kanisa kuu la Kiroma kwa mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko ambaye, mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu, Dominika tarehe 29 Mei, aliomba kwa kauli moja wito wa amani na kuungana naye siku hii. Mwito wa Papa Francisko unakusudia kuwa ishara ya matumaini kwa ulimwengu, unaoteseka kutokana na mzozo wa Ukraine, na kujeruhiwa sana na vurugu za kambi nyingi za vita ambazo bado zinaendelea, katika ufahamu kwamba "amani haiwezekani  bila kuwa na matokeo ya mazungumzo na wala matokeo ya makubaliano ya kisiasa  lakini ni zawadi ya Pasaka ya Roho Mtakatifu".

Papa akiomba kwa Mama Malkia wa Amani.
Papa akiomba kwa Mama Malkia wa Amani.

Papa Francisko ameanza kusali mara tu baada ya kuweka maua ya mawaridi na orchids chini ya sanamu ya zamani sana ya Bikira iliyowekwa kwa makusudi  mnamo 1918 na Papa Benedikto XV, akiomba kuisha kwa Vita vya Kwanza vya Dunia. Hapo kiutamaduni, waamini wengi na mahujaji huweka kadi zao ndogo zilizoandikwa kwa mkono na nia zao za maombi, na kwa maana hiyo Papa Francisko amesoma  hata maombi yake. Hata hivyo Papa amekumbuka maombi yaliyotolewa kwa Mama Yetu wakati wa janga la UVIKO ili  kuunga mkono wagonjwa na kuwapa nguvu wafanyakazi wa matibabu, kuomba huruma kwa wanaokufa, kuwafuta machozi wale walioteseka kwa ukimya na upweke. Papa pia ametaja tendo la  kuwekwa wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria, mnamo  tarehe 25 Machi, kwa mataifa yaliyo katika vita na ombi la zawadi kuu ya uongofu wa mioyo.

Papa Francisko katika sala ya Rosari kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Roma

Papa Francisko amesema:“Tuna hakika kwamba kwa silaha za maombi, kufunga, kutoa sadaka, na kwa zawadi ya neema yako, mioyo ya wanadamu na hatima ya ulimwengu wote inaweza kubadilishwa. Leo tunainua mioyo yetu kwako, Malkia wa Amani: utuombee kwa Mwanao, upatanishe mioyo iliyojaa jeuri na kisasi, nyoosha mawazo yaliyopofushwa na tamaa ya utajiri rahisi, amani yako itawale milele juu ya dunia nzima”. 

Papa akiomba kwa Mama Malkia wa Amani.
Papa akiomba kwa Mama Malkia wa Amani.

Pamoja na Papa, mbele ya sanamu ya Maria Malkia wa Amani katika ukanda wa kushoto wa Kanisa Kuu, kulikuwa na vijana wavulana na wasichana ambao wamepokea Komunyo ya Kwanza na Kipaimara katika wiki za hivi karibuni, Skauti, familia za jumuiya ya Kiukreine zilizoko Roma, wajumbe Vijana Ardente wa Maria (GAM), Wajumbe wa Kikosi cha ulinzi wa  Vatican na Walinzi wa Kipapa wa Uswisi, parokia tatu za Roma zilizowekwa wakfu kwa Bikira Maria Malkia wa Amani, na baadhi ya washiriki wa Curia Romana.

Papa akiomba kwa Mama Malkia wa Amani.
Papa akiomba kwa Mama Malkia wa Amani.

Sala hiyo ilikuwa imeunganishwa na utiririshaji, wa sala ya pamoja kutoka  mabara yote matano, kulikuwa na Madhabahu ya Mama wa Mungu ya Zarvanytsia, huko Ukraine, Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Wokovu huko Iraq,  Siria, Ukraine, Bahrain na tena na madhabahu ya kimataifa ya Mama Yetu wa Amani na Yesu Mwokozi; Madhabahu ya Jasna Góra, Poland; Madhabahu ya Kimataifa ya Mashahidi, Korea; Nyumba Takatifu ya Loreto, Italia; Bikira Mwenyeheri wa Rozari Takatifu, Pompei; Madhabahu ya Kimataifa ya Mama yetu wa Knock Ireland; Mama yetu wa Guadalupe; Mama yetu wa Lourdes.

Waamini wa Ukraine wakisali Rosari na Papa katika Kansa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu
Waamini wa Ukraine wakisali Rosari na Papa katika Kansa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu

Tafakati Matendo ya Uchungu yalitangulia kusali Rosari kwa kumkabidhi Mungu, kwa njia ya maombezi ya  Malkia wa Amani, kwa ajili ya wanadamu wote waliojaribiwa vikali na vita na migogoro ya silaha. Maria, ambaye alimtembelea Elizabeth, anaoneshwa kama mwanamke mmisionari katika kuleta na kushiriki furaha ya kutangaza na mwanamke wa upendo katika kujiwekakwenye huduma ya walio hatarini zaidi. Baadaye waliongoza makumi ya Salamu Maria, kwa kubadilishana na familia ya Kiukreni, inayowakilisha familia zote zinazopata vurugu na unyanyasaji wa vita, makasisi wa kijeshi, kwa wale wanaotoa matumaini na faraja kwa watu walioathirika; mtu wa ike na kiume wa  kujitolea, kwa wale wanaoendelea kutekeleza utumishi wao wa thamani kwa ajili ya wengine hata katika hali ya hatari kubwa; familia ya Siria na Venezuela, kwa wale wanaoteseka isivyo haki kutokana na migogoro; baadhi ya wakimbizi, kwa ajili ya watu, wamelazimika kuacha nyumba zao na, kukaribishwa katika nchi nyingine, kujaribu kujenga upya maisha yao.

Waamini wa Ukraine wakisali Rosari na Papa katika Kansa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu
Waamini wa Ukraine wakisali Rosari na Papa katika Kansa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu

Katika tendo la kwanza “Yesu katika bustani ya mizeituni; kutoka moyoni mwa Roma, sala imeinuliwa kwa ajili ya waathirika wa vita, hasa kwa watu wasio na ulinzi: watoto, wazee, wagonjwa, na tena kwa familia zilizoraruliwa; kwa baba na mama ambao wanangojea kurudi kwa watoto wao na kwa watoto wanaongojea kurudi kwa baba na mama kutoka katika uwanja wa vita, ili  pasiwepo mtu yeyote anayepaswa kuteseka isivyo haki ”. Tendo la Pili “Yesu anapigwa mijeledi na askari” imewekwa kuombea makuhani, kwa watawa kati ya watu walioathiriwa na vita, ili wawe vyombo vya hruma  siku zote.

Waamini wa wakisali Rosari na Papa katika Kansa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu
Waamini wa wakisali Rosari na Papa katika Kansa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu

Tendo la tatu, Yesu amevikwa taji ya miiba. Maombi kwa wafanyakazi wa matibabu na watu wa kujitolea ambao kila siku wanatoa  msaada wa kibinadamu kwa wahitaji zaidi, ili waweze kusadikishwa zaidi na zaidi na wengi, na kwa familia na watu wote ambao wamepokea wakimbizi kwenye nyumba zao kwa uwazi na kwa  moyo, ili wasichoke kuonesha ukarimu na mshikamano ”. Tendo la Nne  Yesu anabeba msalaba. katika hili wapenda kuwakumbuka walioteswa na kufa, hasa wale wanaokufa katika upweke, ili wabakie kushikamana na imani, tena watu waliobakwa na kutoweka na familia zao na marafiki zao ili wasipoteze matumaini. Hatimaye, katika tendo la Tano:  Yesu anasulubishwa na kufa msalabani, ambapo wametoa  mwaliko wa kusali kwamba kwa kifo cha ukombozi cha Yesu Kristo, aliyeupatanisha ulimwengu na Baba, vita vikome na amani ya kudumu itawale katika mataifa yote.

Papa Mbele ya Picha ya Salus Populi Romani
Papa Mbele ya Picha ya Salus Populi Romani

Rozari ya Amani imehitimishwa  na litania ya Loreto, na baadaye  Papa akawabariki waamini kwa baraka zake na wimbo wa Maria umeimbwa. Kabla ya kuondoka kwenye Kanisa Kuu la Maria Mkuu  Papa, Francisko hakuacha kwenda kusali mbele ya  Paicha ya  Salus Populi Romani yaani Afya ya Watu wa Roma na baadaye akarudi kwa waamini na kuacha kusalimiana na baadhi,  huku akitoa tabasamu na ishara za upendo akiwa amekaa katika kiti cha magurudumu.

Maombi ya Papa wakati wa hitimisho la mwezi wa Maria
31 May 2022, 19:52