Tafuta

Papa:Tuweke uongo wetu mbele ya mwanga wa Yesu Mfufuka!

Hofu daima inatufunga sisi wenyewe.Yesu kinyume chake anatufanya kuondokana na hofu hizo na kututuma kwenda kwa wengine.Na ndiyo dawa”. Usiseme sina uwezo kwani wale wanawake hawakuwa kwa hakika wanafaa na kuandaliwa kutangaza Mfufuka,lakini Bwana hajali hilo.Kile anachojali ni kwamba watoke nje na kwenda kutangaza.Kwa sababu furaha ya Pasaka haijatolewa kuhifadhiwa binafsi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko akianza tafakari yake Jumatatu ya Pasaka ambapo kiutamaduni inaitwa Pasaka ya Malaika, kwa sababu  Malaika aliwatokea mashuhuda wa ufufuko, amesema “Katika Oktava ya Pasaka ni kama siku moja ambayo inaongeza furaha ya Ufufuko. Kwa maana hiyo Injili ya Liturujia ya siku inaendelea kusimulia juu ya Mfufuka na alivyo watokea wanawake ambao walikuwa wamekwenda kaburini (Mt 28,8-15). Yesu alikutana nao na kuwasalimia; alafu akawambia mambo wawili ambayo yatakuwa mazuri hata kwetu sisi kuyapokea kama zawadi ya Pasaka”.

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari kwa waamini na mahujaji wengi sana ambao wamefika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, tarehe 18 Aprili 2022 amesema “kwa mara ya kwanza aliwahakikishia kwa maneno rahisi: “Msiogope”. Bwana anajua kwamba hofu ni adui zetu za kila siku. Anajua hata kuwa hofu zetu zinazaliwa kutokana na woga,  hofu ya kifo: hofu ya  mahangaiko, ya kupoteza watu wapendwa, kukaa vibaya  tunaposhindwa kufanya chochote zaidi. Lakini Pasaka Yesu ameshinda kifo. Hakuna yoyote, zaidi ya yeye anaweza kutueleza kwa uhakika juu ya neno: ‘Msiogope’. Bwana anasema hasa pale, karibu na kaburi alimotoka kwa ushindi. Anatualika kwa namna hiyo kutoka katika makaburi yetu ya hofu. Papa amekazia tena kwamba ‘sikilizeni vizuri, kutoka katika makaburi ya hofu zetu, kwa sababu hofu zetu ni kama makaburi, zinatuzika ndani mwake’.

Papa akisalimiwa mahujaji na waamini wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu
Papa akisalimiwa mahujaji na waamini wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu

Baba Mtakatifu amesema “Yeye anajua kwamba hofu daima zipo zimechuchumaa katika mlango wa moyo wetu na tunahitaji kusikia anarudia kusema: “Usiogope”: katika asubuhi ya Pasaka kama ile asubuhi ya kila siku kusika Usiogope, na kuwa na ujasiri”. Baba Mtakatifu ameongeza kusema: “Kaka na dada ambao mnaamini katika Kristo, usiogope, ni mimi,  anasema Yesu, nimejaribu mimi kifo kwa ajili yako, na nimebeba ubaya wako. Na sasa nimefufuka kwa kukueleza kwamba niko hapa na wewe, daima usiogope!” Lakini je ni kufanya nini ili kupambana na hofu hizo? Kwa kujibu swali, Papa amesema “Tunasaidiwa na jambo ambalo Yesu aliwambia wanawake: “Enendeni mkawambie ndugu zangu waende Galilaya ndiko watakakoniona”,

Kwa maana hiyo kwenda kutangaza. Baba Mtakatifi amesema: “Hofu daima zinatufunga sisi wenyewe. Yesu kinyume chake anatufanya kuondokana na hofu hizo, na kututuma kwenda kwa wengine. Na ndiyo dawa”. Kwa kutoa mfano, Papa amesema mwingine anaweza kusema kuwa: “Mimi siwezi kwani sina uwezo!  Lakini wale wanawake hawakuwa kwa hakika wanafaa na kuandaliwa kutangaza Mfufuka, japokuwa Bwana hajali hilo. Kile anachojali ni kwamba watoke nje na kwenda kutangaza. Kwa sababu furaha ya Pasaka haijatolewa kuhifadhiwa binafsi. Furaha ya Kristo inaongezeka kwa kuitoa, inaongezeka kwa kuishirikisha. Ikiwa tunajifungua mioyo na kupeleka Injili, moyo wetu unapanuka na kushinda hofu. Hiyo ndiyo siri ya kutangaza na kushinda hofu, amesisitiza Papa.

Waamini katika Sala ya Malkia wa Mbingu Jumatatu ya Pasaka
Waamini katika Sala ya Malkia wa Mbingu Jumatatu ya Pasaka

Andiko la siku hii, linasimulia japokuwa tangazo linaweza kukutana na kizingiti cha uongo. Injili inasimulia kwa hakika kutangaza uongo wa maaskari waliokuwa wamelinda kaburi la Yesu. Wao walilipwa kwa kiasi kikubwa cha fedha kama Injili isemavyo na walipewa maagizo haya: “Semeni ya kwamba Wanafunzi  wake walikuja usiku na kumwiba wakati sisi tulipokuwa tumelala. Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema: Ninyi mlikuwa mmelala. Na katika usingizi mkaona jinsi walivyoiba mwili? Kuna kitu hapo ambacho hakiendi, lakini ni jambo ambalo wote wanaamini kwa sababu katikati kuna fedha. Ni uwezo wa fedha, bwana mwingine ambaye Yesu alisema kamwe hasihudumiwe. Ni bwana wawili “Mungu na fedha. Fedha isihudumiwe kamwe”, amesisitiza. Na ndiyo tazama uongo hapo, mantiki za kugeuza mambo, ambayo yanakwenda kinyume na tangazo la ukweli. Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema huo “Ni mwito hata kwetu sisi dhidi ya uongo katika maneno na katika maisha, yanachafua tangazo, yanaharibu ndani na kupeleka katika kaburi. Uongo unaturudisha nyuma, hasa katika kifo na katika kaburi. Mfufuka kinyume chake anatutaka tuondokane na makaburi hayo ya uongo na kuyategemea.

Waamini wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu
Waamini wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu

Mbele ya Bwana mfufuka, kuna jambo jingine la muungu fedha ambao unachafua kila kitu, unafunga milango ya wokovu. Hiyo ipo kila mahali, katika maisha ya kila siku, kuna kishawishi cha kuabudu muungu fedha”. Baba Mtakatifu Francisko amesema hata hivyo mara nyingi tunakashfu kupitia habari, na tunagundua ulaghai, na uongo katika maisha ya watu na katika jamii. Lakini tunapaswa kutoa hata jina la uongo tulio nao ndani mwetu. Na tuuweke upofu wetu, uongo wetu, mbele ya mwanga wa Yesu Mfufuka. Yeye anataka kutupeleka katika mwanga wa mambo yaliyofichika ili kutufanya tuwe shuhuda wa uwazi na angavu wa furaha ya Injili, wa Ukweli ambao unatufanya kuwa huru (Yh 8,32) . Maria, Mama wa Mfufuka atusaidie kushinda hofu zetu na atuzawadie upendo mkubwa kwa ajili ya ukweli. Amehitimisha Baba Mtakatifu Francisko.

TAFAKARI YA PAPA WAKATI WA SALA YA MALKIA WA MBINGU 18.04.2022
18 Aprili 2022, 12:51