Tafuta

2022.04.23 PAPA ALIKUTANA NA WASHIRIKI WA JUKWAA LA KIMISIONARI LA VIJANA 2022.04.23 PAPA ALIKUTANA NA WASHIRIKI WA JUKWAA LA KIMISIONARI LA VIJANA  

Papa na vijana:muwe wamisionari wa furaha na upendo

Katika mkutano wa Papa Francisko na washiriki wa Kongamano la kimisionari la vijana Aprili 23 jijini Vatican ambapo,amewashuri wasimame,watunze ndugu na kushuhudia kwa njia ya maisha ya Injili ya furaha na sio kuwa na tabasamu za matangazo ya kibiashara lakini tabasamu la kweli litokalo moyoni!

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 23 Aprili 2022 amekutana na washiriki wa Kongamano la kimisionari Vijana  lililoandaliwa na Baraza la maaskofu Italia (CEI). Amemshukuru Katibu wa Kitaifa kwa maneno yake aliyomwelekeza kwa niaba ya wote. Wamefika kutoka katika maeneno mbali mbali ya Italia kwa ajili ya Kongamano la kimisionari la vijana kwa kuongozwa na mada “Back to the COMIGI: La missione riparte dal futuro”, yaani “Kurudi katika Kongamano la kimisionari la vijana: Utume unaanza na wakati ujao”. Ni shughuli iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Taasisi za kimisionari, ambayo inastahiki ratiba yao ya uundaji, ikiwaalika kujipyaisha katika kujitolea kwao katika utume wa Kanisa kwa ujumla. Kwa maana hiyo ni fursa kwa ajili ya kuadhimisha miaka 500 tangu kuanzishwa kwa harakati ya vijana wamisionari katika Baraza la Kipapa la Matendo ya Utume, leo hii Utume wa Vijana”. Ni tarehe muhimu kwa ajili ya vijana wamisionari: ni fursa kwa ajili ya kufanya kumbu kumbu ambayo iliweka msingi wa kuzaliwa kwa harakati hiyo. Na kutokana katika kusima historia yake na imani yake wanatapata msukumo wa mwamko mpya wa kimisionari wa kuishi siku baada ya siku. Utume ni namna hiyo, siku baada ya siku na  siyo mara moja tu  bali kwa kuishi kila siku. Kwa maana hiyo Papa Francisko amependa kuwakabidhi vitenzi vitatu  au maneno rahisi vya kukumbuka ambavyo amefikiria ni msingi kwa ajili ya utume wao leo hii hasa kwa upande wa vijana. Vitenzi hivyo vinapatikana katika hatua tatu za Agano Jipya kwa kutazama Matendo ya Yesu na wanafunzi wake. Vitenzi hivyo ni: Simama, tunza na shuhudia. Haya yanaelezea namna tatu halisi ambazo Papa anawatakia yaweze kuwasaidia katika mchakato wao kwa ajili ya wakati ujao.

Papa alikutana na washiriki wa Kongamano la Kimisionari la vijana
Papa alikutana na washiriki wa Kongamano la Kimisionari la vijana

Akianza na cha kwanza Simama, kimechukuliwa kutoka sehemu ya Injili ya Luka ambayo Yesu anamrudishia mtoto maisha wa mjane wa Naini (Lk 7: 11-17).  Ni Luka pekee, mwenye umakini sana na mienendo ya roho ya mwanadamu hasa, ya wanawake na ndiye anayeandika tukio hilo. Kwa kusoma andiko hilo, unavutiwa na mwenendo wake, ameisitiza na kwamba, Yesu alifika katika mji huu na kuona kwamba kuna maandamano ya mazishi yanayotoka nje ya mji; mama mjane akisindikiza jeneza la mwanae kwenda kuzikwa; mwinjili anabainisha kuwa: “Bwana alipomwona, alishikwa na huruma nyingi kwa ajili yake, akamwambia: ‘Usilie!’ (Lk 7, 13). Alikwenda kwa mama yake na kusema: “Usilie”.  Hiyo huwa tunasema hivyo tunapokwenda kwenye mikesha ya mazishi neno la “usilie”. Lakini Yesu alisema hivyo ili kuanza tendo la dhati. Aliguswa  na maumivu ya walio wa mwisho, Yesu anahusika na maumivu ya wale ambao mara nyingi wanateseka kwa  ukimya na wenye heshima, ya wale ambao wamepoteza tumaini na wale ambao hawaoni tena wakati ujao. Kifo cha mtoto, katika hali hiyo, kilimaaniisha kupoteza kila kitu. Yesu alikaribia jeneza na kuligusa. Yeye hakujali kama kugusa huko kungemfanya kuwa mchafu, kama ilivyokuwa ikisema Sheria. Alikuja kuokoa wale walio katika giza na katika uvuli wa mauti. Kisha akasema “Kijana, nakuambia, inuka!” Hiki ndicho kitenzi cha “Simama”.  Papa ameomba kufikiria kwa mawazo yao wakiwa mbele ya jeneza la kijana huyo, mvulana kama wao: wakisikia Yesu anasema: “Nanakuambia: inuka!”. Kumfufua mvulana huyu kunamaanisha kurudisha maisha yajayo kwa mama yake na kwa jamii nzima pia”, Papa amefafanua.

Papa alikutana na washiriki wa Kongamano la Kimisionari la vijana
Papa alikutana na washiriki wa Kongamano la Kimisionari la vijana

Neno hilo la Yesu, bado linajirudia katika mioyo ya vijana wengi leo hii na anaelekeza mwaliko kwa kila mmoja: “Nanakuambia simama!”. Hii ndiyo maana ya kwanza ya utume ambayo amewaalika kutafakari juu yake. Kwa sababu “Yesu anatupatia nguvu ya kusimama na anatutaka tujikomboe na kifo cha kujiondoa ndani yetu, kutoka katika ulemavu wa ubinafsi, uvivu, na ujuu juu. Kupooza huko kidogo kupo kila mahali”. Na ndiyo inazuia na kutufanya tuishi imani kama ya makumbusho, na sio imani yenye nguvu, imani ambayo imekufa zaidi kuliko hai. Kwa sababu hiyo, ili kutatua mtazamo huu mbaya, Yesu anasema: “Simama!”. “Simaneni”, ili kuzinduliwa tena kuelekea mustakabali wa maisha, uliojaa matumaini na upendo kwa ndugu. Utume inaanza upya tunapochukua neno la Bwana Yesu kwa uzito kwamba: “Simama tena”!

Papa alikutana na washiriki wa Kongamano la Kimisionari la vijana
Papa alikutana na washiriki wa Kongamano la Kimisionari la vijana

Kipengele kingine kilichounganishwa na cha kwanza kinapatikana katika kifungu maarufu kutoka kwa Msamaria Mwema (rej. Lk 10: 25-37). Kwa mara nyingine tena mwinjili ni Luka. Daktari wa Sheria anauliza Yesu: “Jirani yangu ni nani?”, Naye Yesu akajibu kwa kutumia mfano wa Msamaria Mwema: mtu alishuka kutoka Yerusalemu kuelekea Yeriko na njiani aliibiwa na kupigwa na wanyang'anyi, na kubaki karibu ya kufa, kando ya barabara. Tofauti na wahudumu wawili wa ibada, walioomwona lakini wakipita mbali, Msamaria, yaani, mgeni kwa Wayahudi wa wakati huo, ambaye hakuwa na urafiki nao sana, alisimama na kumtunza. Na pia analifanya kwa njia ya akili sana, kwani alimpatia huduma ya kwanza awezavyo, kisha akampeleka kwenye nyumba ya wageni na kumlipa mwenye nyumba ili aweze kuangaliwa siku zinazofuata. Ni vipigo vichache vya kuelezea kipengele kingine chautume, hicho ni kitenzi cha pili cha kutunza. Hiyo ni kuishi upendo kwa njia ya nguvu na ya akili. Leo hii tunahitaji watu hasa vijana wenye macho ya kuona mahitaji ya wanyonge na wenye moyo mkubwa unaowafanya wawe na uwezo wa kujitoa kikamilifu.

Papa alikutana na washiriki wa Kongamano la Kimisionari la vijana
Papa alikutana na washiriki wa Kongamano la Kimisionari la vijana

Baba Mtakatifru Francisko amewambia kuwa hata wao vijana pia wameitwa kuweka ujuzi wao kwa ajili ya  matumizi mazuri na kuweka akili yao katika huduma, kuandaa upendo na mipango ya mbali iliyo mipana. Leo ni zamu yao, lakini wao sio wa kwanza! Ni wamisionari wangapi  yaani “Wasamaria wema” ambao wameishi utume wa kuwatunza kaka na dada waliojeruhiwa njiani! Katika nyayo zao, kwa mtindo na mbinu zinazofaa kwa wakati wetu, sasa ni juu yao kutambua upendo wa busara na ufanisi, upendo wa ubunifu na wa akili, usio wa matukio lakini unaoendelea kwa wakati, wenye uwezo wa kusindikiza watu katika safari yao ya uponyaji na ya ukuaji. Hiki ni kitenzi cha pili ambazo Papa Francisko amewakabidhi ili kutunza ndugu. Bila ubinafsi, bali kutumikia, na kusaidia. Hatimaye, kipengele cha tatu muhimu cha utume kinapatikana katika kipindi cha Matendo ya Mitume, ambacho kinafaa kwa kipindi cha Pasaka tunayoendelea nayo. Kiukweli, baada ya kufufuka kwake, kwa siku arobaini Yesu alijionesha kwa wanafunzi wake. Alifanya hivyo ili kuwafafanulia fumbo la kifo chake, kuwasamehe kutokana na kutoroka kwao wakati wa majaribu yake, lakini zaidi ya yote kuwatia moyo wawe mashahudua wake ulimwenguni kote. Yesu anasema hivi: “Mtapokea nguvu za Roho Mtakatifu atakayewavuvia juu yenu, nanyi mtakuwa mashuhuda wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi yote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” (Mdo 1:8). Kila Mkristo, aliyebatizwa kwa maji na Roho Mtakatifu, anaitwa kuishi kana kwamba amezama katika Pasaka ya kudumu na kwa hiyo kuishi ufufuko. Papa ameongeza “Usiishi kama mtu aliyekufa, ishi kama mtu aliyefufuliwa! Zawadi hii si kwa ajili yetu tu, bali imekusudiwa kushirikishwa na kila mtu. Utume hauwezi kushindwa kuhamasishwa na shauku ili hatimaye kuweza kushirikisha furaha hii na wengine. Uzoefu mzuri na wa kutajirisha wa imani, ambao pia unajua jinsi ya kukabiliana na upinzani usioepukika wa maisha, karibu kawaida huwa wa kusadikisha.

Papa alikutana na washiriki wa Kongamano la Kimisionari la vijana
Papa alikutana na washiriki wa Kongamano la Kimisionari la vijana

Mtu anayesimulia Injili kwa njia ya  maisha yake mwenyewe, hiyo inavunja  hata mioyo migumu zaidi. Kwa maana hiyo Papa amewakabidhi neno la mwisho la mmisionari Mkristo. Kushuhudia na maisha yao. Na asiyetoa ushuhuda na maisha, kwa kujifanya ... ni kama mtu ambaye ana hundi fulani mkononi mwake lakini hasaini. “Nikuzawadia hii” Lakini haina maana. Kushuhudia ni kuweka sahihi ya mtu kwenye mali yake, sifa zake, na wito wake. Ka maana hiyo Papa amewaomba wasichana na wavulana waweke saini daima, Saini hiyo kuiweka katika mioyo yao. Baba Mtakatifu amewaomba wasihahau maneno hayo ya kusimama kutoka katika kukaa, kuwatunza ndugu na kushuhudia Injili ya furaha. Amewaaga na salamu ya Mtakatifu Oscar Romero: “Kadiri mtu anavyokuwa na furaha, ndivyo utukufu wa Kristo unavyodhihirika ndani yake”. Amewatakia wawe wamisionari wa furaha na wamisionari wa upendo. Tangazo linafanywa kwa tabasamu, na si kwa huzuni. Mtakatifu Paulo VI, katika Wosia wake wa Kitume wa Evangelii nuntiandi, karibia na mwisho alisema kwamba ni jambo baya kuona wainjilishaji wenye huzuni na kuhuzunika”. Amewaomba wasome karibu kurasa mbili za mwisho: maelezo ya mwinjili hodari, mmisionari, na wale walio na huzuni ndani yao wenyewe, ambao hawawezi kutoa maisha kwa ajili ya wengine. Kwa hilo Papa anatamani wao wawe wamisionari wa furaha na upendo. Tangazo lazima lifanywe kwa tabasamu: lakini si kwa tabasamu la kitaaluma, au yule anayetangaza dawa ya meno, hapana, hiyo si nzuri. Hilo halihitajiki. Tangazo lazima lifanywe kwa tabasamu, lakini kwa tabasamu ya dhati, na sio kwa huzuni. Kushirikisha Habari Njema kila wakati na watahisi furaha.

HOTUBA YA PAPA KWA KONGAMANO LA KIMISIONARI LA VIJANA ITALIA

 

24 April 2022, 17:04