Tafuta

2022.04.23 Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Fiat. 2022.04.23 Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Fiat. 

Papa: Ukweli wa Unjilishaji na Roho ni uijilishaji na Roho Mtakatifu!

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake na washiriki wa jukwaa lililoandaliwa na Chama cha Fiat amewaelezea kuwa ulimwengu wa sasa ni maskini wa ubinadamu na hivyo ni dharura ya kuwa na ustaarabu wa upendo. Wote tunaitwa kuwa mstari wa mbele wa Kanisa linalotoka Nje na masuala ya uinjilishaji ndiyo kitovu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi 23 Aprili 2022 amekutana na washiriki Mkutano ulioandaliwa na Chama cha Fiat. Kwa kuongozwa na mada ya “kufuata nyayo za Kardinali Suenens- Roho Mtakatifu, Maria na Kanisa”. Amemshukuru Bwana kwa ajili ya kazi ya Kardinali Suenens na Veronica O’Brien, ambayo inaendelea leo hii katika utume wao. Kwa uaminifu wa Kiinjili wa waanzilishi hao  wao wanajikita kushirikishana Injili kwa kila mtu ambaye Mungu Mpaji anaweka katika njia zao. Baba Mtakatifu Francisko amesema leo hii masuala ya uijilishaji ni moyo wa utume wa Kanisa. Leo hii ni wazi katika entensi zile za Papa Paulo VI alivyosema kuwa "Wito wa Kanisa ni Unjilishaji; furaha ya Kanisa ni Uinjilishaji (rej. Evangelii nuntiandi, 14; 80).  Daima leo hii na zaidi  inawaaalika wote kuwa mstari wa mbele katika Kanisa linalitoka nje, chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifu. Kiukweli Unjilishaji na Roho ni unjilishaji na Roho Mtakatifu tangu wakati ule  na kwamba Yeye ni roho ya Kanisa ya Unjilishaji (rej, Evangelii gaudium, 261). Katika ulimwengu ambao unazidi kuwa wa kiulimwengu zaidi tunahitaji kuwa wafuasi aminifu katika kukiri kwa imani na wenye uweze wa kueneza cheche za matumaini kwa wanawake na wanaume wa wakati huu.

Papa na Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Fiat
Papa na Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Fiat

“Majanga ambayo tunaishi katika wakati huu hasa vita katika eneo la Ukraine ambalo ni karibu nasi linatulita katika udharura wa kuwa na ustaarabu wa upendo. Katika mtazamo wa kaka na dada waathirika wa ubaya wa kutisha wa vita, tunaona  kuna huhitaji wa kina na zito wa maisha ambayo yanahitaji hadhi, amani na upendo". Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba kama Bikira Maria, tunatakiwa kuendelea kukuza roho ya utume kwa ajili ya kuwa karibu na wale ambao wanateseka, kwa kuwafungulia mioyo yetu. Lazima kutembea nao, kupambana nao kwa ajili ya hadhi yao ya kibindamu  ya kueneza kila mahali manukato ya upendo wa Mungu. Kwa njia ya roho Mtakatifu, katikati ya watu daima kuna Maria. Yeye alikuwa akiwafanya wanafunzi kumwomba (Mdo 1,14)  na kwa namna hiyo iliwezekana kuibuka kwa  umisionari uliokuja siku ya Pentekoste. Yeye ni Mama wa Kanisa mwinjilishaji na bila yeye hatuwezi kuelewa kwa dhati Roho wa Uinjilishaji mpya. (Evangelii gaudium, 284). Baba Mtakatifu amesema, nyumba yetu ya pamoja, imetetemeshwa na migogoro mingi. Lakini hatupaswi kuogopa migogoro hiyo; migogoro inatutakasa  na inatufanya tuondokane tukiwa bora bila hofu.

Papa na Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Fiat
Papa na Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Fiat

Kutokana na hiyo kuna haja ya kujenga ubinadamu, jamii moja ya mahusianao kidugu na iliyojaa maisha. Kwa uhalisia, mahusiano yanatokana na umoja ambao unainamia daima kuelekea mwingine kwa kumfikiria mwenye thamani, ambaye anastahili, anakubalika na vizuri zaidi ya mtazamo wa kijuu juu wa kimwili na au kimaadili. Upendo kwa wingine unatusukuma kutafuta ubora wa maisha yake. Ni kwa kukuza namna hiyo mahusiano tu ndipo inawezakana  kufanya urafiki kijamii ambao haubagui hata mmoja na udugu unaofungulia kwa wote (Fratelli tutti,94). Papa amewaalika kwa maana hiyo kuwa mashuhuda wa huruma, upole na wingi wa rehema za Mungu.

Papa na Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Fiat
Papa na Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Fiat

Kanisa lina imani kwao na hivyo amewashauri watende  kwa maneno na ushuhuda, ujumbe wa nguvu katika ulimwengu wetu uliyo maskini wa ubinadamu.  Wao wanaweza kuchota, kwa njia ya sala, na utume wenyewe, katika chemichemi ya wingi na ya ukweli na watapata kutoka umoja na Kristo aliyekufa na kukufuka nguvu ya kuona ulimwengu kwa mtazamo chanya, mtazamo wa upendo, mtazamo wa upendo, mtazamoa wa huruma na upole, kuwa umakini maalum kwa watu wasio na fursa na walio pembezoni. Baba Mtakatifu amewakabidhi kila mmoja wao wa washiriki wa Jukwaa na wajumbe wote wa Chama cha Fiat na kwa moyo wote amewabariki wao na familia zao. Wasisahau kumwombea.

HOTUBA YA PAPA KWA CHAMA CHA FIAT
23 April 2022, 15:53