Papa Francisko:katika Predicate Evangelium tunaamini leo hii ushuhuda katika kizazi kijacho
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika dibaji ya Papa Francisko kwenye kitabu cha mahojiano kiitwacho “Praedicate Evangelium”, cha mazungumzo kati ya Fernando Prado na Kardinali Rodriguez Maradiaga Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tegucicalpa (Honduras) Baba Mtakatifu Francisko anaandika kuwa tangu Mtaguso II wa Vatican, Kanisa Katoliki limekuwa na mageuzi tofauti ya Curia Romana katika kutafuta kuendana na hitaji la nyakati, la maisha ya kikanisa na mapakeo ya Mtagusio wenyewe ambao unandelea kuwa dira. Mtakatifu Paulo VI alitaka kuendana na Curia Romana kwa wale ambao walikuwa wamemaliza ktsheherekea Mtaguso II wa Vatican kwa kuwa na Katiba ya Kitume ya Regimini Ecclesiae Universae. Mtakatifu Yohane Paulo II, miaka kadhaa iliyopita,alichapisha Katiba ya Pastor Bonus, yaani Mchungaji mwema akitaka kuanzisha mabadiliko mengine ili kuendana na uendeshaji wa shughuli za Curia Romana katika Gombo jipya la sheria za Kanoni za Kanisa, iliyokubaliwa mnamo 1983.
Mageuzi ni muhimu yaliyoandaliwa mapema
Na kwa upande wake, hata Papa Mstaafu Benedikto XVI alifanya mabadiliko kadhaa na kuendana na katiba ya Pastor Bonus yaani Mchungaji Mwema)kwa njia ya Motu Proprio mbali mbali ili kuweza kukabiliana na baadhi ya changamoto, na kutimiza mahitaji ya lazima ambayo yaendane na hali halisi iliyokuwa ikitakiwa. Tangu wakati huo alifikia kuunda hata muhimili mpya iitwao: “Baraza la Kipapa la Unjilishaji mpya”. Kabla ya kubadilisha Baraza, wakati wa Baraza Kuu ambalo lilitanguliwa na Mkutano Mkuu wa uchaguzi, kati ya mambo mengi muhimu ya kushauriwa, kulikuwa na ombi hai kwa wote kwa Papa mpya ambaye angechaguliwa ili aweze kujikita katika kufanya mageuzi mapya ya Curia Romana. Ilikuwa inaonesha wazi ambavyo kilikuwa ni kitu cha dharura, cha lazima. Kwa maana hiyo mageuzi hayo yalitokana na hilo, Papa amefafanua. Sawa sawa hilo alithubutu kufanya baadhi ya msisitizo, kwa kufikiria kwamba ingekuwa ni aina ya uwajibikaji wa kupeleka mbele. Lakini mambo yalikwenda kinyume. Na ndiyo tangu mwanzo, imeweza kufanyika kazi kwa wote katika miaka hii.
Katiba mpya ni kipimo cha mageuzi ya Curia Romana
Baba Mtakatifu Francisko anashukuru nyumba ya ushapishaji ya Waklaretiani wa Madrid nchini Hispania kwa huduma hiyo mpya. Na amebainisha kuwa hizi sio nyakati rahisi kwa ajili ya utume wa kuchapisha. “Ninashukuru Baraza lote la makardinali kwa uvumilivu wa kazi katika kipindi hiki kirefu cha kutungwa. Ninamshukuru kwa namna ya pekee Kardinali Rodríguez Maradiaga kwa sababu ya huduma yake bila kuchoka katika Makao ya Petro na wakati huo huo pongezi kwa mahojiano haya. Ninaamini kwamba maana na mchakato wa kazi hii ya kina na ya uamuzi ya kusahihisha na pendekezo imechunguzwa vya kutosha ndani yake. Ndani yake inafanya kuona mageuzi ya Curia kuwa ni ya juu katika Katiba ya kitume”. Baba Mtakatifu Francisko ameandika kwamba: “Praedicate Evangelium” yaani Hubirini Injili ambayo ni jina la Katiba Mpya ya Kitume, ni moja ya vipimo vya mageuzi. Ni mategemeo kuwa yote ambayo yanafungwa ndani ya Katiba hiyo yataonekana daima kwa kadiri itakavyokuwa imechapishwa na kujukita kwenye matendo. Mambo haya ambayo yanaonekana katika Katiba ya kitume yalikuwa tayari yametolewa tangu miaka ya kwanza ya Upapa na yameleta matunda ya kutosha. Mengine yatazaa matunda kwa wakati wake.
Kanisa litaendelea kutangaza Injili
Mapinduzi katika miundo na kwa muktadha wa uandaaji ni ya lazima hakuna shaka, lakini kilicho muhimu sana ni kufanywa upya kwa akili na mioyo ya watu. Sote tumeitwa kukunja mikono yetu”, Papa amesisitiza. Na kwa kuhitimisha dibaji yake amesema “Na tusisahau kuwa sheria na hati daima ni finyu na karibu zinapita daima. Kwa wakati mwingine zitakuja. Na katika mazingira mengine zitaleta joto jipya katika ulimwengu…. Na Kanisa, katika mazungumzo yake thabiti, na ulimwengu, kwa msimamo katika asili na katika uaminifu wa Tamaduni, kwa mara nyingine tena zitakabiliana na maisha yake na miundo yake ya kibinadamu kwa hali ya mabadiliko ya nyakati. Kwa namna hii Kanisa litaendelea kutangaza Injili ulimwenguni kwa mtindo mpya. Na hali yetu, kwa kuwa tunaamini kwamba “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele” (Eb 13, 8). Na hivyo sisi tunaamini leo hii kuwa ushuhada katika kizazi kitakachokuja”.