Tafuta

2022.04.20 Papa alikutana na uwakilishi wa Global Researchers Advancing Catholic Education Project. 2022.04.20 Papa alikutana na uwakilishi wa Global Researchers Advancing Catholic Education Project. 

Papa Francisko: mwalimu bora anasindikiza,anasikiliza na kuzungumza!

Jumatano asubuhi kabla ya kuanza katekesi yake,Papa Francisko alizungumza na kikundi cha uwakilishi wa“Global Researchers Advancing Catholic Education Project” kwa kuwaelezea umuhimu wa elimu endelevu ambapo inaendeleza urithi wa wakati uliopita lakini wa kwenda mbele,bila kusimama tu katika mizizi ili kufanya kukua kwa kila mmoja.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuelimisha sio kujaza kichwa mawazo, kwa sababu wafundwe ili waweze kujitegemea tu lakini ni kutembea pamoja na watu katika mivutano kati ya hatari na usalama. Ndivyo Papa Francisko alithibitishaa katika hotuba yake bila kusoma, mara baada ya kuwakabidhi hotuba yake aliyokuwa ameiandaa kwa uwakilishi wa “Global Researchers Advancing Catholic Education Project” (GRACE), yaani (Watafiti wa Kimataifa Kuendeleza Mpango wa Elimu Kikatoliki): Huu ni mpango mpya wa utafiti kimataifa ambao umeandaliwa na watu wa kujitolea kwa lengo la kuhamasisha thamani ya elimu katoliki katika heshima ya utambulisho na mazungumzo. Katika mkutano huo ulifanyika katika ukumbi mdogo wa Paulo VI kabla ya kwenda katika katekesi yake, tarehe 20 Aprili 2022 ambayo ilifanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mara baada ya siku nyingi kutokana na janga la uviko.

Papa Francisko alikutana na Uwakilishi wa Watafiti wa Kimataifa Kuendeleza Mpango wa Elimu ya Kikatoliki
Papa Francisko alikutana na Uwakilishi wa Watafiti wa Kimataifa Kuendeleza Mpango wa Elimu ya Kikatoliki

Hatari na mivutano ya kichwa na moyo

Baba Mtakatifu Francisko alithibitisha kuwa ni kuhatarisha katika mivutano kati ya kichwa na moyo na mikono; katika maelewano hadi kufikia kufikiri kile ambacho ni kuhisi na kufanya kile ambacho unafikiria ili kuleta pamoja maana hiyo ni maelewano. Kwa walimu wa shule ya msingi, sekondari na vyuo vikuu, Baba Mtakatifu anaomba kujiweka karibu na wanafunzi katika mchakato wa elimu. Haiwezekani kuelimisha bila kutembea pamoja na watu wanaoelimishwa. Ni vizuri wanapopatikana walimu ambao wanatembea pamoja na vijana wa kike na kiume.

Kuelimisha ni kusaidia makuzi

Papa Francisko amesema kwamba elimu sio kusema mambo ya kurudia rudia; kuelimisha ni kufanya kukutana kile ambacho kinasema ukweli. Vijana wa kike na kiume wanayo haki ya kukosea lakini pia walimu wawasindikize katika mchakato wa safari ya kuelezwa makosa hayo, kwa sababu wasije kuwa hatari. Kazi ya kweli na muelimishaji, haiogopi kamwe makosa, bali anasindikiza, anawaunga mkono, anawasikiliza na kuzungumza. Haogopi na anawasubiri. Huko ndiko kuelimisha kibinadamu, kuelimisha ndiyo kupeleka mbele na kufanya kukua na kusaidia wakue.

Kuelimisha katika utamaduni ambao ni endelevu

Kwa mujibu wa msemaji wa Wawakilishi wa “Global Researchers Advancing Catholic Education Project” (GRACE), yaani Watafiti wa Kimataifa Kuendeleza Mpango wa Elimu ya Kikatoliki) amefungua mazungumzo na Papa Francisko na kumwelezea Baba Mtakatifu kuwa lengo la mpango huo ni kiukweli ni  kuelimisha si tu katika kuonesha fahamu, lakini pia katika kutoa nafasi hata muktadha wa kiroho na kichungaji na kwa kiasi gani wazee wanaweza kurithisha elimu kwa vijana. Kwa maana hiyo Papa amesisitiza kwamba ni muhimu kuzungumza kati ya vijana na wazeee, kwa sababu ili mti uweze kukua inahitaji mahusiano ya karibu sana na mizizi yake, na hivyo amekumbuka na kuwamsimulia kwamba kuna mtunzi mmoja wa mashairi katika nchi yake alisema jambo zuri: “Kila kitu ambacho mti una maua hutokea kwa kile kilicho chini ya ardhi. Bila mizizi huwezi kuendelea. Ni kwa kuwa na mizizi yetu tunakuwa watu”.  Papa Francisko anasema pasiwepo mapokeo baridi na magumu na kwamba tamaduni za kweli zinachukua kutoka zile za zamani ili kwenda mbele. “Utamaduni sio mtulivu tu ni mwendelezo wa nguvu, inayolenga kwenda mbele”.

21 April 2022, 16:40