Papa Francisko:mapadre waungamishi wawe na msamaha mkubwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 7 Aprili 2022 amekutana na kuzungumza na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa ya Teutonic ya Mtakatifu Maria wa Roho, wakiwa katika fursa ya adhimisha miaka 500 tangu kuchaguliwa kwa Papa Adrian VI, ambaye alikuwa ni mmojawapo wa Papa wa mwisho kutoka Ujerumani, na kaburi lake limo katika Kanisa la Taasisi yao mjini Vatican. Papa Adrian VI, Florensz alizaliwa huko Utrecht, ambayo wakati ule ilikuwa sehemu ya Imaya ya Roma Takatifu ya Taifa la Kijerumani. Alipata elimu nzuri kutoka katika Chuo Kikuu cha Lavanio. Baadaye alikuwa mfuasi wa Karoli V na baadaye baada ya kumaliza shughuli muhimu za kikanisa na kisiasa, alipanda kwenye jukumu la juu na kuundwa kuwa Kardinali mnamo mwaka 1517. Aliposikia habari za kuchaguliwa kwake kuwa Askofu wa Roma, mara moja alikataa, lakini kwa maana ya uwajibikaji hatimaye akakubali.
Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa katika upapa wake mfupi, ambao ulidumu kwa muda mfupi wa zaidi ya mwaka mmoja tu, alitafuta hasa kujikita na maridhiano katika Kanisa na katika ulimwengu, kwa kuweka kwenye matendo ya Mtakatifu Paulo kwa mujibu wa Mungu ambaye aliwakabidhi kwa dhati mitume wake , huduma ya upatanisho (2 Kor 5,18…). Kwa maana hiyo alimtuma Balozi wa kitume Chieregati huko Dieta ya Norimberg ili kuweza kupatanisha Kanisa la Kiluteri na wafuasi wake, huku akiomba kwa wazi msamaha kwa ajili ya dhambi za wakuu wa Sekretarieti Kuu ya Vatican. Katika suala la kisiasa, na kushinda ugumu mwingi, alijitahidi kuweza kufikia makubaliano kati ya nguvu hizi mbili zenye mitafaruko. Mfalme Francis I wa Ufaransa, na Mfalme Karoli V wa Asburg hata wao aliweza kufikia pamoja kuondoa kabisa tishio la alama hiyo kwa kushinda wanajeshi wa Ottoman
Baba Mtakatifu Francisko amesema, kwa bahati mbaya Papa Adrian kwa sababau ya kifo cha mapema, hakuweza kuhitimisha mpango wowote. Lakini ushuhuda wake wa kufanya kazi sana bila kuchoka kwa ajili ya imani, kwa ajili ya haki na amani inabaki kuwa hai katika kumbu kumbu ya Kanisa, amesisitiza Papa. Kwa mfano wa maisha na jitihada za Papa Adrian, Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo waweze kukua katika wito wao wa kuwa watumishi wa Kristo. Bwana awasaidie katika huduma yao na kuwapeleka katika imani yenye kusimika mizizi katika upendo wake, kwa kuishi kwa furaha na kujitoa. Kwa namna ya pekee kwa kufikiria shauku ya kuhamasisha maelewano na mapatano, Papa Francisko amewashauri wafuate nyayo zake hasa katika kuwa wahudumu wa sakramento ya ya upatanisho.
Papa ameongeza kusema: “Hili ni muhimu: kazi ya muungamishi ni kusamehe, si kutesa. Kuweni na huruma, wasamehevu wakuu, na ndivyo hivyo Kanisa linawataka”. Hii ina maana ya kutoa muda wa kusikiliza maungamo, na kufanya vizuri kwa upendo, kwa hekima na huruma nyingi. Lakini si hiyo tu Papa amsema. Huduma hiyo inahusiana hata kuhubiri, katekesi, kuwasindikiza kiroho; na hii inahitaji hasa kama daima kushuhudia. Ili kuwa watumishi wa msamaha wa Kristo, Kuhani lazima ajue kusamehe wengine; lazima awe na uhuruma katika uhusiano wake, na kuwa mtu wa amani na umoja. Mama Maria awasadie kwa hilo. Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru kwa kufika kwao. Amewatakia kila wema na kuwasindikiza katika sala na baraka zake. Amehitimisha kwa kuwaomba nao wasisahau kusali kwa ajili yake. Kwa sababu kazi hiyo sio rahisi.