Tafuta

Papa Francisko:heshima na hadhi kwa wazee ni muhimu!

Papa Francisko katika mwendelezo wa katekesi yake kuhusu Uzee,amebainisha kwamba jamii haizingatii kila mara kuwarudishia wazee wetu upendo uliopokelewa,kwa upole na heshima inayostahili.Familia zote zinaalikwa kuwapeleka watoto karibu na bibi na babu na kuwatembelea lakini sio kuwapuuza wakati wanapowapeleka katika vituo vya kutunzia au nyumba ya kustaafu.Wazee ni ustaarabu wetu

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa mara ya kwanza mara baada ya kipindi kirefu sana cha kukosa kukaa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kutokana na janga la uviko, Jumatano ya Pasaka tarehe 20 Aprili 2022, Baba Mtakatifu Francisko, ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliokusanyikakatika uwanja huo Vatican. Akianza mzunguko wake wa Katekesi  hiyo kuhusu uzee Papa amesema: “Leo hii kwa msaada wa Neno la Mungu lililosomwa, tunafungua hatua kupitia udhaifu wa umri wa uzee, ambao unajikita kwa namna ya pekee katika uzoefu wa upotevu na kuvunja moyo, kupoteza na kuachwa, kukata tamaa na mashaka. Bila shaka, uzoefu wa udhaifu wetu, unaokabiliwa na hali ya kushangaza wakati mwingine wa kutisha wa maisha, unaweza kutokea wakati wowote wa kuishi. Walakini, katika uzee wanaweza kuamsha hata hisia kidogo na kusababisha aina fulani ya mazoea hata kuudhika, kwa wengine. Papa Francisko amesema ni mara ngapi hali hiyo imesikika au kuifikiria kwamba “Waze wanasumbua au lakini wazee hawa daima wanaleta usumbufu”? Hayo tumesema na tumefikiria…”

Papa amerudi kufanya katekesi yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa amerudi kufanya katekesi yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Baba Mtakatifu amesema kuna majeraha makubwa zaidi ya utoto na ujana  ambayo husababisha hisia ya udhalimu na uasi, nguvu ya majibu na mapambano. Badala yake, majeraha, hata makubwa ya uzee yanaambatana na hisia kwamba, kwa hali yoyote, maisha hayajipingi yenyewe, kwa sababu tayari yameishi. Na kwa maana hiyo wazee wamewekwa kandoni kidogo hata kutoka katika uzoefu wetu pia tunataka kuwaweka mbali. Katika uzoefu wa kawaida wa binadamu, upendo kama wasemavyo ni urithi, haurudi nyuma ya maisha ambayo yako nyuma ya mabega na nguvu sawa kama yale maisha ya yule ambaye yuko mbele yetu. Upendo wa bure pia unaonekana katika hili na  wazazi wanajua kila wakati na wazee hujifunza kwa haraka. Pamoja na hayo, ufunuo huo unafungua njia ya urejesho tofauti wa upendo ni njia ya kuwaheshimu wale waliotutangulia. Namna ya kuwaenzi watu waliotutangulia  kutoka hapa ndiyo kuwaenzi wazee.

Papa amerudi kufanya katekesi yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa amerudi kufanya katekesi yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Upendo huo maalum ambao unafungua njia katika mtindo wa heshima yaani huruma na heshima wakati huo huo, hatia ya umri wa uzee imewekwa muhuri na amri ya Mungu. “Heshimu Baba na mama yako.  Ni juhudi kuu, ni ya kwanza kati ya pili ya amri kumi za Mungu. Hii si kusema baba tu na mama peke yake. Ni kwa kizazi na kizazi ambacho kitafuata  ambaye likizo yake pia inaweza kuwa ya polepole na ya muda mrefu na kuunda wakati na nafasi ya kuishi kwa muda mrefu na enzi nyingine za maisha. Kwa maneno mengine ni kuhusu uzee wa maisha. Heshimu ni neno zuri ili kutazama muktadha wa kurudisha upendo ambao unatazama umri wa uzee. Kwa maana ya kwamba tumepokea upendo wa wazazi, wa babu na bibi na sasa sisi tunatakiwa kuurudisha upendo huo kwao. Baba Mtakatifu Francisko amesema: "Leo tumegundua tena neno hadhi ili kuashiria thamani ya heshima na utunzaji wa maisha ya mtu yeyote. Hadhi kimsingi ni sawa na heshima: kuwaheshimu baba na mama, kuwaheshimu wazee ni kutambua hadhi walio nayo.

Baba Mtakatifu Francisko ameomba kufikiria vema mwinamo huo mzuri wa upendo ambao ni heshima. Utunzaji wenyewe wa wagonjwa, msaada wa wale wasiojitegemea, dhamana ya riziki, inaweza kukosa heshima. Heshima inashindikana wakati unakosa kujiamini na badala ya kuinamia kama unyeti na mapendo, upole na heshima, vinageuka kuwa ukali na upendeleo. Udhaifu unaposhutumiwa, na hata kuadhibiwa, kana kwamba ni kosa. Wakati upotovu na kuchanganyikiwa unapata mwanya wa dhihaka na uchokozi. Baba Mtakatifu Francisko amesema, inawezekana hadi kufikia kwenye kuta za nyumbani, katika nyumba za kutunza wazee, kama vile katika ofisi au katika nafasi zilizo za wazi katika mji. Kuwatia moyo vijana, hata kwa njia isiyo ya moja kwa moja, mtazamo wa kutosha na hata dharau, kwa uzee, udhaifu wao na hatari zao, huzalisha mambo ya kutisha.

Hii inafungua njia isiodhaniwa. Vijana ambao wanafikia hatua ya kuunguza blanketi ya maskini, kwa sababu wanamwona kama binadamu wa kubagua na mara nyingi kufikia  wazee kubaguliwa na tunakubaliana na hilo. Vijana ambao wanachoma blanketi ni kama kuanguka ncha  ya barafu; hiyo ni dharau kwa maisha ambayo, mbali na vivutio na misukumo ya ujana, tayari yanaonekana kama maisha ya ubadhirifu. Taka ni neno linaloonekana hapo. Ili kuwadharau wazee na kuwatupa kutoka katika maisha, kuwaweka kando, kuwatupa chini. Dharau hii, inayowavunjia heshima wazee, inatuvunjia heshima sisi sote. Ikiwa ninawadharau wazee, ninawajivunjia heshima. Kifungu kutoka katika Kitabu cha Sira kilichosikika mwanzoni ni kikali kwa haki dhidi ya fedheha hiyo, ambayo inalia kulipiza kisasi mbele ya Mungu. Kuna kifungu katika historia ya Nuhu ambacho kinaeleza sana kuhusu jambo hilo, Papa ameuliza kama wanayo kumbukumbu akilini. Mzee Nuhu, shujaa wa mafuriko na ambaye bado alikuwa ni mchapakazi, alijilaza baada ya kuwa amekunywa sana. Tayari ni mzee, lakini alikuwa akinywa pombe kupita kiasi.

Papa amerudi kufanya katekesi yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa amerudi kufanya katekesi yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Watoto wake, ili wasimwaibishe kwa aibu, walimfunika kwa upole, kwa macho yao yakitazama chini, kwa heshima kubwa. Andiko hilo ni zuri na linaeleza yote juu ya heshima inayostahili kwa wazee. Kufunika udhaifu wa wazee, ili wasifanye aibu. Ni andiko ambalo Papa amewashauri kusoma na litawafaa sana kutafakari. Licha ya riziki zote za zana ambazo jamii tajiri zaidi na zilizopangwa zaidi hufanyika na kuwekwa kwa uzee ambazo kwa hakika tunaweza kujivunia mapambano ya kurudi kwa aina hiyo maalum ya upendo ambayo ni heshima bado inaonekana kwa upande wa  Baba Mtakatifu kuwa dhaifu na isiyofaa. Kwa maana hiyo ni lazima tufanye kila kitu, tuuunge mkono na kutia moyo, tukitoa usaidizi bora wa kijamii na kiutamaduni kwa wale ambao ni nyeti katika aina hii ya maamuzi ya ustaarabu wa upendo.

Kufuatia na hiyo Baba Mtakatifu Francisko ameomba ruhusa  kuwashauri wazazi kwamba wawakaribie watoto, vijana na wazee daima. Mzee anapougua na kichwa kuwa nje, daima akaribiwe, kwa utambuzi kwamba huu ni mwili wetu ambao mwanzo ulikuwa na uwezo kama tulivyo nao. Papa amesisitiza kwamba wasiweke wazee kandoni. Na ikiwa hakuna uwezekano wa kukaa nao na kuwapeleka kwenye nyumba za wazee, basi waende kuwatembelea, na kuwapelekea watoto wao pia. Wazee waliotufungulia milango ni heshima ya ustaarabu wetu. Mara nyingi watoto wanasahau hilo. Papa amewaeleza jambo moja kwamba yeye alipokuwa Buenos Aires, nchini Argentina alipendelea kutembelea nyumba za wazee. Mara nyingi alikwenda kutembelea kila mmoja na anakumbuka kuwa siku moja alimuuliza mwamke mmoja, ana watoto wangapi, akamjibu wanne na wote wameolewa na wana wajuu na hivyo alianza kusimulia juu ya familia yake. Papa aliuliza kama wao wanakwenda kumtembelea na yeye alijibu  ndiyo wanakwenda daima. Lakini alipotoka nje ya chumba hicho, muuguzi aliyekuwa anasikiliza maongezi hayo, alimwambiwa kuwa amemsimulia uongo ili kufunika watoto wake. Kwani ilikuwa ni miezi sita bila kuona mtu yeyote pale.

Papa amerudi kufanya katekesi yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa amerudi kufanya katekesi yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Papa ameongeza kusema:“hii ni kubagua wazee ni kufikiria kwamba wazee ni mambo ya kubagua. Hii ni dhambi kubwa! Amri kuu ya kwanza ndiyo hii ambayo ni ya  pekee isemayo tuzo: “Waheshimu baba yako na mama yako nawe utakuwa na maisha marefu duniani”. Amri hii ya kale ya kuheshimu inatupatia baraka, ambayo inatumika hivi: “Utakuwa na maisha marefu.” Kwa maana hiyo amesisitiza zaidi  Papa kwamba wathamini wazee. Na ikiwa watapoteza akili zao, wathamini tu wazee, kwa sababu wao ni uwepo wa historia, uwepo wa familia yangu, na shukrani kwao ninaishi hapa; na  sote tunaweza kusema, asante babu na bibi, niko hai. Papa ameshihi wasiaachwe peke yao. Suala la kutunza wazee, sio suala la vipodozi na upasuaji wa kiplastiki: hapana. Badala yake,ni suala la heshima, ambalo linapaswa kubadilisha elimu ya vijana kuhusu maisha na awamu zake. Upendo kwa mwanadamu ambao ni wa kawaida kwetu, pamoja na heshima kwa maisha yaliyo hai, sio suala la wazee. Badala yake, ni shauku ambayo itawafurahisha vijana ambao hurithi sifa zake bora zaidi. Hekima ya Roho wa Mungu ituruhusu kufungua upeo wa mapinduzi haya ya kiutamaduni ya kweli kwa nguvu muhimu,  amehitimisha.

KATEKESI YA PAPA FRANCISKO 20.04.2022 KATIKA UWANJA WA MTAKATIFU PETRO
20 April 2022, 11:40