Tafuta

Misa ya Huruma ya Mungu Dominika ya Pili ya Pasaka Misa ya Huruma ya Mungu Dominika ya Pili ya Pasaka 

Misa ya Huruma ya Mungu itafanyika katika Kanisa la Mt.Petro

Kwa miaka miwili ya mwisho kuanzia 2020 katikati ya janga la Uviko,Papa Francisko likuwa amefanya misa ya faragha katika Kanisa la Roho Mtakatifu,Sassia.Ni misa iliyoanizhswa na Mtakatifu Yohane Paulo II.Ni sehemu ya Ibada kwa mujibu wa maelezo ya Mtakatifu Sr Faustina Kowalska aliyepata maono na kutumwa na Yesu kuadhimisha Siku Kuu katika Dominika ya Pili ya Pasaka.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baada ya miaka miwili ya mwisho ya maadhimisho ya faragha katika Kanisa la Roho Mtakatifu huko Sassia, Misa ya Papa Francisko hatimaye itaadhimishwa kwa mara ya kwanza kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro Vatican  kwa uwepo wa waamini katika Dominika iliyowekwa wakfu kwa ajili ya  Huruma ya Mungu iliyoanzishwa miaka na Mtakatifu Yohane Paulo II katika Dominika ya Pili ya Pasaka. Kwa mujibu wa taarifa  kutoka Ofisi ya Maadhimisho ya Kiliturujia ya Kipapa  ni kwamba misa hoyo itafanyika tarehe 24 Aprili kuanzia saa 4 asubuhi. Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 20 Aprili 2022  mara baada ya katekesi yake akisalimia mahujaji wa Poland, alisema Kristo anatufundisha kuwa mwanadamu si tu anafanya uzoefu wa huruma ya Mungu, lakini anaitwa hata kuonesha kwa jirani, huku akiwashukuru kwa huruma hiyo kuelekeza kwa wakimbizi wengi kutoka Ukraine, ambao wamepata milango iliyo wazi na mioyo ya ukarimu nchini Poland.

Papa wakati wa misa katika Madhabahu ya Huruma katika Kanisa la Roho Mtakatifu huko Sassia Roma
Papa wakati wa misa katika Madhabahu ya Huruma katika Kanisa la Roho Mtakatifu huko Sassia Roma

Hata hivyo Papa Francisko anayo ibada kuu ya Huruma ya Mungu katika mchakato wa upapa wake hadi kufikia kutoa mada kuu msingi wa Jibilei ya huruma mnamo 2016. Kwa kuwa na mwendelezo wa  urithi wa Karol Wojtyla , yaani Mtakatifu Yohane Paulo II aliyeanzisha sikukuu hii kwa ajili ya Kanisa duniani kote mnamo mwaka 2000 sanjari na Domenica in albis, Dominika  ya kwanza baada ya Pasaka. Tarehe ambayo, kulingana na maono ya fumbo lwa  Mtakatifu wa Kipoland Sr Faustina Kowalska, ni kwamba Yesu mwenyewe ndiye aliyemuomba na kumpa maelekezo  jinsi ya kuchora picha ambayo ilipata umaarufu duniani kote.  “Ninataka kuwe na sikukuu ya huruma. Ninataka picha, ambayo utaipaka rangi kwa brashi, ibarikiwe sana katika Dominika ya kwanza baada ya Pasaka; Dominika  hii lazima iwe sikukuu ya Huruma”,  tunasoma katika Shajara maarufu ya Sr.  Faustina, iliyetangazwa na Yohane Paulo II mnamo 1993  kuwa mwenye heri na kutangazwa kuwa mtakatifu mwaka 2000. Kwa maneno  ya mtawa wa kipoland  kuhusu maagizo ya Yesu anaandika kuwa “Natamani kwamba Sikukuu ya  huruma  iwe kimbilio na kimbilio la roho zote na hasa kwa wenye dhambi maskini ... Nafsi inayokaribia maungamo na Muungano Mtakatifu unapokea msamaha kamili wa dhambi na uchungu ”.

Papa wakati wa misa katika Madhabahu ya Huruma katika Kanisa la Roho Mtakatifu huko Sassia Roma
Papa wakati wa misa katika Madhabahu ya Huruma katika Kanisa la Roho Mtakatifu huko Sassia Roma

Mtakatifu Faustina alikuwa wa kwanza kusherehekea sikukuu hii kibinafsi kwa idhini ya muungamishi wake. Lakini tayari mnamo 1944 ibada ya Huruma  ya Mungu ya Dominika ya  kwanza baada ya Pasaka ilikuwa inafanyika  katika Madhabahu ya  Krakow, Lagiewniki baadaye ikaenea Poland yote katika miaka iliyofuata. Tena Wojtyla, kama Papa, aliyejitolea kwa ibada iliyohamashwa na Sr Faustina  katika Kanisa la Roho Mtakatifu  huko Sassia, Roma  mahali pa ibada tangu karne ya 16 ni hatua chache kutoka Uwaja wa Mtakatifu Petro. Tangu 1994 Kanisa hilo limeinuliwa kuwa madhabahu na kila mwezi ni marudio ya mahujaji na waamini ambao husali Rozari hapo kila alasiri.

Papa akiwa anasali  katika Madhabahu ya Huruma katika Kanisa la Roho Mtakatifu huko Sassia Roma
Papa akiwa anasali katika Madhabahu ya Huruma katika Kanisa la Roho Mtakatifu huko Sassia Roma

Ni katika madhabahu hayo ya Roho Mtakatifu, Sassia ambapo Papa Francisko mwaka jana 2021, katika kumbukumbu ya miaka 90 ya kufunuliwa kwa sura ya Yesu Mwenye Huruma, aliongoza Misa ya Huruma ya Mungu, hata hivyo kwa namna iliyowekewa vikwazo kwa kufuata kanuni za kupambana na UVIKO19, katika kuwepo na  kundi la wageni wa magereza, madaktari na wauguzi na wakimbizi kutoka Afrika na Mashariki ya Kati tu. Hiyo ya 2021 ilikuwa Misa ya tatu ya Papa  ya  Huruma ya Mungu; ya kwanza ilikuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,mnamo  tarehe 3 Aprili 2016, katikati ya Jubilei Maalum ya Huruma.  Upendeleo wa  ulimwengu wote ambapo Papa alithibitisha tena ujumbe wa upendo wa kimungu: “Kila udhaifu unaweza kupata msaada wa ufanisi katika huruma ya Mungu. Huruma  yake, kiu kweli, haikomi kwa mbali: inataka kukutana na umaskini wote na watu huru kutoka kwa wengi, kwani  aina za utumwa zinatesa dunia yetu. Mungu anataka kuyafikia madonda ya kila mmoja, awaponye. Kuwa mitume wa huruma maana yake ni kugusa na kubeba majeraha yake, yaliyopo hata leo katika mwili na roho ya ndugu zake wengi sana”.

Mtakatifu Faustina Kowalska
Mtakatifu Faustina Kowalska

Mwaka uliofuata, 2017, Papa Francisko alisherehekea hapo kwa kufanya masifu  ya kwanza ya jino katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Wakati mnamo 2020, katikati ya janga la uviko alirudi katika Kanisa la Roho Mtakatifu kwa sherehe ya kibinafsi, bila waamini. Wakati ulimwengu ulikuwa ukipambana na dharura ya kiafya ya ghafla na hofu ya vifo na maambukizi. Kwa maana hiyo Papa wakati wa Misa iliyotangazwa ulimwenguni kote na kwa lugha kadhaa  alikuwa ametuhimiza tena kutazama huruma ya  Mungu, mkono unaoinua kila wakati kwa ajili yetu sisi na, wakati huo huo, alikuwa ameonya dhidi ya hatari kuwa na pigo jingine la virusi vya ubinafasi na kutokujali ambayo inasababisha kuwatupilia mbali ndugu zetu  mwenyewe.

21 April 2022, 16:57