Maadhimisho ya Pasaka ya Bwana, yalete mang’amuzi na maisha mapya miongoni mwa wafuasi wake. Maadhimisho ya Pasaka ya Bwana, yalete mang’amuzi na maisha mapya miongoni mwa wafuasi wake.  

Kipindi Cha Pasaka Ni Wakati Wa Kuimarisha Fadhila Za Kristo.

Maadhimisho ya Pasaka yalete mang’amuzi na maisha mapya. Kristo Mfufuka awe ni chemchemi furaha ya kweli na upendo wenye huruma ndani ya familia. Katika kipindi hiki cha Pasaka ya Bwana, bado kuna watu wengi wamegubikwa na vita, maambukizi makubwa ya Virusi vya Korona, UVIKO-19, uchafuzi mkubwa wa mazingira nyumba ya wote; njaa na utapia mlo wa kutisha.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 27 Aprili 2022 amesema, katika Kipindi hiki cha Sherehe ya Pasaka ya Bwana, Liturujia ya Neno la Mungu inaendelea kuonesha jinsi ambavyo Kristo Mfufuka alivyowatokea watu mbalimbali ili kuwaimarisha katika imani, matumaini na mapendo. Maadhimisho ya Pasaka ya Bwana, yalete mang’amuzi na maisha mapya miongoni mwa wafuasi wake. Kristo Mfufuka awe ni chemchemi furaha ya kweli na upendo wenye huruma ndani ya familia. Katika kipindi hiki cha Pasaka ya Bwana, bado kuna watu wengi wamegubikwa na vita, maambukizi makubwa ya Virusi vya Korona, UVIKO-19, uchafuzi mkubwa wa mazingira nyumba ya wote; njaa na utapia mlo wa kutisha.

Bado kuna athari kubwa za Ugonjwa wa UVIKO-19

Huu ni mwaliko kwa waamini kuendelea kusali ili kuombea amani duniani. Lengo ni kuhakikisha kwamba, mashambulizi ya silaha za kivita yanakoma. Viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa wenye madaraka ya kusitisha vita wahakikishe kwamba, wanatekeleza vyema dhamana na wajibu wao, kwa kusikiliza na kujibu kilio cha walimwengu wanaotaka amani duniani. Amewatakia heri na baraka tele wajumbe wa vikosi vya ulinzi na usalama kutoka Ukraine walioshiriki kwenye katekesi tarehe 27 Aprili 2022. Hata katika shida, magumu na changamoto za maisha, wajitahidi kukutana na Kristo Mfufuka, anayewawashia moto wa Injili ili hatimaye, waweze kuwa ni mashuhuda wa imani, matumaini na mapendo huku, wakiendelea kutangaza na kushuhudia matendo makuu ya Mungu katika maisha. Wajitahidi kuwa ni mashuhuda na vyombo vya amani katika jamii na ulimwengu katika ujumla wake.

Madhara ya vita kati ya Urussi na Ukraine ni makubwa sana.
Madhara ya vita kati ya Urussi na Ukraine ni makubwa sana.

Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru kwa namna ya pekee kabisa watu wa Mungu kutoka Vignale Monferrato, waliochanga fedha, kielelezo cha mshikamano na upendo wa kidugu na kuhakikisha kwamba, John Baldri aliyekuwa na umri wa miaka 25 kutoka Ghana aliyekuwa kufani na akatamani kufia nchini mwake, mikononi mwa wazazi wake, anarudishwa nyumbani kwao. Kipindi hiki cha Pasaka, ni wakati muafaka wa kutafakari Fumbo la Pasaka, yaani: mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu kutoka kwa wafu, chemchemi ya maisha mapya, kuelekea kwenye wokovu na uzima wa milele. Hiki ni kipindi cha kuimarisha imani na matumaini na kwamba, ni dhamana na wajibu wa wanandoa wapya kusimika maisha na utume wao katika kweli na tunu msingi za Kiinjili.

Ushuhuda

 

 

 

27 April 2022, 16:18