Tafuta

Jumuiya ya Kimataifa imeadhimisha Siku ya Magonjwa Adimu, tarehe 28 Februari 2022 kwa kunogeshwa na kauli mbiu: “Usawa wa watu wanaoishi na magonjwa adimu.” Jumuiya ya Kimataifa imeadhimisha Siku ya Magonjwa Adimu, tarehe 28 Februari 2022 kwa kunogeshwa na kauli mbiu: “Usawa wa watu wanaoishi na magonjwa adimu.” 

Siku ya Magonjwa Adimu Duniani: Mshikamano Wa Huduma ya Upendo

Papa Francisko aliwakumbuka na kuwaombea wagonjwa wanaoteseka kutokana na magonjwa adimu. Amevitia shime, ari na moyo mkuu vyama vyote vinavyowahudumia wagonjwa wenye magonjwa adimu kuendeleza upendo na mshikamano. Amewataka wataalam katika sekta afya sanjari na watafiti kuendeleza huduma na tafiti zao kama sehemu ya huduma kwa wagonjwa hawa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Jumuiya ya Kimataifa imeadhimisha Siku ya Magonjwa Adimu, tarehe 28 Februari 2022 kwa kunogeshwa na kauli mbiu: “Usawa wa watu wanaoishi na magonjwa adimu.” Jumuiya ya Kimataifa haina budi kuendeleza elimu na uragibishaji kuhusu magonjwa adimu ili kuleta tofauti kwa watu zaidi ya milioni mia tatu wanaoteseka kutokana na magonjwa adimu sehemu mbalimbali za dunia. Magonjwa adimu yanawasibu watu wachache sana yaani watu 10 kati ya watu 10, 000. Mfano wa magonjwa haya kadiri ya wataalamu ni ulegevu wa misuli. Haya ni magonjwa yanayosababishwa na itililafu za kijenetiki. Kuna magonjwa takribani 7, 000 ambayo ni adimu na kwamba kuna aina 500 za Saratani ambazo pia ni adimu. Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 27 Februari 2022 wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, aliwakumbuka na kuwaombea wagonjwa wanaoteseka kutokana na magonjwa adimu pamoja na familia zao. Amevitia shime, ari na moyo mkuu vyama vyote vinavyowahudumia wagonjwa wenye magonjwa adimu sehemu mbalimbali za dunia, kuendeleza upendo na mshikamano huu wa udugu wa kibinadamu. Amewataka wataalam katika sekta afya sanjari na watafiti kuendeleza huduma na tafiti zao kama sehemu ya huduma kwa wagonjwa hawa.

Magonjwa mengi adimu ni kutokana na itilafu za kijenetiki
Magonjwa mengi adimu ni kutokana na itilafu za kijenetiki

Kwa upande wake, Kardinali Michael F. Czerny, S.J. Mwenyekiti wa muda wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu na Fungamani ya Binadamu katika ujumbe mahususi kwa maadhimisho haya anasikitika kusema kwamba, matibabu ya magonjwa haya ni ghali sana. Serikali nyingi zimewekeza kidogo sana katika tafiti, tiba na huduma kwa wagonjwa hawa ikilinganishwa na mahitaji halisi. Waathirika wakuu ni maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Kumbe, kuna haja ya kuwa na mwelekeo na mtazamo mpya kisiasa, kiuchumi na kiafya, ili kuhakikisha kwamba, huduma kwa wagonjwa wenye magonjwa adimu inakuwa ni endelevu na fungamani, kwa kung’oa tabia ya uchoyo na ubinafsi, ili hatimaye, kukuza na kudumisha utamaduni wa kuwakubali na kuwapokea wengine jinsi walivyo, kwa kuimarisha mshikamano wa udugu wa kibinadamu, daima mafao ya wengi yakipewa kipaumbele cha kwanza.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, mwelekeo huu unapaswa pia kudumishwa katika sekta ya elimu, ili watoto ambao wameathirika kwa magonjwa adimu waweze kupata elimu na tiba muafaka. Pale inapowezekana, familia zenye wagonjwa kama hawa zipewe ruzuku, ili kukabiliana na changamoto za kila siku katika huduma. Jumuiya ya Kimataifa haina budi kujielekeza zaidi katika maboresho ya mazingira ya mahali pa kazi, ili kujenga na kudumisha utamaduni unaosimikwa katika haki, usawa pamoja na kuwajumuisha watu wote, kwa ajili ya ulimwengu endelevu. Baba Mtakatifu Francisko anasema, ujenzi wa utamaduni wa udugu wa kibinadamu ni muhimu sana katika mchakato wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazomsibu mwanadamu katika ulimwengu mamboleo.

Magonjwa Adimu

 

04 March 2022, 15:00